Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,709
- 13,461
View: https://www.youtube.com/live/R29ql0qn41I?si=HUvsJC1La1-T6RWb
Viongozi mbalimbali pamoja na Waigizaji wakiwa kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Mafanikio yaliyopatikana kufuatia Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea kuanzia tarehe 31 Mei, 2024 hadi tarehe 05 Juni, 2024.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 06 Juni, 2024 kuhusu masuala mbalimbali ya Teknolojia ya Mawasiliano wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji), Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na Waandishi wa Habari Ikulu, Dar es Salaam Juni 06, 2024 kuhusu masuala ya Uwekezaji wakati wa Ziara Rasmi ya Kiserikali aliyofanya Rais Samia Suluhu Hassan, Jijini Seoul, Jamhuri ya Korea.