Enyi wanawake acheni ligi na wanaume mtaumia

Chief Kumbyambya

JF-Expert Member
Jun 16, 2022
550
1,744
Nipo zangu eneo langu la biashara... Ni kasoko flani hivi kalikochangamka kwahiyo nikaona niwe na kastationary pale kakuzugia, mambo yote ya photocopy, printing, scanning, binding na kuchapa chapa material nini unapata na huduma ya passport size zile za fasta dakika 3 pia zipo fresh tu.

Mwezi uliopita kulitokea kutokuelewana kati yangu na mwenye frem pale mzozo ukawa mkubwa kiasi cha kurushiana ngumi. Ebwana yule mwenye frem kipigo kikamzidi akakimbilia frem ya jirani ambayo ni saluni ya kike ya sistaduu mmoja anamdomo balaa na hatuivi hata kidogo... nikamfata jamaa huko huko... Kichapo kikaendelea.

Ile vuta nikuvute vuta nikuvute nikamlima jamaa bonge la buti jamaa chini.. yule dada na wateja wako ... Bwana tokenii mpiganie hukooo hatutaki magomvi... Sasa ile namvuta jamaa twende nje mchiz alinirukia kichwa kimoja hivi matata. Kumbe alikuwa ananivizia bana... Nikaenda kugonda dryer kubwa la yule dada nikadondoka nalo mpaka chini mzee likaasukaa. Na huyu dada hatuiviiiiii.. yani elewa maana ya hatuivii.

Aaaaa bibie akapata stata. Hilo draya nimenunua 220,000 nalihitaji kama lilivyo aisee ukawa mzozo mkubwa nikamuomba msamaa nilipe nusu ilikuwa bahat mbaya na wadau wakawa wanamsihi nilipe nusu yani 110,000 ooohooo bibie yuko wapii? Ashachukua boda kaenda polisi fasta.. mazee akasema pamoja na usumbufu niliomfanyia ofisini kwake nilipe 300,000 nikajiumauma palee mwisho nikatoa yakaisha. Ila moyoni nikawa nakinyongo kisicho na mfano...

Hiyo ni mwezi uliopita mwanzoni. Mungu si zakayo aisee naye jana si kayatimbaa.

Kuna kadem ni kafanyakazi kangu nakaachaga ofisini sasa huyu sista duu si hatuivi! Nisipokuwepo kumbe anaingiaga ofisini kwangu kupiga stori na yule mfanyakazi wangu, sasa kutokana na tatizo la umeme pale nina kajenereta kangu kadogo kwa ajili ya emergency ya umeme ikitokea umekatika kazi zisisimame.

Sasa nikawa nimeacha chaji sim yangu ofisini pale aina ya SAMSUNG GALAXY S23 ULTRA ya Tsh 2,500,000/= na risiti ninayo.

Kumbe wakati sipo kaingia kupiga stori akaanza kuishikashika sim yangu ananiangalia.. aisee Mungu akiwa upande wako yuko kwako tu. Si akaitwa na wenzie fasta ofisini kwake akasikilize mteja! Katoka mbio na sim yangu akajisahau kakaa nayo huko mtoto wako anatambaa kaishika kaitia kwenye ndoo ya maji kuoshea nywele ikakaa humo zaidi ya lisaa.

Narudi moyo unadunda sim yangu iko wapi? Ndo yule mfanyakazi wangu akaniambia alikuwa nayo ashura (yule sista duu) nikasema whaaaaaaaaaat??? Ashura kuulizwa akaanza kuitafuta ndo mteja wake mmoja akasema aliishika mwanao hapa.. ebwana baada ya kuitafuta weee tukaikuta kwenye ndoo ya maji... kuiwasha hauwakiiii... inavuja maji kama kuitambaa kimelowekwa vile.

Nikasema Asante Mungu nimempata kwenye anga zangu huyu, kwanza bibie kidogo azimie.

Nilichokifanya nikaenda hom nikaja na risiti ya simu inasoma Tsh 2,500,000/= akaanza kulia pale wenzake wanamuombea msamaha, nilitoa kauli moja tu...

