Mwanzo nilikuwa binti mwenye nuru sana, pamoja na kufiwa na wazazi wote wawili wakati nikiwa na miaka 8 lakini sikuwahi kuwa na maisha ya ukiwa hata kidgo, ndugu zangu upande wa mama walilichukua jukumu la kunilea kwa zamu tena kwa mapenzi makubwa sana. Nikafanikiwa kupata elimu ya msingi na sekondari na wakati naingia chuo mwaka wa kwanza kwa sababu za kiafya nikamua kucheki afya yangu ndipo nilipogungua nipo + hapo kila kitu nikawa cheusi
Kwangu sikuiona tena future, na sikuwa na ujasiri wa kusema nyumbani coz tulishazika ndugu kama 4 hivi tayari na majonzi yalikuwa bado hajawaisha ndugu zangu. Baada ya kujua hali yangu kila kitu kilibadilika sikuwa na hamu tena na dunia nilikuwa na mawazo ya kufa kila wakati.
Elimu sikuiona tena ya maana., nilivurugwa kabisa nikaona niachane kabisa na chuo coz kwa muda huo sikuona kabisa umuhimu wake. Nikapata sonona moja kali nikawa najifungia tu ndani na kuangukia kabisa kwenye dunia ya waliokata tamaa.
Wakati nikijaribu kutoka na kushindwa siku moja nikapata simu nyumbani kuna ndugu yangu alikuwa kalazwa, sikutaka kwenda kabisa lkn kuna kitu kikaniambia niende tu nikamwone. Baada ya kufika pale na kumwona macho yalinifunguka na kuamua kutoka usingizini hali ya ndugu yangu iliweka simanzi kubwa kwenye nyuso za ndugu zangu, Mungu amlaze salama, hapo nikaamua kutoka gizani.
Baada ya kukaa ukiwa kwa miaka 4 nikaamua kwenda kituo cha afya na kuanzia dawa pamoja na ushauri sasa ni mwaka wa 6 tangu nitoke ndotoni maisha si sawa tena.
Sina future ya maana na ninatamani japo ningemaliza elimu yangu maisha yamekuwa magumu zaidi ya yenye ukiwa zaidi japo kidogo sina tena mawazo ya kijinga na afya yangu imeimarika sana. Mambo yamebadilika sasa, + si tishio tena watu wana + na maisha yanaenda kama kawaida
Mimi natamani miaka ile ingekuwa ni sasa nadhani ningekuwa na bright future.
Asanteni sana