Zanzibar haina mwenyeji wa asili

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,818
5,420
Inashangaza sana kumuona mtu wa Zanzibar akimbagua mtu wa bara.

Zanzibar ni moja ya visiwa vinavyounda nchi ya Tanzania. Zanzibar ina utawala wake unaounda serikali ya Zanzibar.

Kiasili Zanzibar haina mwenyeji, watu wote na wakazi wa wazanzibar ni watu wa kuamia.

Wakazi wa Zanzibar kiasili ni watu wa bara, Watu wengi walijikuta kisiwani Zanzibar baada ya uhamaji ya watu wa bara hasa Wabantu waliokuwa wakiama kutafuta maeneo ya Uvuvi na kilimo. Wavuvi wengi kutokea bara walijikuta wakigota au kutia nanga katika kisiwa icho katika harakati zao za utafutaji ridhiki kwa njia ya bahari. Na kama unavyojua wavuvi uwa wana desturi ya kujenga makazi ya muda mfupi katika mwambao wa ziwa au bahari hili shughuli zao ziweze kwenda sawa. Hiki kitendo cha kutoka bara hasa Mombasa na Tanganyika kwenda kuvua katika kingo za bahari katika visiwa vya Zanzibar kulipelekea watu kuamia katika kisiwa hicho karne nyingi zilizopita ukisoma kitabu cha Bantu migration in Africa utaelewa zaidi.

Baada ya miaka kadhaa waarabu nao wakaanza kuwasili na mashua zao wakitoka Oman na yemen katika harakati zao za kibiashara nao wakatua katika mwambao huo wa visiwa vya Zanzibar wakifanya shughuli za kibiashara na wenyeji wa muda huo ambao walikuwa wavuvi kutokea bara walioweka makazi katika visiwa hivyo. Waarabu nao wakaweka makazi katika visiwa hivyo.

Baadae kwenye karne ya 7 na kuendelea ukoloni ukaaanza kushamili na watu wa bara wengi wakawa wanakamatwa na waarabu na kupelekwa visiwani humo kwa ajili ya shughuli na biashara za kitumwa chini ya utawala wa Kisultani ulioletwa na waarabu. Kitendo cha watu wa bara kupelekwa visiwani Zanzibar kulisababisha muingiliano wa watu wa bara kuwa mkubwa katika visiwa hivyo. Huku watumwa wengine wakisafilishwa kwenda mataifa ya jirani kama Comoro, na wengine kwenda urabuni, ulaya na Marekani kwa ajili ya utumwa.

Muingiliano wa waarabu na watu wa bara na kuzaliana ukasababisha watu kuwa wakazi wa Zanzibar.

Na kwa sababu watu hawa wa Zanzibar ni watu wa makabila mbalimbali kutokea Bara, hawakuweza kuelewana vizuri na kupelekea kuzalisha lugha mpya ya Kiswahili yenye mchanganyiko wa maneno ya lugha za kibantu, kiarabu, kiingereza na lugha nyinginezo.

Ukitaka kujua Zanzibar haina wenyeji asilia, ukikutana na Mzanzibari muulize wewe ni Kabila gani? Hili swali uwezi kujibiwa na Mzanzibari yeyote na ni kwa sababu Zanzibar haina makabila ya asili, wote walioko huko ni wa kutoka bara. Mababu zao walienda huko kwa shughuli za uvuvi au utumwa.

Wanzabari ni watu wa bara waliopoteza asili za makabila yao baada wa babu zao kwenda kuishi huko visiwani na kuchangamana na waarabu ambao walikuwa maboss zao. Wakaanza kuona nao na kuzaliana na ndio maana leo hii ukienda huko shombe shombe wa kiarabu ni wengi sana.
 
Sio kwamba historia ya asili yao hawaijui.

Wanajua zaidi na zaidi

Tangu wamezaliana na waarabu, wanajiona nao ni waarabu.

Yaani kwa ndani wao ni waarabu pure na kwao ni oman,

Kwa nje ni wabantu rojorojo ., sio watanganyika tena hao.
 
Hata Tanganyika pia ni watu wa kuhamia ukitaka kujua hivyo Adam na Eva waliishi wapi?
Ikiwa hawa tunawazingatia kama wanadamu wa mwanzo kwa mujibu wa imani zetu na vitabu vya dini vinaeleza hivyo.

Hivyo maeneo mengine yote yalihamia na wanaadamu kutoka kwenye asili ya mwanadamu wa mwanzo.

Kiufupi tusibaguane sote asili yetu moja.
 
Back
Top Bottom