"Aliou Sawadogo" kijana wa Burkina Faso aliyeitungua "Drone" ya Ufaransa kwa manati

Juma Wage

Member
Sep 8, 2023
60
202
Novemba 24, 2021 Kijana wa miaka 13 raia wa Burkina Faso, Aliou Sawadogo akiwa na manati yake porini akiwinda ndege, aliona kitu kikiambaa angani.

Sawadogo akatoa jiwe kutoka katika kaptula yake kisha akaliweka katika kigozi cha manati na kuanza kutafuta shabaha.

Akavuta pumzi na kuzishusha kwa kuachia jiwe lililoenda kuidungua ndege nyuki (drone) iliyokuwa angani.

Ndege nyuki hiyo ilikuwa ikipiga picha za kijasusi ambazo serikali ya Ufaransa huzitumia kwa manufaa yake.

Baada ya kuidondosha "drone" hiyo akaiokota kurudi nayo mjini.

Wananchi wakamtunza tuzo ya ushujaa kwa kumuinua juu kisha kuzunguka naye mitaani huku wakiimba nyimbo za kumsifu mtoto huyo.

Ndimi Juma Wage
Dodoma.

IMG-20230911-WA0093.jpg
Screenshot_20230916-231905.jpg
 
Tunajifunza kutokana na Makosa. Hayakusemwa ni Makosa ya nani, yaweza kuwa ya kwetu au ya wengine.

Muhimu ni kujifunza (funzo).

Kijana alistahili zaidi ya hicho, huenda walimpatia maana taarifa zaidi kumuhusu huyo dogo zimekuwa ngumu kupatikana.
Huyo dogo alitakiwa awe viunga vya jeshi, kama bado mdogo, awe shule za jeshi
 
Back
Top Bottom