Black poison The Factor
JF-Expert Member
- May 31, 2020
- 1,034
- 1,498
Juzi mama wa mwanangu alikuwa anaenda dukani, mtoto nayeye akataka kwenda mama yake akamzuia dogo akawa mbishi.
Ikabidi wakubaliane kwamba hakuna kubwebwa, mtoto akakubali safari ikaanza, kama dakika 6 tu dogo akataka abebwe.
Mama akawa mkali, mtoto akatumia akili nyingi akaita mama mamaake akaitika abee mtoto akasema mbebe mtoto wako amechoka.
Akalamika kidogo pale kama kawaida dogo akapata lift.
Ni mengi sana mnayopitia akina mama wakati wa kutulea . Kiukweli hongereni sana sana sana.
Bila kusahau upendo wenu kwa watoto wenu haijalishi wanafanya mangapi ila upendo haupungui.
Mama ni nguzo muhimu sana kwa kila kiumbe, bila mama hakijakamilika kitu.
Hongereni akinamama wote MUNGU awabariki.
Ingependeza sana kama mngewapenda wanaume wenu kama muwapendavyo watoto,
Dunia ingekuwa sehemu salama sana kwetu sote kuishi muwe na jioni njema.