Baraza la Wafamasia kwa nini hamtoi matokeo?

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,401
4,144
Ni muda mrefu tangu mwezi wa pili kama sio januari tangu mitihani ya leseni ifanyike.

Nauliza hivi hakuna mkataba wa huduma kwa mteja? Hivi ninyi mnaweza kuamua tu mkusanye pesa halafu mnakaa kimya tu hadi mtakapojisikia kusema?

Hivi hata taarifa tu tangu muda wote huo,hamtaki kutoa?Mbona mnakuwa miungu watu katika ofisi zenu?

Nawaomba mjitokeze mtoe taarifa ili watu wajue wanafanya nini
 
Ingia kwenye tovuti ya Baraza, hata hivyo nyie si ndo wale mitihani yenu mnafeli hovyo!
 
Paper lilivuja na inawezekana mkarudia mtihani mkuu, hivyo be patient.
 
Pongezi nyingi kwao kwa kufuta baadhi ya matokeo kwa mitihani iliyovuja maana nchi sasa ni academic forgery na fraud iliingia kwenye taaluma.

Ni muhimu watu wajifunze kwa wenzetu huku jinsi walivyo makini kwenye udanganyifu katika taaluma na wanavyolivalia njuga bila kujali ni nani kafanya wala ana nafasi gani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom