brasy coco
JF-Expert Member
- Apr 25, 2012
- 1,489
- 900
Na Salmin Botea
Hilo ni swali ambalo nmekuwa nikikutana nalo sana au kulisikia watu wakijiuliza, nami nikaona nfanye utafiti ili nijue kwanini Mkuu wa Mkoa wa Mjini magharibi ni kipenzi cha vijana na makundi ya watu wote?
Ili kupata jawabu hili kwanza ikabidi niangazie waliomtangulia kabla yake katika nafasi ile, nkaona utafauti mkubwa sana.
Nikarudi kwa Rc Ayoub anafanya nini kipya, au ana tabia zipi ambazo labda vijana wakavutika sana na utendaji wake?
Mambo ya kipekee ambayo Mkuu huyu wa Mkoa wa Mjini au napenda nimwite sasa "Simba wa Mjini" anayo ni;
1. Mkweli
Vijana wengi hawapendi kudanganywa, kutumiwa na kisha kutupwa kama ganda la muwa, RC Ayoub akapass kwenye hilo, ni kiongozi mkweli mwenye uaminifu wa kipekee kabisa, hasemi kitu hasichoweza kukitenda na wala akisema akangeuki kile alichokisema au kukitolea ahadi, Kwa tabia hii vijana wengi wakampenda sana simba huyu wa mjini.
2. Mtendaji
Jambo ambalo ni geni kwenye afisi yake kwa miaka ya nyuma ni kukuta afisi ya Mkuu wa Mkoa ina hudumia wananchi mpaka saa 5 za usiku, hili jambo ni geni lakini simba huyu wa mjini yeye kwa imani kubwa, huruma, uadilifu wa hali ya juu kwa kuwajali wananchi wake anafanya kazi za wananchi mpaka saa 5 za usiku, wakati mwingine mpaka saa 8 za usiku yuko katika kazi za wananchi wake na hata wasio wananchi wake kwake kila mtu anastahili huduma yake, hili ni moja ya jambo ambalo vijana na makundi mbalimbali yakamshangaa RC huyu wa mjini wakajikuta wakimjaza moyoni kwa mapenzi ya dhati kwa utendaji wake pamoja na uadilifu wa hali ya juu.
3. Muadilifu
Uwezi kuvutia wengine kama huna sifa hii, kwake Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi ndiyo kitu cha kipekee uadilifu, kuheshimu kazi yake, kuheshimu anawaongoza, kutotumia cheo chake kujilimbikizia mali au kufanya dhurma, Mkuu huyu kajiepusha nayo, uadilifu huu ukawavutia wengi kumpenda.
4. Mwenye Maono
Maono ni picha inayojengeka katika fikra ya matokeo ya jambo ambalo linapangwa kutekelezwa.
Kama wewe ni kiongozi asiyeweza kuona picha ya baadaye ya sehemu unayoingoza basi viatu ulivovaa havikutoshi.
Ndiyo havikutoshi!
Rc Ayoub ni mtu mwenye maono sana, na maono yake haya ndiyo yanamfanya kufanya kazi zake ziende sawa sawia, kwa maana picha aloijenga namna ya mkoa wake uwe, na namna ya watu wake wawe ndiyo anayoifanyia kazi sasa kwa vitendo ambavyo wengi wetu tunaendelea kuviona, Vijana wakatambua ya kuwa Simba huyu wa Mjini ana maono ya kipekee.
“Kiongozi ni yule anayejua njia anayokwenda, na kuionesha njia.”
RC Ayoub amezionesha na anaendelea kuzionesha kila kukicha
5.Jasiri
Uwezi kuwa kiongozi bora kama hutakuwa na ujasiri katika maswala mbalimbali. Unahitaji ujasiri kufanya maamuzi mbalimbali, yapo mambo ambayo wengi awakuyazoea lakini kwa vile simba wa mjini (RC Ayoub) tayari ana maono yapo mengi aloyafanyia mamuzi yenye ujasiri ili kuwaletea maendeleo wananchi wake, ujasiri huu wakipekee umemfanya RC ayoub kuwa nae Mkuu wa Mkoa bora na wakipekee kuwahi kutokea.
6. Subra
Kuna mambo yanayohitaji subra katika maisha. Kiongozi asiye bora hutaka kila kitu kitimie kwa siku moja. Kuwa kiongozi mkomavu ni kuwa na subra na uvumilivu.
Mkuu wa Mkoa wa Mjini ni mtu mwenye subra sana na subra yake inamfanya hata mambo yake anayopanga leo akitaraji yatimie baada ya miezi sita, sio mtu mwenye pupa anafahamu nini anatenda, alazimishi kila kitu kifanikiwe kwa siku moja, lakini subra hii pia ameonesha hata kwa maadui zake ambao wamekuwa wakimshambulia, na wengine kufanya mbinu za kumdhoofisha utendaji wake, lakini baada ya kufatilia nikagundua kuwa RC ayoub moja ya wosia alopewa na wazee wake kuwa
"Mwanangu jifunze kukaa kimya, si kila kitu ujibu"
Hivyo subra yake na mafundisho alofunzwa kwao vinamfanya hata kutojibu wanaomshambulia badala yake yeye yuko busy na kazi zake ndiyo majibu yake.
7. Mbunifu
“Ubunifu unatofautisha
kati ya kiongozi na mfuasi.”
Ubunifu ukamfanya kuwa wapekee na kujitafautisha na wengine, ubunifu ukamfanya kuvutia wengi na wengine kujifunza kupitia kwake, ubunifu ukamfanya kuonesha ari na nguvu ambayo uwenda vijana walitamani siku zote, ubunifu wa kuleta fikra mpya na zenye matokeo chanya, ubunifu wa kiutendaji wenye kuja na faida nyingi nyingi kwa wananchi wake simba wa mjini.
8. Uwajibikaji
“Uongozi ni kuwa mtumishi kwanza.”
Ukitaka kuwa kiongozi bora huwezi kujitenga na uwajibikaji. Lazima uwajibike kutimiza majukumu yako yote.
Utawezaje kuwaongoza na kuwahimiza wengine kutimiza majukumu yao kama weye mwenyewe huwezi kutimiza majukumu yako?
Uwajibikaji wa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Mh. Ayoub ukawavuta vijana wengi sana nao kuanza kuwajibika kwa Taifa lao, na hilo haikuja kwa bahati mbaya hapana! Imekuja baada ya kumuona simba wa mjini namna anavyowajibika kwa kuwatumikia wananchi wake, imekuja baada ya kuona aliyepaswa kubweteke abweteki anapiga kazi usiku na mchana, imekuja baada ya kuona RC Ayoub anavoumiza kichwa awafanyie nini wananchi cha kuwaletea maendeleo, akageuka kutoka kuwa boss akawa mtumishi wa wananchi kweli kweli na kutimiza kiapo alichokula. Katika kuchimbua chimbua nilikutana na Kijana mmoja akanambia
"nliwahi kwenda kwa RC Ayoub afisini kwake muda nloenda ni nje ya kazi nmeingia afisini kwake saa 4 usiku, niliamni kabisa atakuwa amechoka sidhani kama atanipokea vyema, lakini nilishangaa akanikaribisha kwa ucheshi akaonesha umakini wa kunisikiliza na kunipa suluhisho la suala langu vizuri tu, namini alkuwa amechoka lakini tu hayuko tayari kumkera mwananchi wake yule ni zaidi ya kiongozi" alimaliza kijana huyu mkazi wa Magomeni Zanzibar.
9. Nidhamu
Kuna mambo ambayo huwezi kufanya unapokuwa kiongozi hata kama wengine wanayafanya au unavutiwa nayo. Siku zote epuka tabia zisizo endana na kiongozi bora kama vile ulevi, umbeya, uvivu, anasa, starehe kuongea hovyo n.k.
Haya Mkuu wa Mkoa wa Mjini akaepukana nayo, nidhamu imekuwa ngao yake, na nidhamu hii anayo mpaka kwa anawaongoza.
10. Hana majivuno
Tabia mbayo watu wengi hawaipendi basi ni majivuno, kiongozi mwenye majivuno uwa mbali na anawaongoza, hii imekuwa tafauti na kwake simba wa mjini, si mpenda majivuno wala si mtu mwenye kujikweza, daima amekuwa mcheshi kwa wananchi wake, si jambo la ajabu akiwa katika ziyara zake akujuwi akakufata kukusalimia ni moja ya mambo ambayo watu wengi yamewavutia kwake.
11. Mawasiliano
Mawasiliano ni suala muhimu sana linalojenga utawala bora.
Mkuu wa mkoa wa Mjini magharibi Ayoub Mahmoud amejenga mfumo bora wa mawasiliano na anaowaongoza, mfumo huu umemfanya kuwa karibu sana na wananchi wake, na hapa niwapongeze sana wasaidizi wake wote, ukarimu wao, wepesi wao wa kurahisisha mawasiliano baina ya Mkuu wa Mkoa na wananchi kuwa bora zaidi.
Ahsante.