Uchaguzi 2020 Yaliyojiri Vikao vya CHADEMA: Tundu Lissu aibuka kidedea kuwania Urais wa Tanzania kwa kupata kura 405 dhidi ya Nyalandu 36 na Dkt. Majige 1

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,228
Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo imewapitisha Tundu Antipas Lissu Lazaro Nyalandu na Dr Mayrose Majige kusaka nafasi ya kuwania Urais Tanzania.

Katika kikao chake cha Kamati Kuu kilichomalizika usiku mnene majina hayo Leo yataletwa ndani ya Baraza Kuu ambao watakata mzizi wa Fitna kumpata Mgombea mmoja baada ya kupigiwa kura na jina moja kuwasilisha ndani ya Mkutano Mkuu kesho kuidhinishwa.

Yeyote atakayepitishwa na Baraza Kuu anafaa kuwania Urais Kama vigezo vilivyowekwa na kuchambuliwa na chama hicho.

CHADEMA.jpg

Stay Tuned.


UPDATES:



======

Ratiba ya leo Tarehe 3, Agosti 2020, Baraza Kuu la Chama litakutana katika kikao chake, ambapo litajadili masuala mbalimbali ikiwemo “kufanya mapendekezo ya wagombea wa Urais na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Zanzibar na kuyawasilisha katika Mkutano Mkuu kwa uamuzi,” inavyoelekezwa kwenye ibara ya 7.7.12(a).

Aidha, kwa mujibu wa ibara ya 7.7.12 (n) Baraza Kuu litajadili rasimu ya Ilani (manifesto) ya Uchaguzi Mkuu na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Mkutano Mkuu kwa maamuzi.

= > Viongozi Wakuu wa Chadema wameshafika hivyo shughuli rasmi inatarajiwa kuanza hivi punde. Kwa sasa Viongozi hao wapo mbele na Wimbo wa Taifa unaimbwa.

= > Baada ya wimbo wa taifa imefanyika dua kwa ajili ya kufungua Mkutano.

= > Baada ya dua utambulisho wa Kanda mbalimbali zilizohudhuria, Wajumbe wa Bodi ya Udhamini, Wajumbe wa kamati kuu na wageni waalikwa unafanyika.

Katibu Mkuu wa chama John Mnyika akabidhiwa kipaza sauti kwa ajili ya kuongoza mkutano
Nimesimama kufanya kazi mbili tu kwa sasa. Kazi ya kwanza ni kueleza hakidi ya kikao hiki. Baraza kuu letu kwa sasa lina jumla ya Wajumbe 456 wa kikatiba na mpaka nasimama kuzungumza na nyinyi jumla ya Wajumbe 367 sawa na asilimia 80.5wamekwisha ingia kwenye kikao.

La pili ni kueleza kwa muhtasari Ajenda za kikao hiki. Kikao hiki kina jumla ya ajenda saba;

Ajenda za Kikao/ Mkutano:
  • Ufunguzi wa Kikao ambao utafanywa na Mwenyekiti wa Chama (Freeman Mbowe).
  • Ajenda ya pili ni kuthibitisha ajenda zitakazofuata
  • Ajenda ya tatu ni kujadili rasimu ya ilanio ya Uchaguzi Mkuu kwa mwaka 2020
  • Ajenda ya nne ni kupendekeza majina ya Mgombea wa Urais, Mgombea Mwenza na Mgombea Urais wa Zanzibar
  • Ajenda ya tano ni kuthibitisha mikakati na rasilimali za kuendesha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2020
  • Ajenda ya Sita ni kufanya mapendekezo ya ajenda za kikao kitakachofanyika kesho
  • Ajenda ya saba ni kuhitimisha kikao.

Ufunguzi wa kikao

Freeman Mbowe
Kwa niaba ya chama kama kiongozi mkuu wa chama nachukua nafasi hii kuwapongeza kwa kukiimarisha chama na kukipigania chama wakati watesi wetu walitegemea mkate tamaa nyinyi mliopo katika ukumbi huu mmesimama kukilinda chama, mmekipigania chama, mmekuza thamani ya Chama chetu.

Na binadamu anasema kila jambo ni mpango wa Mungu. Yawezekana tulikwazika sana tulipoona baadhi yetu tuliowaamini na kufanya kazi pamoja wakikisaliti chama chetu, wakiisaliti dhamira yetu. Natambua ni namna gani tuliumia tulipoona Wabunge wetu wakitukana viongozi, wakikidhalilisha chama hiki. Hatukuwaombea mabaya kwa sababu anayetoa adhabu ni Mwenyezi Mungu. Lakini binadamu tunasema malipo ya dhambi yanaweza kuwa hapahapa na si lazima akhera.

