Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,454
- 11,427
Mwanzo ilikuwa kama tetesi na mshangao kuwa Iran imeiuzia au imeipa zawadi Urusi droni zake ili zishiriki kuitandika Ukraine.Na hata raisi wa Ukraine mwanzoni alizitaja droni kuwa haziwezi kazi na hazitobadilisha kasi yao ya kuteka miji ya Urusi.Mambo yamebadilika tangu wiki mbili zilizopita wakati droni hizo zilipoupiga mji wa bandari wa Odessa na kupelekea Zelensky kuitupia lawama Iran kwa kutoa droni zake za Shaheed kusaidia kuwapiga.Malalamiko hayo yameongezeka hapo juzi Urusi ilipoipiga miji mingi ya Ukraine kwa wakati mmoja.Kwa mara nyengine jeshi la Ukraine limetaja hofu yao kwa droni hizo zinazodowea angani na zinazopiga kama mwewe.