Wizara ya Afya na TAMISEMI mmetukosea sana Idara ya Afya Halmashauri ya Wilaya Kibiti

nditolo

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
3,718
4,257
Katika hali ya kushangaza wizara na TAMISEMI imetuletea DMO kutoka Mtama DC.

DMO huyu alikuwa na tuhuma lukuki huko alikotoka na ikafikia madiwani kuazimia kumtoa madarakani lakini cha kushangaza mnatuletea huku.

Ilishindikana kuteua Daktari yoyote ndani ya halmashauri yetu mpaka mkaamua kutuletea mtu huyu. Huyu mtu amutuhumiwa na kuandikwa mara kadhaa kwenye kurasa za kigogo ikionyesha kufanya ufusika na watumishi na kuchonganisha watumishi kwenye vituo vya kutolea huduma.

Sasa na sisi mnataka kutupeleka huko?

Huyu mtu ni mgomvi mfitini na mwenye hulka ya kukurupuka.

Huko aliotoka aliteua CHMT ya kumkusanyia posho, watu wakienda safari za kikazi wanaleta posho mezani. Ameiacha CHMT ambayo aliiteua bila kuzingatia viwango vya elimu.

Ngoja tuone! Lakini kwa malengo mazuri ya Idara yetu hapa Kibiti Mtoeni kabla hajaharibu.
 
Badala ya kulalamika ilipaswa muanze kuishi nae ndio mumuone ili hata kama akiendelea basi isiwawie vigumu kutoa malalamiko,

Sasa ukishakuwa na mtazamo wako tayari kichwani basi hakuna jema kila litakalofanyika basi utaoanisha na yale uliyoyasikia

Mpeni muda!!
 
We nditolo mbona hii taarifa imekaa kinafiki na kikuda sana. Kunawezekana wewe upo mtama dc unaamua kumwagia upupu huyu mtu. Utachelewa sana kimaisha acha ngebe mpechempeche.
 
Mbona Una taarif zake nyingi ? Nin kimepelekea wewe kumfaham kiasi hicho ?

Nchi hii kila Kona majungu Tu, Kama hiyo nafasi ya DMO uliitaman basi endelea kuitaman
 
Daaah.
Wawaweza kuta Mletq mada unamsagia mwamba kunguni kwa habari hewa. Pole kwa DMO Kupelekwa KIBITI ni somo tosha kwake
 
Afike mumuone utendaji wake...

Mtu hajaanza kazi hapo na tayari mmeshakuwa na "negative attitudes and prejudices"....

Huu si usomi...
Huu si uungwana....

#Kusoma ni kuelimika

#Nchi Kwanza
 
Back
Top Bottom