Lakini niwaambie ndugu viongozi, hatuna sababu hata moja ya kusikitika. Waliokata shauri la kuondoka katika chama chetu hatuna sababu ya kujutia, tuna sababu ya kujifunza. Lakini tutambue wakati wote, chama cha siasa ni watu. Ili muweze kuwa chama kinachokua lazima utamaduni wa kuwapata wanachama wapya, viongozi wapya, watu wapya uwe ni utamaduni wa kudumu katika chama cha siasa.

Nasema hili kama kiongozi wa Chadema, kwamba chama hiki tumekijenga na kimefikia hapa kwa kuwa siku zote tumefungua milango. Tumeruhusu watu waje hapa kwa mamia, tumeruhusu watu waje hapa kwa maelfu. Chama hikitumekijenga kuwa chama cha watu na sio kikundi kidogo cha watu kinachojiita Chadema ambacho hakitaki kufungua milango wengine waingie. Tunatamani siku moja kila Mtanzania awe mwanachama wa Chadema.

Nimesikia kauli kutoka kwa viongozi mbalimbali wakitamka kuwa mtu yoyote akitoka Chama cha Mapinduzi asiingie katika chama hiki hiyo sio sera ya CHADEMA mtu akitoka chama chochote anakaribishwa CHADEMA lakini atambue akifika anawajibu wa kuishi kwa mila, desturi, katiba, kanuni na muongozo wa Chadema.

Tunapowakataa wanachama wa chama cha Mapinduzi eti kwa sababu tunasema tunasomo kutoka kwa waliotuhama je wakitupa kura zao tutazikataa au tutazikubali? Tunapoenda kwenye Uchaguzi Wapiganaji wenzangu, tunatamani kura za wote, wa CCM wasio wa vyama vingine, wasio na chama. Haiwezekani tukabaguana, tukawabagua wa vyama vingine halafu kesho tukawashawishi wakatupe kura zao.

Tunahitaji kujenga umoja wa chama wakati huo huo tukijenga umoja wa taifa. Inawezekana tukawachukia sana baadhi ya viongozi wanaofanya maamuzi katika Chama cha Mapinduzi lakini ikaja kama chama hatuwezi kuwachukia wanachama wote wa CCM kama ni maadui zetu.

Tunahitaji kujenga ushawishi wa kisiasa tunahitaji kuonesha upendo huo ndani ya nchi yetu. Tunataka tukiongoza nchi hii tuwe united as a country. Hatuhitaji tuongoze nchi ambayo imepasuka pasuka vipande vya kiitikadi. Tunahitaji umoja wa kitaifa tunahitaji mmoja, tunahitaji wawili tunahitaji Milioni moja.

Ndugu viongozi lazima tuendelee kukilinda chama chetu. Mimi kama kiongozi Mkuu wa Chama wakati wote nafikiria tufanye nini kukiimarisha chama hiki. Tufanye nini migogoro yetu ya ndani isikiumize chama chetu. Kwamba miongoni mwetu hakuna mbora kuliko chama chetu. Umoja wetu ndio nguvu yetu na hakuna kipindi kibaya cha kukigawa chama kama kipindi cha uchaguzi.

Chama hiki kinakuwa hakijawahi kuwa na historia ya kusinyaa. Ukitaka kupima ukuu Chadema leo, usipime propaganda za vyombo vya habari. Pima kwa kuangalia chama hiki kimesambaa mikoa mingapi, wilaya ngapi, majimbo mangapi, wilaya ngapi ndo namna ya kuipima Chadema. Kazi hiyo na matunda haya ni lazima tuyalinde kwa nguvu zetu kwamba yoyote asitutoe kwenye reli chaguzi zinapita na chama kitabaki na tunawajibika kukiacha salama. Matendo yetu ya leo yasitutoe kwenye dhamira hiyo.

Mwaka 2005 Chama hiki kilikuwa kidogo kwelikweli. lakini safari ile ndio ilikwenda kutufanya kuwa chama kikuu cha Upinzani. Kiukubwa tulikuwa chama cha nne. Lakini sisi tulisema tutakijenga chama hiki kwa kupokea yoyote anayetoka katika chama kingine ndio ilikuwa roho ya kuijenga Chadema.

Mwaka 2010 tukasema tufanye utafiti ni nani miongoni mwetu amabye tumtume akabebe bendera ya chama. Kila miaka mitano ya kisiasa ina dynamics zake. Hatulazimiki kutumia mbinu za miaka mitano iliyopita kukabili matakwa ya wakati huo. Tukampitisha Dkt. Wilbroad Silaa akiwa katibu wa Chdema alipendekezwa kuwa mgembea wa urais hatukumpigia kura Dr Slaa. Tulivyofika mwaka 2015 kwa mazingira ya siasa yalivyokuwepo tukakubaliana lile jina moja.

Naposema chama hiki kimekuwa ndugu viongozi kwa mara ya kwanza tunakwenda kwenye historia ya nchi yetu. Tunakwenda kwenye uchaguzi wa Urais na Madiwani tukiwa na wagombea katika majimbo yote 214 Tanzania Bara, kwamba chama hiki leo kinakwenda kuweka wagombea full house. Halafu anatokea mtu anasema chama hiki kinakufa inabidi tucheke kidogo.

Kwa upande wa Tanzania Zanzibar tuliweka malengo, tuliweka malengo mpango mkakati miaka mitano kwamba ikifika 2020 kwenye uchaguzi Zanzibar kwa maana ya Pembe na Unguja tuwe na uwezo angalau wa kusimamisha asilimia 50 ya wagombea wa Ubunge na asilimia 50 ya Wagombea wa udiwani wa wadi mbalimbali Zanzibar na asilimia 50 ya Baraza la Wawakilishi.

Hadi hatua ya sasa katika Majimbo 50 ya Zanzibar tayari tuna wagombea ambao wamepatikana katika Majimbo 38. Hii sio kazi ndogo kwa wale tunaojua siasa za Zanzibar. Katika Baraza la Wawakilishi lenye viti 50, hadi tunavyoongea tunawagombea katika viti 30 ambayo ni sawasawa na asilimia 60. Katika Wadi 112 za Zanzibar tuna Wagombea katika wadi 59 ambayo ni sawa na asilimia 53.

Katika Bara tuna kata 3956, navyozungumza hivi tuna Wagombea katika kata 3920. Kuna kata kama 40 tunakamilisha lakini mpaka tufike mwisho tutasimamisha Wagombea katika kata kwa asilimia mia moja na Ubunge asilimia mia moja.

Waheshimiwa Viongozi wenzangu, huko nyuma tuliingia katika mazungumzo na Vyama vingine. Miongoni mwa sababu ni unyonge wa Chama chetu katika baadhi ya maeneo, bado tunazungumza leo, tukishirikiana na Vyama vingine sio kwa sababu tumekosa Wagombea ila ni kwa sababu katika sehemu nyingine inawezekana kuna kiongozi wa Chama kingine akawa na nafasi zaidi ya kushinda kuliko Mgombea wa Chadema. Tukilazimika kufika hapo inawezekana baadhi ya nafasi tukaachia.

Sisi ni sehemu ya Watanzania, tusijenge tabia ya kujimwambafai na kujiona sisi ni bora kuliko wote. Yawezekana tukawa chama kikubwa lakini tumuheshimu kila mmoja wetu kwa ukubwa wake ama kwa udogo wake. Ukubwa wetu utujenge unyenyekevu na ukubwa wetu usitujenge kiburi. Tutapoona kuna sababu ya kushirikiana tutashirikiana. Tukiona kushirikiana hakuna maslahi kwa chama chetu na zaidi hakuna maslahi kwa nchi yetu tutafikiria tofauti.

Kwahiyo, sisi kama Chama Waheshimiwa Viongozi ni lazima macho yetu na masikio yetu yawe wazi. Hatutaingia tu kwenye ushirikiano kama Fasheni, tutaingia kwenye ushirikiano tu endapo kwa kufanya hivyo tutashirikiana na watu ambao wapo genuine, watu ambao wako serious na watu ambao hawatouza nchi yao tutaendelea na mazungumzo. Mazungumzo tunayoendelea nayo mpaka sasa ni ya Chama kimoja ambacho ni ACT Wazalendo.

Kwahiyo, ndugu viongozi hatukukijenga chama kwa bahati mbaya, tumekijenga kwa confidence na commitment. Tunamaliza mkutano Mkuu kesho tukiwa na mgombea mmoja. Tunahitaji tumalize mkutano mkuu wa kesho wa kesho tukiwa wamoja twende tukapambane tukiimba wimbo mmoja tukitamaliza mkutano mkuu kesho tutatoka na jina moja la mgombe na tukimaliza wote na wamoja tutoke tumeshikana. Fikiria leo unamkashifu na kumtukana mtu halafu kesho mnataka kunia mamoja.

Ni kwa nini tusijifunze kwa chama cha mapinduzi ambacho kimeshindwa kujenga umoja wao kwa makundi ua uchaguzi. Ni matumaini yangu wagombea wote watatu waliopendekezwa kwenda baraza kuu tutafanana katika hili. Natamani katika muda uliobakia tukaitengeneze amani. Tukaitengeneze amani katika chama hiki tusijenge makundi. Nguvu yetu ni umoja wetu tutoke hapa na nyuso za furaha tumpate mgombea wetu kwa furaha na sio kujenga mpasuko.

Ni vyema tuwe na akiba kwa hiyo kila mmoja kwenye chama chetu ni wajibu wetu kumpigania na kumpendekeza anaemtaka. Sisi ni familia ya Chadema na familia inaimirika wakati wa majaribu. Huu ni wakati wetu wa majaribu na tuioneshe dunia sisi tutaimarika zaidi wakati wa majaribu.

Nimalize kwa kuwaambia Viongozi tumeonewa sana tumebezwa sana tumefungwa sana uchaguzi huu tukaseme enough is is enough kwa kiswahili tunasema sasa basi. Nikisema tumeonewa sana sasa sasa baasi.


LAZARO NYALANDU ANATOA HOTUBA YA KUOMBA KURA
Asema mimi nilikuwa kipofu nilikuwa sioni ni kama yule kipofu anaelezwa kwenye biblia baadaya kupakwa matope na mzee wa siku akaona tena.

Na mimi nimeguswa tena katika hiki chama naomba mkiona vyema mnipe nafasi ya kusisimama kama mgombea uraisi wa CHADEMA.

Nasema uwezo wa kuiondoa CCM tunao na tupate Urais madiwani na wabunge wa kutosha nipo tayari na nimejiandaa tufanye kampeni kwenye majombo manne kwa siku twende ardhini twende kwa anga na kwa maji.

Turudishe tena tabasamu la wazee wetu tunataka wazanzibar wamiliki tena rasilimali zao za mafuta na gesi na uchumi wa baraza kuu.

Tunataka CHADEMA wasiisome namba tena nao wana CCM wasiisome namba tena na watanzania wasiisome nammba tena, watanzania watamiliki rasmi rasilimali, tutahakikisha tunapunguza madaraka rukuki ya rais, na tutaandika upya katiba ya Tanzania tukianzia na rasimu ya jaji Warioba tutaanzisha benki ya vijana tutaanzisha tena bima ya afya.

Tutashusha kodi, tutaimarisha uchumi wa nchi yetu, tutarekebisha ubora wa elimu kote nchini na tutashirikiana na wanachama wetu tutashusha kodi na kuongeza uzalishaji na kuimarisha ushiriki wa wanawake katika uchumi na uzaishaji kote nchini. Na tutahakikisha CHADEMA inaendelea kukua kutoka utukufu hadi utukufu.

Nilijiunga na CHADEMA 2017 na nikawa kiongozi wa kawaida nikawa mjumbe wa
Kamati tendaji ya Wilaya Singida kasikazini.


TUNDU LISSU ANATOA HOTUBA YA KUOMBA KURA

Kabla siajaenda mbali sana, ninaomba nianze kwa kusema kwamba nimepata fadhaha kubwa jinsi ya Kuwaita nyinyi wote mliokusanyika hapa katika ukumbi huu kama baraza kuu la Taifa la chama chetu. Katiba yetu ya chama inawaita wote wajumbe wa baraza kuu la taifa. Hata hivyo,
tangu kura za maoni zianze kwenye Chama cha Mapinduzi na wajumbe kuwapiga spana wale wagombea wajasiliamali wa kisiasa was aliosaliti harakati za kiukombozi ambazo ziliongozwa na chama chetu na kuunga mkono juhudi. Hali ilikuwa mbaya kwa wajasiliamali hao wa kisiasa, kiasi kwamba mmoja wao alisikika akisema kwamba wajumbe si watu. Kwasababu ya maana hii mpya ya neno wajumbe ninaomba mniuie radhi na mnirushisu nisitume ni neno wajumbe. Badala yake ninaomba niwaite nyinyi wote viongozi, ili niweze kujinusuru kutoka katika masahibu ya kupigwa spana na wajumbe kama wale waliokimbilia CCM.

