Jina la Mtoni kwa Aziz Ali limetoka wapi?

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,498
3,464
JINA LA MTONI KWA AZIZ ALI LIMETOKEA WAPI!?

Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, kuna eneo linaitwa Mtoni. Mtoni yenyewe nayo ina mitaa mingi ikiwamo Mtoni Kijichi, Mtoni Mtongani, Mtoni kwa Chaurembo, Mtoni kwa Mwenye Kuuchimba na Mtoni kwa Aziz Ali.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam haswa wenye kuishi maeneo ya Mtoni, barabara ya Kilwa mpaka Mbagala jina ili la Mtoni kwa Aziz Ali, si jina geni.

Hapo Mtoni kwa Aziz Ali, siku nyingi nyuma alipata kuishi bwana mmoja aliyekuwa mmoja wa Waafrika matajiri sana kupata kutokea wakati huo wa ukoloni nchini Tanganyika. Aliitwa Ali Dossa Kidonyo na kwa hiyo kutokana na umaarufu wake, mahala hapo pakaitwa Mtoni Kwa Aziz Ali.

Aziz Ali, alikuwa Mdigo aliyetokea sehemu za Tanga na kuja kuweka kambi mjini Mzizima (sasa Dar es salaam), mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.

Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizoanzia kufanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi na kuajiri mafundi kadhaa.

Aziz Ali alijitengenezea umaarufu kutokana na kwamba aliweza kumiliki majumba mengi na magari ya biashara (yaani malori ya mchanga) pamoja na ya kutembelea, na vitu vingine kadhaa, kutokana na kazi yake ya kuwa mtaalamu wa kujenga nyumba (building contractor).

Hili jina la Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.

Huyu Aziz Ali alikuwa mwamba katika miamba ya Dar es Salaam. Alikuwa tajiri ,contractor,' wa kujenga, majumba, Mwafrika wa kwanza kununua magari na kujenga nyumba ya vigae na vioo Mtoni.

Yeye alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa muda hadi atakapoweza.

Nyumbani kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.

Nyumba hii hadi leo ipo na sehemu hiyo kandokando ya barabara ya Kilwa na ndipo hapo pakaja kuitwa Mtoni kwa Aziz Ali.

Lakini katika sifa hizi sifa yake kubwa sana Aziz Ali ilikuwa ujenzi wa misikiti na kuihudumia misikiti. Hii ilikuwa miaka ya 1930 na hapakuwa na umeme Kariakoo.

Misikiti ilikuwa ikitumia karabai kuonea. Aziz Ali yeye alinunua karabai kwa kila msikiti na ikifika Maghrib mwanae Hamza alikuwa akizitia mafuta na kuziwasha kisha akizipeleka kila msikiti tayari kwa sala ya Maghrib.

Inapomalizika sala ya Isha alikuwa anapita tena katika ile misikiti kukusanya karabai zake na kurudi nazo nyumbani kwao Mtaa wa Mbaruku na Kongo.

Mzee Aziz Ali alikuwa na nyumba nyingi sana Dar es Salaam na ndiyo zilikuwa moja ya utajiri wake. Katika nyumba hizi nyumba ambayo imaecha historia ya pekee ni hii nyumba ya Mtaa wa Mbaruku na Congo.

Nyumba hii ilikuwa moja ya sehemu ambazo harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika zilianzia hapo. Nyumba nyingine ilikuwa Mtaa wa Kipata kwa Ally Sykes, hapo zamani lilipokuwa duka la baba yake na barza ya wazee.

Nyumba nyingine ilikuwa Stanley Street kwa Abdul Sykes. Nyumba hii ilikuwa pia ya Kleist na kulikuwa na duka la vifaa vya ujenzi katika uhai wake.

Mzee Azizi Ali alitoa mchango mkubwa sana katika harakati za uhuru wa nchi hii kwa kujitolea mali zake na nguvu zake mfanyabiashara na aliyemiliki kampuni ya ujenzi wa nyumba, yetu yeye ndie alikua mjenzi miaka hiyo na nyumba nyingi tu mjini mitaa ya Kariakoo yeye alikua amezijenga tena kwa kumlipa kidogo na baadae kummalizia malipo yake kwa makubaliano maalum na wala hajawahi kumshtaki mtu kumcheleweshea malipo yake.

Ndipo kutokana na ukarimu wake mkubwa wakamwita "Aziz" yaani "Kipenzi." Ikawa wakimtaja jina wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali." Kiasi ikapelekea jina lake la Kidonyo likafa kabisa. Kwa hakika Aziz Ali alikuwa mcha Mungu sana.

Mzee Aziz Ali alipokufa mwaka wa 1951 miaka miwili baada ya kifo cha rafiki yake Kleist gazeti la Tanganyika Standard liliandika kifo chake kwa maneno haya: 'Aziz Ali the Builder of Mosques is Dead,' yaani, Aziz Ali Mjenzi wa Misikiti Amekufa.'

Alipofariki Mzee Aziz Ali, biashara zake ziliendelezwa na Mmoja wa watoto zake, Dossa Aziz Ali, na hata zile harakati za uhuru alijihusisha nazo tena kwa undani zaidi.

Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka wa 1950. Mambo yalipamba moto sana kuanzia mwaka huo pale vijana wazalendo walipoanza kufanya mipango ya kuunda chama cha siasa halisi kupambana na ukoloni wa Muingereza.

Nyumba zlizokuwa anamiliki Mzee Aziz Ali ndizo zikawa nyumba ambazo Nyerere alikuwa akifikia kuanzia mwaka wa 1952 kila anapokuja mjini kutokea Pugu alipokuwa akifundisha.

Dossa Aziz Ali (Mtoo wa Aziz Ali), alikuwamo katika kuasisi vyombo vyote vya mwanzo vinavyonasibishwa na harakati za kumng’oa Mkoloni, kama vile TAA na TANU akiwa Afisa na Mjumbe mwanadamizi aliye na sauti - hili sawa; hili fanya; hili wacha na mambo yakawa hivyo asemavyo.

Dossa, kwa kushirikiana na mwanachama mwengine Alexander Tobias, walichaguliwa na wenzao wakati fulani wawe makatibu wa pamoja wa muhtasari.

Harakati ziliposuasua alikuwa hachoki kuwapitia wenzake na kuwakumbusha majukumu waliyopeana akienda kwa mmoja mmoja nyumbani kwake kwa kutumia gari lake na kutaka kujua kulikoni mambo hayendi ipasavyo.

Katika siku za mwanzo za harakati, chama cha TAA na baadaye TANU havikuwa na uwezo wa kifedha wa kujiendeshea mambo yake hata kidogo.

Tegemeo lao kubwa lilikuwa ni kwa watu kama akina Dossa Azizi, aliyekuwa mkurugenzi na msimamizi mkuu wa biashara na mali za babake.

Wengine ni Mzee John Rupia na wale akina Sykes watatu (Abdul, Ally na Abbas), ambao baba zao walikuwa na uwezo wa fedha, ‘wawapige jeki’ (wachangie pakubwa).

Habari zinasema, ilikuwa ni Dossa Aziz aliyemwomba Nyerere kuacha tena kuvaa kaptura mbele ya wazee, kwani sasa ameshakuwa kiongozi ambaye atakuwa akikutana na watu wazima na hivyo si vizuri kuonekana na kaptura na stockings (zile soksi ndefu mpaka magotini).

Mzee Dossa alifanikiwa katika hilo kwani alimnunulia pia Nyerere suti kadhaa maridadi katika safari yake ya kule UNO -Umoja wa Mataifa (wakati ule), ili kupeleka kilio cha Watanganyika kudai nchi yao.j
 
Sawa

"ᵂᵒʳʳʸ ⁱˢ ᵃ ʷᵒʳᵈ ᵗʰᵃᵗ ᴵ ᵈᵒⁿᵗ ᵃˡˡᵒʷ ᵐʸˢᵉˡᶠ ᵗᵒ ᵘˢᵉ"
 
...kazi yake ya kuwa mtaalamu wa kujenga nyumba (building contractor).

