NADHARIA India ilijitoa Kombe la dunia sababu ya kukataliwa kucheza peku

Taarifa hii ni nadharia tu, tumeitolea ufafanuzi kwa kadiri ilivyowezekana
Source #1
View Source #1
Habari,

Taarifa zinaeleza kuwa mnamo mwaka 1950 timu ya Taifa ya India iliamua kujiondoa kushiiriki Kombe la Dunia sababu ya Shirikisho la Soka Ulimwenguni kuwakatalia kucheza peku.

Kuna ukweli wowote hapa?

1715893197490.png
 
Tunachokijua
Kumekuwapo na hoja inayodai kuwa nchi ya India ilijitoa kwenye kombe la dunia la mwaka 1950 sababu ya kukataliwa kushiriki mashindano hayo peku. JamiiCheck imepitia vyanzo mbalimbali na kubaini kuwa hoja hii imewekwa kwenye kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii, Tazama hapa, hapa na hapa

Pia JamiiCheck imepitia kwa kina historia ya India na michuano ya soka kuanzia mwaka 1948 kuelekea 1950 ambao ndiyo Kombe la Dunia lilichezwa nchini Brazil. Vyanzo vya Kihistoria vinasimulia kuwa Mnamo mwaka 1950 Vita vya Pili vya Dunia vilikuwa bado vipo katika kumbukumbu za mataifa mengi hasa mataifa ya Ulaya. Nchi nyingi za Ulaya zilikuwa zimeharibiwa kutokana na mapigano huku nchi za Bara la Asia zikiwa zimezama katika migogoro mipya huko Indochina. Baada ya mapumziko ya kulazimishwa ya miaka 12, Amerika Kusini ambayo haikuathirika sana na Vita -- ilichaguliwa kuandaa kombe la Dunia la mwaka huo wa 1950, na Brazil ikakaribisha mashindano ya kwanza ya bara hilo tangu lile la kwanza mwaka 1930 huko Uruguay.

Mwaka 1948 nchi ya India iliingia kwenye historia ya Soka la Dunia baada ya kufanya vizuri kwenye Mchezo wake wa Olimpiki ilipofanikiwa kuonesha upinzani mkubwa kwenye mechi yake dhidi ya Ufaransa. Japo taifa hilo lilipoteza mchezo kwa mabao 2-1 lakini mchezo mzima wachezaji wa India walicheza peku na wengine wakiwa na soksi tu.

1715892662121-png.2991991

Kikosi cha India kilichoshiriki Olimpiki 1948

Mechi hii ilivutia sana kwa kuwa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya 1948 ilikuwa mara ya kwanza kwa India kushiriki katika mashindano ya kimataifa kama taifa huru (baada ya kupata uhuru kutoka Uingereza). Hata hivyo, ukweli kwamba timu ya India ilifanya yote haya bila viatu ulivutia zaidi.

Upi ukweli kuhusu India kujitoa kisa kukataliwa kucheza peku?
India ilijikuta ikiingia katika kombe la Dunia baada ya timu za Philippines, Indonesia na Burma kujitoa na hivyo kuipa nafasi India ya kwenda moja kwa moja nchini Brazili kwaajili ya michuano hiyo. Hata hivyo inaelezwa kuwa mwaka 1950 shirikisho la soka duniani (FIFA) liliipiga marufuku India kucheza peku watakaposhiriki Kombe la dunia ambapo mwaka huo huo India ilijitoa kwenye kombe la dunia.

Timu shiriki hupewa fedha kwaajili ya maandalizi, hivyo sababu ambayo wengi waliamini pia mbadala na hii ya kucheza peku peku ilikuwa ni timu kushindwa kujigharamia safari zake, ambayo haikuwa kweli.

Kwa mujibu wa shirikisho la mpira wa miguu nchini humo, sababu kubwa waliyotoa ilikuwa ni ‘kutokubaliana na katika uchaguzi wa timu na maandalizi kuelekea michuano hiyo’. Hivyo basi, India wanaamini hizo sababu za ‘peku peku’ na kukosa nauli hazikuwa sababu ya timu yao kushindwa kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Brazili. Hadi sasa ni takribani miaka 68, India haijanusa Kombe la Dunia.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom