UZUSHI Clatous Chama awaaga Mashabiki wa Simba SC Mtandaoni Aprili 29, 2024

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Source #1
View Source #1
Nimeona Mwamba wa Lusaka amewaaga mashabiki wa Simba kuwa anaondoka. Nimesikitika sana, kwaheri Clatous Chama.

Chama123.jpg
 
Tunachokijua
Clatous Chota Chama au maarufu zaidi kama Mwamba wa Lusaka alizaiwa Juni 18, 1991 nchini Zambia. Kiungo huyu mshambuliaji kwa sasa anaitumikia klabu ya Simba ambapo kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, mkataba wake na klabu hii unatarajia kuisha mwishoni mwa msimu huu wa 2023/24 huku ikidaiwa upo uwezekano wa kuongeza muda zaidi katika kuitumikia klabu hiyo.

Madai ya kuaga Mtandaoni
Aprili 29, 2024 ziliibuka mtandaoni taarifa zinazodai kuwa mchezaji huyu alikuwa ameaga viongozi na Mashabiki wa Simba kuwa anakwenda kutafuta changamoto nyingine.

Mojawapo ya akaunti za Mtandao wa X iliyochapisha taarifa hii ni ile inayoitwa Clatous Chama, ambayo inatajwa kumilikiwa na mchezaji huyo.

Hadi kufikia Mei 2, 2024, chapisho hili lilikuwa limesomwa na watu takribani 188,900 na lilikuwa limepokea maoni 230.

Kwa kunukuu, andiko hilo lilisema;

"Asanteni sana viongozi na mashabiki wa Simba sports club nimekua nanyi kwa kipindi kirefu na siku zote nawapenda Sana. Ni mda sasa kwenda kutafuta changamoto sehemu nyingine. Daima takumbuka nafasi yangu ndani ya mioyo yenu"

Ukweli wake upoje?
JamiiChek imefuatilia chapisho hili na kubaini kuwa siyo chapisho halisi la Clatous Chama.

Akaunti rasmi ya Chama inatumia majina matatu ambayo ni Clatous Chota Chama (@ClatousCC) huku Akaunti iliyotumika kuchapisha andiko hilo ikitumia majina 2 ambayo ni Cloutus Chama (@ClaotusCC).

Aidha, kuna utofauti wa herufi kwenye majina, Jina sahihi la Chama huanza na Clatous badala ya Cloutus kama lilivyoandikwa kwenye akaunti hii ya kughushi.

JamiiCheck imekagua historia ya machapisho ya nyuma ya Akaunti hii na kubaini kuwa kwa mara kadhaa imekuwa inajihusisha kuchapisha matukio mengi yenye kuvuta hisia yanayoibuka kwenye jamii.

Mathalani, Juni 24, 2023 iliwahi kuchapisha andiko linaojinasibisha na Mwanafunzi mmoja wa kike aliyehusika kwenye kisa kimoja cha mapenzi ambapo stori yake inapatikana pia kwenye makavazi ya JamiiForums

1000034305-jpg.2978909


Kutokana na uwepo wa historia ya kubadilika kwa majina ya Akaunti tajwa, kukosewa kwa baadhi ya herufi kwenye Majina pamoja na kukosekana kwa chapisho la aina hii kwenye Akaunti rasmi za Clatous Chama, JamiiCheck inatambua taarifa hii kama Uzushi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom