Wimbo wa Taifa na Bandera: Cassian Chibogoyo Anajikanyaga Kanyaga na Kujiuma Uma Clouds TV!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,679
119,316
Wanabodi,

Naangalia Clouds TV kipindi cha 360 Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Cassian Chibogoyo Anajikanyaga Kanyaga sana na Kujiuma uma kuhusu mamlaka ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali kupiga marufuku matumizi ya wimbo wa Taifa na bandera ya Taifa.

Kiukweli jamaa amechemsha big time pale alipoulizwa ni sheria ipi inayompa mamlaka yeye kutoa amri ya matumizi ya bendera na wimbo wa taifa, ameshindwa kuonyesha akaishia kusema kuna mambo yanaandikwa na kuna mambo hayaandikwi.

Watangazaji wakamuuliza mbona Kikwete alihamasisha uzalendo kuwataka vijana walipende taifa lao na kuipenda bendera hadi kuivaa kama leso, iweje yeye apige marufuku? . Jamaa kashindwa kujieleza.

Lengo la Mpigachapa Mkuu wa Serikali kwenda Clouds TV ni zuri kuelimisha kuhusu uzalendo katika matumizi ya wimbo wa taifa na bandera, tatizo hakujipanga kikamilifu, tuligemea aje pale aeleze kutoka kichwani as a knowledgeable person yaani mtu anayejua kutoka kichwani na sio kuja na lundo la makaratasi hata kueleza tuu katiba mtu anasoma kutoka kwenye makaratasi katiba ni nini wakati ni abc tuu za mtu anayejua anayejua anazungumza nini from his finger tips.
Paskali
 
Hujamtendea haki ilibidi useme ni wapi kakosea.HALAFU utakuta watu wanakusifia habari hii imeletwa na mwandishi nguli wa Tanzania Pascal Mayala!!!.Uandishi wako ni janga la kitaifa.Kama wewe nguli unaandika hivi uuuuu ni aibu kwa tasnia ya habari.Halafu mnalalamika kuwa mnadharaulika.Kwa uandishi koko kama huu kuna mtu ataheshimu waandishi kama wewe?
 
Kuna mambo yanashangaza, wakati nchi nyingine wanajivunia bendera za nchi zao, huzivaa nk hapa kwetu no. huo uzalendo tunaotaka utakujaje kama hatuipendi bendera yetu? Kama ni sheria inakataza, imechelewa sana kufutwa katika vitabu vyetu vya sheria.
 
mmmh! nadhani umemshambulia Paschal bila sababu. kipi kimekuudhi katika andiko lake,labda ungesema angefafanua lakini hayo mengine umemshambulia pasipo na haja ya kufanya hivyo.
 
Nchi ya kupiga marufuku hii.

Wanadhani hata wasipopiga marufuku watu watavaa vitu vyenye bendera ya TZ?
 
Huu wimbo wa taifa wa Mungu ibariki......... haujakaa poa kabisa.

Bora ule wa Tanzania Tanzania.......maana una viashiria vya uzalendo na unakumbusha wajibu wa mtanzania kama raia.
 
usi mu attack mwandishi mwenzangu jibu hoja aliyoileta
 
We ambacho hujaelewa apo nini!!
 
Chibogoyo ameshindwa kujibu maswali amebaki kusema katiba, katiba, katiba,
Hivi katiba inakataza mtu kupeperusha bendera ya taifa lake kwa vyovyote vile bila kuvunja sheria?
Bendera na nyimbo ya taifa tumefundishwa mashuleni tena from foundation ina maana hii ipigwe marufuku?

Wanamichezo wakienda nje wanabeba Bendera ya taifa, wanaimba nyimbo ya taifa, mashabiki wanavaa nguo zenye bendera ya taifa lao, vipeperushi vyenye kuonyesha utaifa wao kwahiyo vyote hivi havitakiwi?

Headed letters zenye logo ya taifa nazo hazitakiwa?
Au sijaelewa Mimi?
 
Kuna mambo yanashangaza, wakati nchi nyingine wanajivunia bendera za nchi zao, huzivaa nk hapa kwetu no. huo uzalendo tunaotaka utakujaje kama hatuipendi bendera yetu? Kama ni sheria inakataza, imechelewa sana kufutwa katika vitabu vyetu vya sheria.
Matamshi ya kitaifa yanayofanywa bila consultation yanaishia kwa kutumbuliwa mhusika. Kama alifanya consultation, mnapoteza muda kumjadili
 
Huyu jamaa kwa sasa ni kituko.toka alipoanza kupambana na juhudi za serikali dhidi ya madawa ya kulevya,kwa kuanza kum-undermine Makonnda
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…