Kumezuka tabia ya baadhi ya wananchi kuvamia viwanja na mashamba yaliyopatikana kihalali na yanayomilikiwa kisheria kwa kisingizio cha eti "yametelekezwa".
Nimeshuhudia wananchi wa mabwepande wakitetewa na viongozi wao wa serikali ya mtaa na kata wamevamia shamba la Sumaye kwa madai kuwa ni pori na amelitelekeza. Katika Mkutano ulioitishwa na mh. Makonda kwa sasa mkuu wa mkoa wananchi hao walikiri kuvamia na kujiwekea mipaka na viongozi wao mwenyekiti na diwani wakiafiki uvamizi huo licha ya kutakiwa kuonyesha nyaraka na kushindwa lakini mmiliki halali alionyesha hati ya wizara.
Wavamizi hao wamekuwa wanadai waanavamia viwanja/mashamba yaliyotelekezwa huku wakimtaja mh.Rais Magufuli aliwahaidi wananchi wakati wa kampeni kuwa atayatwaa mashamba/viwanja vilivyotelekezwa.
Ushauri Kwa bw. Makonda aache utaratibu wa kuwatambua wavamizi kwani kufanya hivyo kunawajengea kiburi kuwa tukivamia serikali itatutambua badala afanye kama alivyofanya mtangulizi wake mh.Mecky Sadiq mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro wa kuwabomolea vijumba walivyo vijenga na viwanja hivyo vikatumika kwa wahanga wa mafuriko ya jangwani mwaka 2012.
Tusilee Waharifu kwani wenye viwanja /mashamba nai wakiamua kuyalinda kwa nguvu zote mauaji yatatokea.Uvamizi In kosa kisheria , hivyo sheria zitumike badala ya siasa za bw.Makonda Za kuwatambua wavamizi.