Zitto: Hali mbaya ya uchumi, watu hawasafiri wala hawauzi, tutaangamia wote, mabenki yanauza nyumba

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
Jana nilikuwa nazungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa Kigoma kuhusu hali za biashara zao. Msafirishaji mmoja ( transporter ) kaniambia siku hizi hawezi kufikisha abiria 20 katika basi la abiria 55 kutoka Kigoma kwenda Dar. Hii ni Kwa sababu wananchi hawana fedha na hivyo hawasafiri.

Nimeambiwa kuwa huko Kasulu mawakala wa pembejeo za ruzuku wanaoidai Serikali wameanza kupata misukosuko ikiwemo nyumba zao kupigwa mnada na mabenki. Kasulu peke yake nyumba 5 zimeshapigwa mnada mpaka sasa.

Serikali itazame masuala haya maana yanarudisha watu kwenye umasikini. Kuna haja ya Wabunge kuisimamia Serikali Kwa umadhubuti kwenye suala zima la Uchumi. Kitaani hali ni mbaya Sana
 
Ninawashangaa sana wabunge wetu sijui wamerogwa na haya magwanda ya kijani???. Kwa kweli watu wanaopaswa kulaumiwa ni CCM kwa kutofanya upepmbuzi vizuri wa nani awe Rais. Tutakuja simama juu ya makaburi yao na kutoa makufuru makubwa kwao.
 
hio ishu ya mabasi nilisikia habari maali mabosi wengi wamepaki magari yao kwasababu ni hasara kuingiza magari barabarani alafu abiria wachache kuliko gharama ya usafirishaji
 
Nimeanza kuangalia Tamthilia inaitwa THE YOUNG POPE, hakika wandugu anayofanya huyo papa hayana tofauti kabisa na anayofanya baba hapa nyumbani, majivuno, kiburi na kutoshaurika.........naye kama alivyo dingi yetu kuna mahali anasema watamkoma maana hakuna aliyemsaidia kupata huo wadhifa.....wakuu mkipata muda iangalieni, imechezwa na Jude Law na kutengenezwa na HBO........munaojua Series munafahamu jinsi gani HBO wasivyobahatisha.
 
Acha tu tuisome kisha
badae akili zitawarudi tu
Mlimchagua Msukuma ambae akifika kwake akiona
meza imejaa vyakura anajuwa wote tunakula hivyo hivyo,
Ndio mwaka mmoja tu, baada ya muda wote mtakuwa barabarani kuandamana.
 
Mliompigia kura au kumsapoti kwa namna yoyote ile nadhani mnajuta saiv na nyoyo zenu
 
juzi mkuu alitwambia kuwa mitandao ya kijamii inafanya kazi ya udaku na sio kutoa mawazo ya maendeleo, wakati tumeandika mara nyingi sana kuusu bandari na njia ya kuirudisha katika hali yake, hamna jipya, tukapiga kelele hela zirudishwe kwenye mabenki ila ziwe monitored vizuri , hamna kitu, tukapiga kelele kuwa private sector inakufa , sasa ni lipi utatusikiliza?
 
Mkulu anatupeleka wapi? Mbona kama hana hata huruma na wananchi wake?
Mojawapo ya haruf.ya serikal za kidikteta ni kuwafanya masikin wananchi na kufanya nguvu kubwa kuwaziba midomo wapinzani na kufanya nguvu kubwa wananchi wasijue haki zao ikiwemo katiba ya nchi ndo mana hapa nchini anaishia kusema katiba sio priority
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…