Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,847
- 15,260
Kituo kikuu cha mabasi ya kwenda mikoani kilichopo jijini Arusha kimekuwa kero kwa watumiaji wake kutokana na adha mbalimbali zinazowakabili abiria pamoja na wanaowasindikiza.
Kituo hicho kikuu cha mabasi kipo hapo tangu uhuru hadi na sasa kitu ambacho hakiendani na hadhi ya leo hii kutokana na changamoto lukuki zilizopo kituoni hapo.
Moja ya changamoto zilizopo kituoni hapo ni usalama mdogo wa abiria na mizigo yao na hii inatokana na Kukosekana kwa uzio Kuzunguka kituo hicho.
Kukosekana kwa huduma muhimu kama vile choo, sehemu ya kujikinga mvua/jua ni moja ya changamoto muhimu inayoikabili kituo hicho.
Makundi ya vibaka, matapeli. Wahuni na madalali wasiokuwa waaminifu wamekuwa wakishinda katika eneo hilo la kituo kutokana na Kukosekana kwa miundombinu rafiki kituoni hapo.
Udogo wa kituo. Haukidhi idadi ya mabasi yaliyopo kulinganisha na hali ya maisha ya sasa ambapo idadi ya wasafiri ni wengi kulinganisha na miaka iliyopita, kituo hicho kwa sasa hakiwezi kukidhi mabasi 20 kwa wakati mmoja.