Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,461
- 11,443
Yapo mambo mengi ambayo yametoa picha ya namna Israel na Marekani wanavyoshirikiana kimkakati ili kuhakikisha Israel inaitawala Gaza na Palestina yote bila upinzani.
Ni kweli Israel ilikuwa na nia ya kuipiga Iran kwa nguvu kubwa na kuleta madhara zaidi lakini kwa kushauriana na Marekani na kujua kwamba Iran inajiamini kujibu na silaha zake zinafika Israel,hapo wawili hao wakaona ni afadhali waipe ushindi Iran ili Israel ibaki salama kuendeleza vita na Hamas.
Kujizuia kupigana na Iran mkono kwa mkono pia ilikuwa ni mbinu ya kurahisisha kupitishwa kwa msaada mkubwa wa kifedha wa dola bilioni 95 ambao kwa muda mrefu ulikuwa ukipingwa wa wabunge wa mabaraza yote na ulitarajiwa usingepita kabisa.
Hayo yanaonekana tangu pale walipoacha kuipiga Iran wamekuwa wakiongeza nguvu kuipiga Gaza hasa maeneo ya Rafah.
Wamezidisha mashambulizi maeneo ya kati ya Khan Younis na kaskazini katika maeneo ya Zeitoun ambako hawajaweza kuingiza vikosi vya miguu.
Mbinu hizo wanaziita ni vita vya kiakili na kisaikolojia dhidi ya Hamas japo uwezekano upo wa kutokuwapa ushindi wanaoutarajia