Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,459
- 11,443
Hapo jana Misri imetoa tamko kuwa kuanzia sasa haitotoa ushirikiano tena na Israel katika kupitisha misaada mpaka wa Rafah.
Nongwa hiyo ya Misri ni kwa vile ati Israel imejichukulia jukumu la kukikalia kituo hicho cha mpaka kibabe ambacho ndicho kikuu katika kuingiza misaada Gaza.
Maelezo hayo ya Misri hayana maana wala faida yoyote kwa wapalestina wa Gaza baada ya kuumizwa kwa takriban miezi 7 sasa. Zaidi ni kuwa nongwa hiyo itakuwa ni kama wameipa zawadi Israel kuendelea kuwaua watu wa Gaza bila vikwazo vyovyote.
Tangu awali Gaza inachukuliwa kama ni mali ya wapalestina na wala si mali ya Israel. Sijui kwanini tangu hapo awali Misri ilikubali kutoa ushirikiano na Israel kwa kukubali bidhaa zinazoingia Gaza ziwe zinapekuliwa na Israel ndani ya Misri takriban kilomita mia kabla ya kufika Rafah.
Baada ya kuona Israel ina harakati za kuivamia Rafah basi Misri ingeamua kukidhibiti kituo cha Rafah pande zake zote na kusingekuwa na lawama na wala Israel isingeweza kuwaondoa.