Hivi Mshauri wa Saikolojia na Ndoa za watu nchini Tanzania Dkt. Mauki ndiyo kusema yeye ni Malaika na hakumbani na kero zitupatazo?

Labda kama mmekutana wawili wanafiki na wazindiki, ila wanaopendana kwa dhati lazima wakumbane na changamoto tu, ukikutana na mnafiki wa kukujibu "sawa baby" kwa kila kitu hutaona changamoto zozote.

Changamoto sio chuki
Changamoto za kiuchumi na maisha sio tatizo kwenye mapenzi.

Ila zile za kitabia kama usaliti wa zinaa, mapombe, dharau sijui ubinafsi hizô kwa baadhi ya mahusiano hakuna kitu kama hicho.

Wanafiki na wasaliti wanafanana kitabia ya kutokuaminiana na kudhani Watu wote ni wanafiki au sio waaminifu kama wao walivyo.
 
Kwahiyo Yeye Mkewe hachepuki, Yeye hachepuki na kwamba Yeye ni Mtakatifu sana katika Mahusiano na Saikolojia? Tafadhali mwenye Picha ya Mke wa Dk. Chris Mauki tafadhali aiweke hapa ili labda wenye Changamoto zetu za Kimahusiano tuitumie Kuwaonyesha Wapenzi / Wake zetu ili Wakiiona tu nao Wabadilike upesi Kitabia na Kero ziishe Majumbani mwetu na Mapenzi yawe mwemwere mwemwere tu.
Ili asipendelee upande wowote aliamua asiwe na mke.
 
Watu kama wakina Mauki ndio wana matatizo kuliko sisi, Mmesahau ishu ya JJ Mwaka anawahubiria watu na kuwauzia dawa za kuongeza nguvu za kiume wakati yeye mwenyewe ana hilo tatizo. Na akakimbiwa na Mke? Hawana ishu watu kama Hawa ni blah blah tu na kujitafutia pesa kupitia wanyonge.
JJ Mwaka kumpe jogoo hapandi mtungi??
 
Kwahiyo Yeye Mkewe hachepuki, Yeye hachepuki na kwamba Yeye ni Mtakatifu sana katika Mahusiano na Saikolojia? Tafadhali mwenye Picha ya Mke wa Dk. Chris Mauki tafadhali aiweke hapa ili labda wenye Changamoto zetu za Kimahusiano tuitumie Kuwaonyesha Wapenzi / Wake zetu ili Wakiiona tu nao Wabadilike upesi Kitabia na Kero ziishe Majumbani mwetu na Mapenzi yawe mwemwere mwemwere tu.
hao motivation speakers wote ni waongo tu, hasa ukija kwenye suala la utekelezaji wa hio miradi wenyewe wameshindwa ndio maana wamechagua hio kazi ya ushauri na kuuza vitabu ili mkono uende kinywani! ukiwaskiliza
 
Changamoto sio chuki
Changamoto za kiuchumi na maisha sio tatizo kwenye mapenzi.

Ila zile za kitabia kama usaliti wa zinaa, mapombe, dharau sijui ubinafsi hizô kwa baadhi ya mahusiano hakuna kitu kama hicho.

Wanafiki na wasaliti wanafanana kitabia ya kutokuaminiana na kudhani Watu wote ni wanafiki au sio waaminifu kama wao walivyo.
Sasa hizo changamoto za dharau, pombe, uzinzi, uongo, kuumizwa kihisia nk ndio sehemu halisi ya mapenzi. Huwezi kuishi na mwenzi wako kwa miaka 10+ bila kukutana na mojawapo kati ya hayo. Kumbuka tu graph ya upendo huwa haipandi wakati wote, no matter how you love her. Zile ups na downs zinaweza hata kukufanya ukawaza(question) upendo wako kwake.

Ukiona ndoa inaenda smooth for decades kuna mmoja anaminywa na hana namna, ila wote mkiwa huru, utashangaa na kujiuliza mengi.

Waliosema marriage is not a bed of roses hawakuwa wajinga.
 
Kwahiyo Yeye Mkewe hachepuki, Yeye hachepuki na kwamba Yeye ni Mtakatifu sana katika Mahusiano na Saikolojia? Tafadhali mwenye Picha ya Mke wa Dk. Chris Mauki tafadhali aiweke hapa ili labda wenye Changamoto zetu za Kimahusiano tuitumie Kuwaonyesha Wapenzi / Wake zetu ili Wakiiona tu nao Wabadilike upesi Kitabia na Kero ziishe Majumbani mwetu na Mapenzi yawe mwemwere mwemwere tu.

MSANII TU HUYO NIMESOMA NAYE UDSM
 
Yule ile ni fani yake kasomea, huwezi kumjudge kwa ajili ya hiko. Unaambiwa fuata maneno na siyo matendo, ni kama wachungaji tu wanavyotuhubiria ila mwisho wa siku nao ni binadamu
 
Kwahiyo Yeye Mkewe hachepuki, Yeye hachepuki na kwamba Yeye ni Mtakatifu sana katika Mahusiano na Saikolojia? Tafadhali mwenye Picha ya Mke wa Dk. Chris Mauki tafadhali aiweke hapa ili labda wenye Changamoto zetu za Kimahusiano tuitumie Kuwaonyesha Wapenzi / Wake zetu ili Wakiiona tu nao Wabadilike upesi Kitabia na Kero ziishe Majumbani mwetu na Mapenzi yawe mwemwere mwemwere tu.
Mapenzi hayana formula!...unaweza kuta yeye ndo anapitia mazito kwenye ndoa yake
 
Kwahiyo Yeye Mkewe hachepuki, Yeye hachepuki na kwamba Yeye ni Mtakatifu sana katika Mahusiano na Saikolojia? Tafadhali mwenye Picha ya Mke wa Dk. Chris Mauki tafadhali aiweke hapa ili labda wenye Changamoto zetu za Kimahusiano tuitumie Kuwaonyesha Wapenzi / Wake zetu ili Wakiiona tu nao Wabadilike upesi Kitabia na Kero ziishe Majumbani mwetu na Mapenzi yawe mwemwere mwemwere tu.
Haaaa genta kama genta nimecheka sanaa
 
Back
Top Bottom