Je, kwa kisa hiki kijana alipaswa kumwambia mchumba wake kabla ya kumuoa kuwa ana mahusiano mengine?

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
489
1,271
Hiki ni kisa cha kweli kimetokea mtaa jirani, je mwanaume alikuwa sahihi kutoa talaka?

Iko hivi baada ya kijana kuhangaika kutafuta maisha kijijini aliamua kuzama mjini kusayasaka maisha hata hivyo haikuwa rahisi ikabidi azame kwa Jimama mwenye pesa.

Aliishi na huyu Jimama zaidi ya miaka 10 hata hivyo alifikiria kuoa na huyu mama alimkubalia ila kwa sharti la kutoachana baada ya kuoa.

Jimama aliamua kumfanyia kijana surprise kwa kumjengea nyumba na kumfungulia duka la magodoro ili akishaoa aishi mle ndani na mke wake ila mahusiano yaendelee

Baada ya kijana kuoa binti mahusiano yaliendelea na jimama huku akimwambia kule kwa Jimama ndiyo huwa anafanyia kazi kwa hiyo kuna siku atakuwa analala pale

Baada ya miaka kadhaa mke wa jamaa aligundua kuwa mume wake alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na jimama,hata hivyo mume alimwambia mke kuwa hataweza kuachana na jimama kwa sababu maisha mazuri waliyonayo ni kwa sababu ya jimama.

Huku mwanamke akiwa sasa ana watoto wawili hasira zilimpanda na kuamua kutembea na kinyozi karibu na mtaani Kama kwake kulipa kisasi na mbaya zaidi alimshawishi kinyozi amuoe na waondoke huo mji waende mbali.

Kinyozi alikubali na kuondoka na mke wa jamaa, hata hivyo walipofika walikokuwa maisha yao hayakwenda vizuri na kinyozi akaamua kumtelekeza huko.

Mwanamke aliona amepata mateso ya mtaani vya kutosha akaamua kumtafuta mume wake kumuomba msamaha hata hivyo kesi ilipelekwa mahakamani na kutolewa talaka.
 
Mwanaume anaweza kuoa hadi wanawake 6 kama ana uwezo wa kuwahudumia.

Jamaa yupo sawa 100% kutoa talaka.

Wanawake hufikiria suala la mahusiano ni rahisi hata kutafuta hela pia ni rahisi.
 
Kinyozi alikubali na kuondoka na mke wa jamaa,hata hivyo walipofika walikokuwa maisha yao hayakwenda vizuri na kinyozi akaamua kumtelekeza huko
.. Umesema kinyosi/zi yuko wapi 🤒


.. Ni kinyosi/zi wa nini kwanza 🤔
 
Hiki ni kisa cha kweli kimetokea mtaa jirani ,je mwanaume alikuwa sahihi kutoa talaka?

Iko hivi baada ya kijana kuhangaika kutafuta maisha kijijini aliamua kuzama mjini kusayasaka maisha hata hivyo haikuwa rahisi ikabidi azame kwa Jimama mwenye pesa
Aliishi na huyu Jimama zaidi ya miaka 10 hata hivyo alifikiria kuoa na huyu mama alimkubalia ila kwa sharti la kutoachana baada ya kuoa

Jimama aliamua kumfanyia kijana surprise kwa kumjengea nyumba na kumfungulia duka la magodoro ili akishaoa aishi mle ndani na mke wake ila mahusiano yaendelee

Baada ya kijana kuoa binti mahusiano yaliendelea na jimama huku akimwambia kule kwa Jimama ndo huwa anafanyia kazi kwa hiyo kuna siku atakuwa analala pale

Baada ya miaka kadhaa mke wa jamaa aligundua kuwa mume wake alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na jimama,hata hivyo mume alimwambia mke kuwa hataweza kuachana na jimama kwa sababu maisha mazuri waliyonayo ni kwa sababu ya jimama

Huku mwanamke akiwa sasa ana watoto wawili hasira zilimpanda na kuamua kutembea na kinyozi karibu na mtaani Kama kwake kulipa kisasi na mbaya zaidi alimshawishi kinyozi amuoe na waondoke huo mji waende mbali

Kinyozi alikubali na kuondoka na mke wa jamaa,hata hivyo walipofika walikokuwa maisha yao hayakwenda vizuri na kinyozi akaamua kumtelekeza huko

Mwanamke aliona amepata mateso ya mtaani vya kutosha akaamua kumtafuta mume wake kumuomba msamaha hata hivyo kesi ilipelekwa mahakamani na kutolewa talaka
Haieleweki
 
Back
Top Bottom