Wheshimwa vioongozi, nilipotangaza nia yangu ya kugombania u Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa niabaya Chama Chetu, mnamo tarehe 08/06/2020. Nilieleza kwa kirefu kidogo ajenda mahususi za uchaguzi mkuu huu na kwanini ninaamini kwamba ninafaa kupewa dhamana huyo na Chama Chetu.

Watia nia wengine pia walishatoa maelezo yao kuhusu jambo hili. Leo mbele yenu viongozi wa barazakuu la Taifa, ninaomba nisirudie yale niliyoyasema 08/06/2020. Maswala hayo yote na mengine mengi yamefafanuliwa kwa kirefu katika ilani yetu ya uchaguzi mkuu ambayo tutaipitisha leo.

Na ilani hiyo na agenda zake zote ndiyo itayokuwa agenda mahsusi ya kwangu ambapo mtanipa ridhaa ya kupeperusha bendera ya chama chetu leo.

Ninaomba mniruhusu viongozi nielezee aina ya uchaguzi mkuu tutakao kuwa nao mwaka huu. Na aina ya mgombea wa Chadema anaehitajika kukabiliana na uchaguzi huo. Ili kukiletea chama chetu ushindi.

Waheshimiwa viongozi, uchaguzi mkuu huu utakuwa mgumu kuliko uchaguzi mkuu mwingine wowote katia historia ya mfumo wa vyama vingi vya siasa katika nchi yetu. Mheshimwa Mwenyekiti, katika mazingira haya halisi. mgombea au kiongozi wetu atakaegombea anatakiwa kuwa mgombea wa aina gani.

1. mgombea wa Chadema lazima awe mwenye historia ndani na nje ya chama ya kuaminika kwa msimamo wake.

2. Pili ndugu mwenyekiti, mgombea Uraisi wa Chadema awe ni yule mwenye uwezo wa kuunganisha nguvu kubwa ya umma inayohitajila ili kushinda uchaguzi mkuu huu. Hatutashinda kwa mvua za kawaida za masika ya kiuchaguzi, tutashinda kwa kutengeneza kimbunga cha wapiga kura a umma wa Watanzania. Amacho yeyote atakaejaribu kukizuia kitamsomba na yeye mwenyewe. Kimbunga hicho cha kisiasa hakiwezi kutengenezwa na mgombea asiye kuwa na hitoria yeyote ya mapambano ya kidemokrasia. Asiyekuwa na msimamo unaoeleweka na ambae uwaminifu wake ni wa mashaka.

3. Waheshimiwa viongozi, tunahitaji mgombea atakae we za kwainua wagombea ubunge na udiwani wa chama chetu. Mgombea asiye weza kuamsha hisia za wapiga kura hataweza kuingiza watu wetu barabarani. Kwa idadi inayohitajika pale kura zetu zitakapoibiwa au pale ambapo wagombea wetu walioshinda watakapodhurumiwa.

Matokeo:
IMG-20200803-WA0016.jpg

Matokeo ya kura Baraza Kuu yamempa ushindi Tundu Antipass Lissu kwa asilimia 91% ambapo jina lake kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu kuidhinishwa.

Jumla ya wapigakura 442

Hakuna kura iliyoharibika

1. Tundu Lissu kura 405

2. Lazaro Nyalandu kura 36

3. Dkt. Mayrose Majinge kura 1

Mara baada ya kutangazwa matokeo ukumbi ulilipuka kwa Shangwe huku Lazaro Nyalandu akiahidi Baraza Kuu kumuunga mkono Tundu Lissu kwa asilimia zote.
 
Mpaka hapo Nyalandu kashinda, Lisu hana uwezo wa kupambana na Nyalandu, Nyalandu ana pesa za kampeni wakati Lisu kapuku hana kitu
Kigezo chako ni pesa za kampeni, vipi Tanzania yetu?

Bara letu litaendelea kuendeshwa na mabara mengine kama tutaendelea na ubinafsi wa aina hii. Nyalandu au Membe wa Act ni watu ambao watatubakisha kwenye business as usual.

hatutasonga popote, tutajikuta tunashangilia tena uchumi wa kati kutoka matangazo ya world bank huku hali zetu zikiendelea kuwa duni.
 
Back
Top Bottom