Bei ya luku ishuke, viwanda vifufuliwe, wananchi wapikie majiko ya umeme kuzuia uharibifu wa mazingira

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,318
24,668
Salaam, Shalom.

Samahani Kwa waliozaliwa 2000+, Miaka ya 90 kurudi nyuma, yalikuwepo majiko( Meko) ya umeme katika nyumba nyingi za watumishi wa umma, mapolisi, mahakimu, bankers, watoza ushauri, matajiri nk nk.

Matumizi ya majiko ya kutumia umeme, yalisaidia kupunguza matumizi ya mkaa, hivyo kuzuia uharibifu mkubwa wa mazingira na kupunguza matumizi ya mkaa na Kuni.

Hivi sasa, kaya nyingi zinatumika majiko ya Kuni na mkaa Kwa wingi,gesi kidogo.

Kwa kuwa nchi yetu imekopa matrilioni kujenga BWAWA la JNHP, na Kwa kuwa walipaji wa deni Hilo ni sisi wananchi, na Kwa kuwa majiko ya umeme Yana faida zaidi kimazingira, na Kwa kuwa Bei kubwa za luku ni chanzo kikubwa Cha kutotumika majiko ya umeme nchini Kwa wananchi wa kipato Cha chini,

Na Kwa kuwa, mradi wa REA kuunganisha vijiji Kwa huduma ya umeme umewafikia wengi, uwezekano wa kutumia umeme kupikia ni mkubwa zaidi Hadi vijijini.

Ninashauri Bei za luku zishushwe Ili wananchi waongeze matumizi ya umeme Kwa kupikia ili kuboresha na kutunza mazingira.

Kushushwa Bei za luku Kuna faida ZIFUATAZO;

1. Matumizi ya umeme yataongezeka na mapato pia yataongezeka hivyo kulisaidia shirika kujiendesha Kwa faida..

2. Serikali itaongeza ukusanyaji wa mapato Kwa ajili ya kulipa mikopo iliyotumika kujenga BWAWA la JNHP.

3. Matumizi makubwa ya umeme wa kupikia majumbani, itaongeza matumizi ya mitambo ya kufua umeme, hivyo kuondoa hatari ya kuchakaa na kiharibika mitambo Kwa kuzimwa mara Kwa mara.

4. Kupunguza gharama za umeme Kwa wananchi kutachagiza viwanda vidogo vidogo , viwanda vya kati na vikubwa kuoperate Kwa faida kubwa hivyo kuinuka Kwa kipato na mxunguko wa pesa, Uchumi utakua na export zitaongezeka.

5. Kupunguza gharama za umeme kutusaidia kuondoa mafuriko Kwa wakazi vijiji vinavyopakana na BWAWA la JNHP Kwa kuwa mashine za kuzalisha umeme zitatumika ipasavyo hivyo kupunguza zoezi la kumfungulia maji ya BWAWA Hilo.

USHAURI:

Ikiwa Kwa sasa ukinunua umeme wa sh 5,000 unapata unit 14,

Tafsiri hapo ni kuwa, 1unit =sh 357.

Bei ishuke kuwa 1unit =sh 10.

Ili Ukiwa na sh 5000 upate Unit 500.

Hapo itawezekana kupikia majiko ya umeme Hadi huko bush Kwa bibi zetu.

HITIMISHO:

Kupungua Kwa gharama za umeme wa luku Kuna faida kubwa kiuchumi, Kijamii, kisiasa, kiafya, ninashauri Serikali yangu kuacha mawazo ya kuuza umeme nje ya Nchi, umeme upunguzwe Bei kufufua viwanda vidogo vidogo vya kati na vikubwa tupate faida za kiuchumi.

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿

Amen

Karibuni🙏
 
Chini ya utawala wa CCM usitegemee bei ya umeme kushuka Hilo sahau kabisaa!!!
Wakijitahidi Sana wataondoa Yale Makato ya Tsh 1500/= Kwa kila Mita ya luku, hawa watu ni zaidi ya mashetani
CCM itakufa very soon ikiendelea kupuuza mawazo haya Kwa kuwa itafika time mikopo itashindwa kulipika, viongozi watazikimbia ofisi.

Mada hizi zitafufuliwa na kufanyiwa KAZI, kama Si Leo, kesho, ndio maana hatuchoki kuandika na kutoa ushauri Chanya,

Ubarikiwe.
 
Daah hawawezi kushusha na pia wanaongeza bei ya gesi kila kukicha usitegemee neema kwenye hilo mimi mara ya mwisho kutumia jiko la umeme ilikua home kwa wazazi miaka ya 90 huko sasa hivi majiko ya umeme nayaangalia kama ni kipuli cha Tractor CAT...
Uzalishaji wa umeme kupitia JNHP ni cheap,

Inatakiwa tunufaike na umeme wetu sababu tutalipa mikopo hiyo sisi Hawa Hawa.

Sasa ikiwa miaka ya 90 tulipikia majiko ya umeme tukiwa na mtera pekee, tushindweje ikiwa JNHP IPO?

Maendeleo ni kusonga mbele, Si kurudi nyuma!!

Tutafika tu!!
 
Kwa kuwa nchi yetu imekopa matrilioni kujenga BWAWA la JNHP, na Kwa kuwa walipaji wa deni Hilo ni sisi wananchi, na Kwa kuwa majiko ya umeme Yana faida zaidi kimazingira, na Kwa kuwa Bei kubwa za luku ni chanzo kikubwa Cha kutotumika majiko ya umeme nchini Kwa wananchi wa kipato Cha chini,

Na Kwa kuwa, mradi wa REA kuunganisha vijiji Kwa huduma ya umeme umewafikia wengi, uwezekano wa kutumia umeme kupikia ni mkubwa zaidi.
Upo sahihi ila tuna laana ya kudumu
  1. Rejea wimbo wa gas ya Mtwara walisema bei itashuka kumbe kuna mtu ameiuza
  2. Rejea ya yule aliyeficha fedha China huku akiwa mwanasheria mkubwa tu
  3. Hili Bwawa lina umeme mwingi lakini subiri sarakasi zake zitavyokuwa
 
Upo sahihi ila tuna laana ya kudumu
  1. Rejea wimbo wa gas ya Mtwara walisema bei itashuka kumbe kuna mtu ameiuza
  2. Rejea ya yule aliyeficha fedha China huku akiwa mwanasheria mkubwa tu
  3. Hili Bwawa lina umeme mwingi lakini subiri sarakasi zake zitavyokuwa
Saizi waliokuwa mbele kupinga ujenzi wa JNHP,

Leo ndio wako mstari wa mbele kutafuta wanunuzi wa umeme Toka nje ilhali Mwananchi wa kawaida hata kuwasha tu fridge anaogopa akihofia gharama kubwa ya luku,

Bei zikishuka, hata maskini atamudu kugandisha ice cream na kuuza Ili kuongeza kipato Cha family.

CCM Ina muda, haitodumu milele,

Thread za namna hii zitakuja kufufuliwa na kufanyiwa KAZI Kwa Maslahi mapana ya nchi,

Tusubiri!!
 
Back
Top Bottom