"Hiyo simu nakuachia baki nayo naitaka ikiwa mpyaa nafikiri bei yake umeiona kwenye risiti hapo"

Bibie akajifanya kizimia hapo watu kibao wanamuombea msamaha nikawakumbusha tukio langu alilinifanyia watu kimyaaa.

Wakiwa wenzake wanampepea aamke mimi fastaa kituoni... Baada ya saa moja nikampgia jirani yangu mwngine wa frem pale kwamba waambie wamlete huyo atazindukia huku. Dem akaja kashikiliwa huku na huku na weupe ule uso umekuwa mwekunduuu kwa kulia.. nikajisemea moyoni na "badooo... hili ni tela tu"

Nikaunganisha kesi kama yeye nikamwambia polisi kaingia ofisini kwangu wakati sipo akabeba simu. Kwanini abebe kitu sio chake tena kwenye ofisi ya watu? Pamoja na usumbufu wa kuingia ofisini kwangu bila ruhusa siwezi kujua kachukua nini kingine, Kwa hiyo kwenye hiyo 2,500,000 ya simu aongeze 500,000 ya usumbufu jumla iwe 3,000,000/=

Dem akaanza kulia tena kwa kwikwi nyungiiii.. mimi waalaaaaa.... Tena naona kama ananicheka kwanza.

Hivi tunavyoongea saluni yake tumefunga na vitu vyote vikiwa ndani na polisi wakiwepo...

Aisee kumbe saluni za kike zina gharama aisee.. Kwa hesabu niliyopiga harakat harakat hii ofisi yeke inalipa simu na gharama zangu zotee na machenji juu.

Halafu nilichofurahisha zaidi kumbe hela za kufungulia ile saluni alikopa mkopo BLACK kwa wahindi.

Hata sijui namba yangu kaitoa wapi.. anapiga simu balaa kuomba msamaha namsikiliza weeeeee siongei kitu alafu nakata simuu

Nafikiri hapo nimecheza kama Pele wazee mpaka alipe.. hapa ligi ligi tu si wanataka haki sawa?
 
Nipo zangu eneo langu la biashara... Ni kasoko flani hivi kalikochangamka kwahiyo nikaona niwe na kastationary pale kakuzugia, mambo yote ya photocopy, printing, scanning, binding na kuchapa chapa material nini unapata na huduma ya passport size zile za fasta dakika 3 pia zipo fresh tu.

Mwezi uliopita kulitokea kutokuelewana kati yangu na mwenye frem pale mzozo ukawa mkubwa kiasi cha kurushiana ngumi. Ebwana nukamzdi yule jamaa akakimbilia frem ya jirani ambayo ni saluni ya kike ya sistaduu mmoja anamdomo balaa... nikamfata jamaa huko huko.

Ile vuta nikuvute vuta nikuvute nikamlima jamaa bonge la buti jamaa chini.. yule dada na wateja wako ... Bwana tokenii mpiganie hukooo hatutaki magomvi... Sasa ile namvuta jamaa twende nje mchiz alinirukia kichwa kimoja hivi matata. Kumbe alikuwa ananivizia bana... Nikaenda kugonda dryer kubwa la yule dada nikadondoka nalo mpaka chini mzee likaasukaa. Na huyu dada hatuiviiiiii.

Aaaaa bibie akapata stata. Hilo draya nimenunua 220,000 nalihitaji kama lilivyo aisee ukawa mzozo mkubwa nikamuomba msamaa nilipe nusu ilikuwa bahat mbaya na wadau wakawa wanamsihi nilipe nusu yani 110,000 ooohooo bibie yuko wapii? Ashachukua boda kaenda polisi fasta.. mazee akasema na usumbufubniliomfanyia ofisini kwake nilipe 300,000 nikatoa yakaisha. Ila moyoni nikawa nakinyongo kisicho na mfano...

Hiyo ni mwezi uliopita mwanzoni. Mungu si zakayo aisee naye jana si kayatimbaa.

