Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,555
- 1,153
Kufuatia agizo lililotolewa na Serikali kupitia kwa Waziri wa TAMISEMI nchini Mhe Mohamed Omary Mchengerwa,
Agizo hilo limeitaka DART kuhakikisha inakamilisha taratibu zote za Ubia na Mbia wa UDART ndani ya miezi Saba.
Mkurugenzi wa Ubia nchini PPP Bwana David Kafulila amesema ndani ya muda mfupi ujao watakuwa tayari wamekamilisha mkataba baina ya DART na Mbia ili kuhakikisha Wananchi wa Dar es Salaam hawapati adha ya usafiri na Usafirishaji.
Kafulila amesema, Mbia huyo wa UDART atanunua Mabasi yeye mwenyewe na atayaendesha kwa Ubia na Serikali katika kipindi Cha mkataba na hivyo kuifanya gharama ya usafiri kuwa nafuu Kwa wananchi na wakazi wa Jiji la Dar es salaam.
Kafulila amesema kuwa 40% tu ya wafanyakazi waishio Dar es salaam ndio wanakwenda kazini kwa miguu ( working distance).
Hivyo zaidi 60% wanafanya kazi sehemu ambazo wanalazimika kulipa nauli kila siku ili kwenda kazini na kurudi nyumbani.
Nia ya Serikali ikiwa ni kutoa unafuu wa gharama za Usafiri na usafirishaji Kwa Wananchi hasa wakazi wa Jiji la Dar es salaam.
Musukuma: Serikali iache kufanya Biashara haiwezi, Mwendokasi Walikuwa na Mabasi 300 yamebaki 4 tu. Biashara mtuachie Watoto wa Mjini!
Mbunge wa Geita vijijini mh Msukuma ameishauri serikali iachane na kufanya Biashara na badala yake Biashara ziachiwe sekta binafsi Dr Msukuma alikuwa analia na kampuni ya Tanoil ambayo CAG ameripoti inalitia Taifa Hasara ya mabilioni kila mwaka. "Nilionya hapa kuhusu Tanoil hamkunielewa na...
www.jamiiforums.com