JWTZ liwe na kitengo cha elimu kwa raia, kuna upotoshaji mkubwa kulihusu

Wiki iliyopita katika mizunguko yangu ya kusaka noti nilipanda daladala iliyokatiza Kurasini, kuna mahali magari yakasimama kuruhusu wanajeshi wengi waliokuwa wakivuka barabara kwa makundi huku wakiimba nyimbo zao.

Kama mnavyojua Watanzania ni watu wanaopenda na wazuri sana kuanzisha soga popote hata kama hawafahamiania, basi soga au stori za kupoteza muda kuhusu jeshi na wanajeshi zikaanza kwa mshwashwa mkubwa kila upande,

Wa kwanza niliyemsikia alikuwa ni kondokta, yeye alisema hao ndio wenye nchi yao tutulie tu wapite hatuwezi kushindana nao.

Mzee Mwingine aliyevalia kaunda suti wa miaka kama 55 hivi akasema tuogope sana watu waliofundishwa kuua tu, hao ni watu huwezi kushindana nao kabisa!, alikuwa akiyarudia haya maneno kila mara. Pia akaongezea hao watu wakipewa amri ya kuua mahali popote ni lazima kutekeleza bila kuhoji!

Mwanaume mwingine wa makamo akasema hapo huwezi kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke, cha ajabu mimi nilikuwa naona tofauti hiyo tena niliona mabinti wengi tu warembo sana katik hao wanajeshi.

Mwingine alisema kukitokea taharuki au sintofahamu yoyote kubwa katika nchi wao ndio kila kitu na hadi polisi wanageuka kuwa raia!

Katika hayo mastori pia kulitokea jinsi gani zamani wanajeshi walivyokuwa wababe wakichapa watu mitaani.

Mwingine akasema jeshini hakuna sheria ni amri tu!

Itoshe kusema mengi niliyoyasikia yalikuwa ni upotoshaji mkubwa, mtazamo finyu, uongo na chumvi nyingi kuhusu jeshi. Mastori ya aina hii yamejaa mitaani na kwenye vijiwe vya kahawa, hiyo inamaanisha jeshi linahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu kwa raia kuwapa mwanga kidogo kuhusu historia, maisha ya wanajeshi na majukumu muhuimu ya jeshi ili kuondokana na vihiyo makanjaja wapotoshaji
Asante kwa mada hii. Nashauri elimu kuhusu jeshi isitolewe bali tubaki na uelewa huohuo ndiyo lina make sense.

TPDF siyo kama TTCL au VODACOM au TANESCO kila mtu alijuwe. Hivyo ndivyo jeshi linapaswa kuwa. Yaani lisizoeleke kabisa ndiyo ufanisi wake utakuwa mkubwa.
 
Wiki iliyopita katika mizunguko yangu ya kusaka noti nilipanda daladala iliyokatiza Kurasini, kuna mahali magari yakasimama kuruhusu wanajeshi wengi waliokuwa wakivuka barabara kwa makundi huku wakiimba nyimbo zao.

Kama mnavyojua Watanzania ni watu wanaopenda na wazuri sana kuanzisha soga popote hata kama hawafahamiania, basi soga au stori za kupoteza muda kuhusu jeshi na wanajeshi zikaanza kwa mshwashwa mkubwa kila upande,

Wa kwanza niliyemsikia alikuwa ni kondokta, yeye alisema hao ndio wenye nchi yao tutulie tu wapite hatuwezi kushindana nao.

Mzee Mwingine aliyevalia kaunda suti wa miaka kama 55 hivi akasema tuogope sana watu waliofundishwa kuua tu, hao ni watu huwezi kushindana nao kabisa!, alikuwa akiyarudia haya maneno kila mara. Pia akaongezea hao watu wakipewa amri ya kuua mahali popote ni lazima kutekeleza bila kuhoji!

Mwanaume mwingine wa makamo akasema hapo huwezi kutofautisha kati ya mwanaume na mwanamke, cha ajabu mimi nilikuwa naona tofauti hiyo tena niliona mabinti wengi tu warembo sana katik hao wanajeshi.

Mwingine alisema kukitokea taharuki au sintofahamu yoyote kubwa katika nchi wao ndio kila kitu na hadi polisi wanageuka kuwa raia!

Katika hayo mastori pia kulitokea jinsi gani zamani wanajeshi walivyokuwa wababe wakichapa watu mitaani.

Mwingine akasema jeshini hakuna sheria ni amri tu!

Itoshe kusema mengi niliyoyasikia yalikuwa ni upotoshaji mkubwa, mtazamo finyu, uongo na chumvi nyingi kuhusu jeshi. Mastori ya aina hii yamejaa mitaani na kwenye vijiwe vya kahawa, hiyo inamaanisha jeshi linahitaji uwekezaji mkubwa katika elimu kwa raia kuwapa mwanga kidogo kuhusu historia, maisha ya wanajeshi na majukumu muhuimu ya jeshi ili kuondokana na vihiyo makanjaja wapotoshaji
Ikiwa uliona wasichana warembo hukuelewa mada!
 
Haya ni mawazo ya kizamani kabisa ila ndivyo watanzania wengi wanavyoamini. Mtu kama wewe akija mwanajeshi na kukumbia uvue suruali umridhishe haja zake bila shaka utakubali bila kinyongo ukidhani ni jukumu lako kufanya hivyo
Utakubali tu kama wewe ni shoga. TPDF wamefundishwa nidhamu ya hali ya juu. Na ukigundulika kuwa ni shoga au tasa huajiliwi kule
 
Kuna nchi nyingi tu duniani hazina majeshi,
Umekariri au kukaririshwa vibaya.

Hakuna nchi isiyo na jeshi Mkûu.
Jeshi ndio nchi.
Nènda kavamie alafu utajua hizo unazoambiwa hazina jeshi zinazo au hazina.

Ukisema nchi haina jeshi unamaanisha nchi haina ulinzi na usalama

Achana na maneno ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom