Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,606
- 4,262
Kama
wamefuta matokeo ya uchaguzi halali bila kutumia kifungu chochote cha sheria toka kwenye katiba au hata kanuni za uchaguzi, Shein atashindwa kuteua makamu wa Rais KWA KUTUMIA MAMLAKA ALIYOPEWA?Pamoja na CCM kutangazwa washindi katika ngazi ya Urais,Uwakilishi na Udiwani,CUF hawaepukiki katika ustawi wa Zanzibar. Katika uchaguzi wa jana,CUF iligomea uchaguzi huo ingawa wagombea wao hawakuondolewa kwenye karatasi za kupigia kura.
Hali halisi hapa Zanzibar inaonesha kuwa CUF wanahitajika,kuliko wakati wowote ule,katika kutanzua mkwamo mpya wa kikatiba pamoja na kufanyika uchaguzi unaosifiwa kipropaganda. Hapa Zanzibar,kwa hali ilivyo kulingana na matokeo,hakutapatikana Makamu wa kwanza wa Rais.
Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar,makamu wa kwanza wa Rais anapaswa kuwa mgombea aliyeshika nafasi ya pili ambaye lazima awe amepata asilimia kumi ya kura zote halali. Kwa asilimia tisini na moja za Dr. Shein,hakuna mgombea aliyepata asilimia kumi. Ndiyo kusema,hata Hamad Rashid,ingawa ndiye aliyetangazwa wa pili,hawezi kuwa makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar. ADC ya Hamad Rashid haina hata Mwakilishi mmoja pia.
Katika kuliona hilo,leo hii hii,Rais mteule Dr. Shein na hata Hamad Rashid wamekiri uwepo wa mgogoro wa kisiasa. Kwakuwa CUF hawakushiriki katika uchaguzi wa jana waliouita batili,watashiriki kutafuta suluhisho? Hapa,wananchi karibu wote wako puzzled!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Zanzibar)