... Alikuwa tajiri ,contractor,' wa kujenga, majumba,

... aliyemiliki kampuni ya ujenzi wa nyumba, yetu yeye ndie alikua mjenzi miaka hiyo na nyumba nyingi tu mjini mitaa ya Kariakoo yeye alikua amezijenga

Mkandarasi Ustaadhi Azizi Ali Dossa Kidonyo binafsi alipokuwa skuli alijikita kwenye taaluma gani zaidi, civil engineering ama architectural engineering?
 
ndio tabu ya mswahili yaani anajiona yeye anajuwa kuliko wenzie, sa civil au archt zitajibiwa na nani mtoa uzi au mweneye Ali. badala ya kuwaza mafanikio yake we unawaza elimu.
 
sa civil au archt zitajibiwa na nani mtoa uzi au mweneye Ali. badala ya kuwaza mafanikio yake we unawaza elimu.

Mkandarasi Ustaadhi Azizi Ali Dossa Kidonyo mwenyewe keshafariki, hayupo kujibu. Mleta habari ndio anaweza kujua zaidi na kutupa mwanga.

Huyu "mkandarasi wa majengo" aliyepandisha majumba mengi Kariakoo na Dar-es-Salaam ya miaka ya 1930 na 40, alikuwa amejikita zaidi kwenye masomo gani ya ujenzi: je ni civil engineering, architectural, electrical, plumbing, ama real estate surveying na valuation? Si dhambi katika mada ya vipawa na umajiri wake tukajifunza na mafunzo yake.

Ama hakujikita kabisa katika ilm dunia?
 
sijapinga hoja yako ila elimu sio mafanikio bali zana ya mafanikio KWA MAANA UNAIPATA ili kufanikiwa kimaisha wewe shawishika na namna alivyopata hela sio kasoma nini. itafika mahali utauliza hadi GPA.
 
kimaisha wewe shawishika na namna alivyopata hela sio kasoma nini. itafika mahali utauliza hadi GPA.

yes, ndio hivyo hivyo nafanya, nashawishika na namna alivyopata hela.

ujuzi wake ulikuwa nini?

utakuwa jahili la ajabu kama utasikia habari za aliyejenga majumba ya mji huu halafu usitake kujua background yake kiufundi!

usimsifie kwa kugawa halua, kahawa, kashata, tende na sharubati kwa watu wanaoshinda barazani mwake na nyumba za kuabudu, hizo ni tamaduni za kiswahili na kivivu, sitaki kujua hayo peke yake... lazima tukuhoji

Mkandarasi wa majengo, Ustaadhi Ally Dossa Azizi Kidonyo alisoma nini, wapi na lini.

Au hakujikita kwenye ilm dunia ya ujenzi?

Sasa alijengaje majengo ya Kariakoo na Dar-es-Salaam ya 1930 and 1940s?
 
Naona swali lilikosa jibu hili.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
JINA LA MTONI KWA AZIZ ALI LIMETOKEA WAPI!?

Wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam, kuna eneo linaitwa Mtoni. Mtoni yenyewe nayo ina mitaa mingi ikiwamo Mtoni Kijichi, Mtoni Mtongani, Mtoni kwa Chaurembo, Mtoni kwa Mwenye Kuuchimba na Mtoni kwa Aziz Ali.

Kwa wakazi wa Dar es Salaam haswa wenye kuishi maeneo ya Mtoni, barabara ya Kilwa mpaka Mbagala jina ili la Mtoni kwa Aziz Ali, si jina geni.