Kuna kadem ni kafanyakazi kangu nakaachaga ofisini sasa huyu sista duu si hatuivi! Nisipokuwepo anaingia ofisini kwangu kupiga stori na yule mfanyakazi wangu, sasa kutokana na tatizo la umeme pale Nina kajenereta kadogo kwa ajili ya emergency ya umeme ikitokea umekata kazi zisisimame. Sasa nikawa nimeacha chaji sim yangu ofisini SAMSUNG GALAXY S23 ULTRA ya Tsh 2,500,000/= na risiti ninayo.

Kumbe wakati sipo kaingia kupiga stori akaanza kuishikashika sim yangu ananiangalia.. aisee Mungu akiwa upande wako yuko kwako tu. Si akaitwa na wenzie fasta ofisini kwake akasikilize mteja! Katoka mbio na sim yangu akajisahau kakaa nayo huko mtoto wako anatambaa kaishika kaitia kwenye ndoo ya kuoshea nywele ikakaa humo zaidi ya lisaa.

Narudi moyo unadunda sim yangu iko wapi? Ndo yule mfanyakazi wangu akaniambia alikuwa nayo ashura (yule sista duu) nikasema whaaaaaaaaaat??? Ashura kuulizwa akaanza kuitafuta ndo mteja wake mmoja akasema aliishika mwanao hapa.. ebwana baada ya kuitafuta tukaikuta kwende ndoo kuwasha hauwaki... Inavuja maji kama kuitambaa kimelowekwa. Nikasema Asante Mungu nimempata kwenye anga zangu kwanza bibie kidogo azimie.

Nilichokifanya nikaenda hom nikaja na risiti ya simu inasoma Tsh 2,500,000/= akaanza kulia pale wenzake wanamuombea msamaha, nilitia kauli moja tu... "Hiyo simu nakuachia baki nayo naitaka ikiwa mpyaa nafikiri bei yake umeiona kwenye risiti hapo"

Bibie akajifanya kizimua hapo watu kibao wanamuombea msamaha nikawakumbusha tukio langu alilinifanyia watu kimyaaa.

Wakiwa wenzake wanampepea aamke mimi fastaa kituoni... Baada ya saa moja nikampgia jirani yangu mwngine wa frem pale kwamba waambie wamlete huyo atazindukia huku. Dem akaja kashikiliwa huku na huku na weuoe ule uso umekuwa mwekunduuu kwa kulia.. nikajisemea moyoni na "badooo... hili ni tela tu"

Nikaunganisha kesi kama yeye nikamwambia polisi kaingia ofisini kwangu wakati sipo akabeba simu. Kwanini abebe kitu sio chake tena kwenye ofisi ya watu? Pamoja na usumbufu ya kuingia ofisini kwangu Bula rihisa siwezi kujua kachukua nini kingine, Kwa hiyo kwenye hiyo 2,500,000 ya simu aongeze 500,000 ya usumbufu jumla iwe 3,000,000/= Dem akaanza kulia tena kwa kwikwi mimi waalaaaaa.... naona kama ananicheka kwanza.

Hivi tunavyoongea saluni yake tumefunga na vitu vyote vikiwa ndani na polisi wakiwepo... Aisee kumbe saluni za kike zina gharama aisee.. Kwa hesabu niliyopiga hii ofisi inalioa gharama zangu zotee na machenji juu.

Halafu nilichofurahi kumbe hela za kufungulia ile ofisi alikopa black Kwa wahindi.

Hata sijui namba yangu kaitia wapi.. anapiga simu balaa kuomba msamaha namsikiliza weeeeee siongei kitu alafu nakata simuu

Nafikiri hapo nimecheza kama Pele wazee mpaka alipe.. hapa ligi ligi tu si wanataka haki sawa?
Uko sahihi mkuu utani na pesa nshaachaga nimefuza shemeji yangu nyumbani naitaji kukaa kwa amani
 
Kwa namna yoyote ile epuka ugomvi wa aina yoyote na jirani yako,, nyuma ya hizi biashara kuna mambo mengi mno ambayo najua yako juu ya uwezo wako... Hivo visasi sio vizuri katika maisha
Hakuna kuepuka acha huyo bibie anyooshwe..

Kaka shikilia hapo hapo shikilia kwa ajili ya sisi tunaoliwa nauli na kubambikiziwa kesi na hao mabinti
 
Back
Top Bottom