Katika kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo mauaji, Waziri wa Mambo ya Ndani akutana na viongozi wa Dini

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,925
12,202
Katika kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayotokea katika jamii, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefanya Kikao Maalumu na Viongozi wa Dini lengo ikiwa kuhusisha kundi hilo maalumu katika kudhibiti matukio ya uhalifu ikiwemo mauaji, mmomonyoko wa maadili, matumizi ya dawa za kulevya na matukio mengine yanayoweza kuvuruga amani ya nchi.

Akizungumza katika Kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya wizara Mtumba Jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amewaomba viongozi hao wa dini kuendelea kuisaidia serikali katika kudumisha amani na usalama huku akiwaomba kutochoka kutoa ushauri kwa serikali katika kudhibiti matukio ya uhalifu yanayoweza kuvuruga amani ya nchi.


Wakizungumza wakati wa kikao hicho viongozi hao wa dini walitoa maoni mbalimbali huku wakisisitiza uwepo wa amani ndio nguzo ya maendeleo na wakiishukuru Wizara kuona ipo haja ya kuwahusisha katika kudhibiti masuala ya uhalifu.


 
Dini haina mvuto,dini imeshadharaurika,imebaki kuwa genge la wanafiki na majambazi..imalisheni ustawi wa jamii na usimamizi wa sheria ,dini zinazidi kupoteza mvuto kila siku.
 
Muuaji mkubwa ni polisi sasa hao viongozi wana hitajikaje kutoa elimu kwa waumini?. Baada ya serikali kusimamia sheria na haki ya raia wake.
 
Back
Top Bottom