Hapo Mtoni kwa Aziz Ali, siku nyingi nyuma alipata kuishi bwana mmoja aliyekuwa mmoja wa Waafrika matajiri sana kupata kutokea wakati huo wa ukoloni nchini Tanganyika. Aliitwa Ali Dossa Kidonyo na kwa hiyo kutokana na umaarufu wake, mahala hapo pakaitwa Mtoni Kwa Aziz Ali.

Aziz Ali, alikuwa Mdigo aliyetokea sehemu za Tanga na kuja kuweka kambi mjini Mzizima (sasa Dar es salaam), mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918) akiwa askari katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.

Mwajiri wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizoanzia kufanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi na kuajiri mafundi kadhaa.

Aziz Ali alijitengenezea umaarufu kutokana na kwamba aliweza kumiliki majumba mengi na magari ya biashara (yaani malori ya mchanga) pamoja na ya kutembelea, na vitu vingine kadhaa, kutokana na kazi yake ya kuwa mtaalamu wa kujenga nyumba (building contractor).

Hili jina la Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.

Huyu Aziz Ali alikuwa mwamba katika miamba ya Dar es Salaam. Alikuwa tajiri ,contractor,' wa kujenga, majumba, Mwafrika wa kwanza kununua magari na kujenga nyumba ya vigae na vioo Mtoni.

Yeye alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa muda hadi atakapoweza.

Nyumbani kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi na kufuturisha hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.

Nyumba hii hadi leo ipo na sehemu hiyo kandokando ya barabara ya Kilwa na ndipo hapo pakaja kuitwa Mtoni kwa Aziz Ali.

Lakini katika sifa hizi sifa yake kubwa sana Aziz Ali ilikuwa ujenzi wa misikiti na kuihudumia misikiti. Hii ilikuwa miaka ya 1930 na hapakuwa na umeme Kariakoo.

Misikiti ilikuwa ikitumia karabai kuonea. Aziz Ali yeye alinunua karabai kwa kila msikiti na ikifika Maghrib mwanae Hamza alikuwa akizitia mafuta na kuziwasha kisha akizipeleka kila msikiti tayari kwa sala ya Maghrib.

Inapomalizika sala ya Isha alikuwa anapita tena katika ile misikiti kukusanya karabai zake na kurudi nazo nyumbani kwao Mtaa wa Mbaruku na Kongo.

Mzee Aziz Ali alikuwa na nyumba nyingi sana Dar es Salaam na ndiyo zilikuwa moja ya utajiri wake. Katika nyumba hizi nyumba ambayo imaecha historia ya pekee ni hii nyumba ya Mtaa wa Mbaruku na Congo.

Nyumba hii ilikuwa moja ya sehemu ambazo harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika zilianzia hapo. Nyumba nyingine ilikuwa Mtaa wa Kipata kwa Ally Sykes, hapo zamani lilipokuwa duka la baba yake na barza ya wazee.

Nyumba nyingine ilikuwa Stanley Street kwa Abdul Sykes. Nyumba hii ilikuwa pia ya Kleist na kulikuwa na duka la vifaa vya ujenzi katika uhai wake.

Mzee Azizi Ali alitoa mchango mkubwa sana katika harakati za uhuru wa nchi hii kwa kujitolea mali zake na nguvu zake mfanyabiashara na aliyemiliki kampuni ya ujenzi wa nyumba, yetu yeye ndie alikua mjenzi miaka hiyo na nyumba nyingi tu mjini mitaa ya Kariakoo yeye alikua amezijenga tena kwa kumlipa kidogo na baadae kummalizia malipo yake kwa makubaliano maalum na wala hajawahi kumshtaki mtu kumcheleweshea malipo yake.

Ndipo kutokana na ukarimu wake mkubwa wakamwita "Aziz" yaani "Kipenzi." Ikawa wakimtaja jina wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali." Kiasi ikapelekea jina lake la Kidonyo likafa kabisa. Kwa hakika Aziz Ali alikuwa mcha Mungu sana.

