Hawa ndio vijana ambao, mchango wao kwa Taifa hili ni mdogo sana! Unashindwa kujenga hoja unaanza kumshambulia mtu kwa matusi! Ndio hawa wakipewa nchi itagawanyika vipande vipande! Mawazo mbadala yanaruhusiwa lakini sio kutukana,.
Umenena mtaalam! Mchezo kutumia nguvu na akili kama kweli amepata sehemu inamlipa aende, maisha yake yanapita ila Simba ipo tuu! Akapige pesa atengeneze maisha huu ndio wakati wake!
Hii ni hitilafu iliyojitokeza kwenye miundombinu ya umeme sio mgao wa umeme! Ingekua ni mgao wasingekata usiku wa manane. Tuwe na mawazo chanya sio mawazo hasi siku zote!
Nina fundi wangu mmoja ninamkubali ila anasema engine za Mazda zina changamoto sana, toka zimeanza kuingia kwa wingi hizi Mazda anasema zimeletwa kwake zaidi ya nane kwa matatizo engine tena zote namba E'! Ni kweli au hao watumiaji hawana uelewa nazo.?
Tuheshimu mpira wa miguu tuache ushabiki, tuchambue mpira kwa kuangalia viwango vya ubora wa wachezaji ndio tuje na hitimisho la michezo yote kwa timu zetu mbili Simba na Yanga! Kiukweli kabisa Yanga hawana deni hapa walipofikia ila wanaweza kwenda mbali zaidi kutokana na ubora walionao...
Ni kweli mtaalam, tatizo la Simba maamuzi yana mlolongo mrefu na kuna watu wengi wanakula cha juu hapo, tofauti na Yanga, pesa inatoka kwa Gharib moja kwa moja kwa Engineer kutafuta wachezaji!
Timu hii ina mlolongo mrefu sana wa watu wapigaji! Pesa hadi ikifika kwenye malengo husika imebakia ngozi tu, ndio maana kila siku huleta wachezaji wasioeleweka! Yanga pesa ikitoka kwa Gharib moja kwa moja kwa Engineer nae moja kwa moja sokoni!
Kivuko cha Magogoni kilikwenda Kenya kutengenezwa mwezi tatu, tuliambiwa kitakamilika ndani ya miezi mitano! Sasa mwaka sasa unakaribia, Watanzania na Tanzania yangu Mwenyezi Mungu aendelee kutulinda! Mungu Ibariki Nchi Yangu [emoji1241] Mungu Ibariki Afrika!!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.