Mzee Aziz Ali alipokufa mwaka wa 1951 miaka miwili baada ya kifo cha rafiki yake Kleist gazeti la Tanganyika Standard liliandika kifo chake kwa maneno haya: 'Aziz Ali the Builder of Mosques is Dead,' yaani, Aziz Ali Mjenzi wa Misikiti Amekufa.'

Alipofariki Mzee Aziz Ali, biashara zake ziliendelezwa na Mmoja wa watoto zake, Dossa Aziz Ali, na hata zile harakati za uhuru alijihusisha nazo tena kwa undani zaidi.

Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka wa 1950. Mambo yalipamba moto sana kuanzia mwaka huo pale vijana wazalendo walipoanza kufanya mipango ya kuunda chama cha siasa halisi kupambana na ukoloni wa Muingereza.

Nyumba zlizokuwa anamiliki Mzee Aziz Ali ndizo zikawa nyumba ambazo Nyerere alikuwa akifikia kuanzia mwaka wa 1952 kila anapokuja mjini kutokea Pugu alipokuwa akifundisha.

Dossa Aziz Ali (Mtoo wa Aziz Ali), alikuwamo katika kuasisi vyombo vyote vya mwanzo vinavyonasibishwa na harakati za kumng’oa Mkoloni, kama vile TAA na TANU akiwa Afisa na Mjumbe mwanadamizi aliye na sauti - hili sawa; hili fanya; hili wacha na mambo yakawa hivyo asemavyo.

Dossa, kwa kushirikiana na mwanachama mwengine Alexander Tobias, walichaguliwa na wenzao wakati fulani wawe makatibu wa pamoja wa muhtasari.

Harakati ziliposuasua alikuwa hachoki kuwapitia wenzake na kuwakumbusha majukumu waliyopeana akienda kwa mmoja mmoja nyumbani kwake kwa kutumia gari lake na kutaka kujua kulikoni mambo hayendi ipasavyo.

Katika siku za mwanzo za harakati, chama cha TAA na baadaye TANU havikuwa na uwezo wa kifedha wa kujiendeshea mambo yake hata kidogo.

Tegemeo lao kubwa lilikuwa ni kwa watu kama akina Dossa Azizi, aliyekuwa mkurugenzi na msimamizi mkuu wa biashara na mali za babake.

Wengine ni Mzee John Rupia na wale akina Sykes watatu (Abdul, Ally na Abbas), ambao baba zao walikuwa na uwezo wa fedha, ‘wawapige jeki’ (wachangie pakubwa).

Habari zinasema, ilikuwa ni Dossa Aziz aliyemwomba Nyerere kuacha tena kuvaa kaptura mbele ya wazee, kwani sasa ameshakuwa kiongozi ambaye atakuwa akikutana na watu wazima na hivyo si vizuri kuonekana na kaptura na stockings (zile soksi ndefu mpaka magotini).

Mzee Dossa alifanikiwa katika hilo kwani alimnunulia pia Nyerere suti kadhaa maridadi katika safari yake ya kule UNO -Umoja wa Mataifa (wakati ule), ili kupeleka kilio cha Watanganyika kudai nchi yao.j
Historia nzuri japo ina matobo. Huyu bwana alitokea kwao Tanga akiwa mkiristo na jina lake akiitwa Naftali Kidonyo. Kaingia uislam baada ya kuozeshwa binti wa kiswahili na wazee wa Dar es salaam.
 
Mkandarasi Ustaadhi Azizi Ali Dossa Kidonyo mwenyewe keshafariki, hayupo kujibu. Mleta habari ndio anaweza kujua zaidi na kutupa mwanga.

Huyu "mkandarasi wa majengo" aliyepandisha majumba mengi Kariakoo na Dar-es-Salaam ya miaka ya 1930 na 40, alikuwa amejikita zaidi kwenye masomo gani ya ujenzi: je ni civil engineering, architectural, electrical, plumbing, ama real estate surveying na valuation? Si dhambi katika mada ya vipawa na umajiri wake tukajifunza na mafunzo yake.

Ama hakujikita kabisa katika ilm dunia?
Majumba yenyewe yalikuwa ya kujengwa kwa miti na kuezekwa kwa madebe yaliyokatwa, si majumba kama unavyofahamu majumba leo hivyo hayakuhitaji taaluma kuyajenga. Nyumba ya maana aliyojenga ni hiyo ya Mtoni.

Hayo majumba yake ya madebe yalionekana ya maana Kariakoo kwa kuwa nyumba nyingi hapo zilikuwa za makuti.
 
Kwa kipindi hicho na mazingura yetu zilikuwa nzuri ....sioni sababu ya kuzi beza ...na pengine we mwenzangu na mimi hujui hata kujenga banda la kuku
 
Sijabeza, nilikuwa namjibu Kwameh anayehoji taaluma ya mzee Ali, ndiyo nikaandika kuwa ujenzi wa nyumba zile haukuhitaji taaluma.

Mimi ni miongoni mwa watu wanaoheshimu sana mafanikio ya mzee Ali. Kutoka kwao huko vijijini hata kuongea kiswahili ikiwa tabu, kukubali kubadili dini ili tu ampate binti wa kiswahili aliyempenda na baadaye kufanikiwa na kugeuka mfadhili wa hao waliompokea is no small feat.
 
Kwanza asante sana mleta maada kwa kutuelimisha kuhusu Marehemu Aziz Ali Dossa. Huwa napenda sana kusoma kuhusu watu wa jamii yetu la karibu.

Kuna watu wanakerwa sana wakisikia Muislam ambaye sio msomi, lakini kafanya maajabu kwenye maisha yake. Wanauliza marehemu Aziz Ali alikuwa na taaluma gani kwenye ujenzi? Ukiwa mjenzi wa majengo si lazima uwe na elimu ya ujenzi kama architecture, structrural, plumbing, nk. Watu wenye ujuzi huu wanapatikana na unaweza kuwaajiri au kuwa-consult. Hata leo hii kuna builders ambao hawajui ABC ya ujenzi, lakini wanajenga majengo marefu!

Hakika zile karabai zilizowashwa na Marehemu Aziz Ali Dossa Kidonyo na mwanae Hamza, kwenye misikiti ya Kariakoo, zinaleta nuru hadi leo kwenye mioyo ya waumini. Bila shaka wako peponi, na Mungu awaongezee rehema na fadhila pale mbinguni. Amen
 
Binafsi sijaona muuliza swali akionesha kukereka na uislamu, wala hajajitangaza kuwa dini gani.
Lakini pia u-hasi au u-chanya wa swali lake unategemea tafsiri ya alielisoma. Mimi nimelitafsiri kama muuliza swali alitaka kufikisha ujumbe kwa jamii na watunga sera wetu kuwa ubora wa kazi ya mtu hauna uhusiano na elimu ya darasani, maana muandishi wa mada kaeleza wazi kuwa Bwana Dossa alikua msaidizi tu, na aliachiwa mali na Boss wake ndipo akaziendeleza na kuanza hiyo kazi ya ukandarasi (haikutajwa elimu, na kwa mtu wa miaka ile mwenye elimu hata darasa la pili angekua ofisini).

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
daima historia haipotei kuna haja kubwa sana kurejesha historia ya kweli ya nchi hii maana kuna mambo mengi sana na wanaharakati wengi sana wapigania uhuru huwa hata kutajwa hawatajwi sasa hawa watoto wetu wataupata wapi uzalendo ikiwa hauwajazi uzalendo waliouonyehsa babu zao katika kudai uhuru ambao leo hii wao wanautumia kutembea kwa kujistiri kama hawajajistiri,, hivi wale watu 23 vinara wa kupigania uhuru ndani ya TANU na TAA ambapo hata Nyerere aliwakuta tayari wapo katika harakati hizo kama kina YAHYA TAKADIRI,DOSSA AZIZ,ABBAS SYKES,ABDULWAHEED SYKES,JOHN RUPIA n.k wanawajua kweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom