Wenye vyeti feki kulipwa mafao yao..

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,945

Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel.

Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki.

Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao, kauli hiyo imekuja baada ya kilio kikuu kuhusu hatima ya maisha ya watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki hivyo kuondolewa kazini, hatimae serikali imekisikia na inaandaa mpango wa kuwalipa watumishi hao kwa kuwa wamehudumu katika nafasi mbalimbali serikalini kwa muda mrefu, Waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angellah Kairuki ameeleza hayo kwa kuthamini michango ya watumishi hao.

Aidha Katibu Mkuu Utumishi Dr Laurean Ndumbaro anategemea kutangaza matokeo ya rufaa ya watumishi waliokata rufaa dhidi ya vyeti feki sambamba na kutangaza majina ya watumishi wengine wa serikali kuu wenye vyeti feki ifikapo tarehe 15.5.2017 siku ya jumatatu



Chanzo: Gazeti Uhuru
 
Source P'se......
 
Hizo ni hadaa za serikali. Kama ni walipaji wangeanza kuwalipa wastaafu wa ATCL ambao wanadai PPF zao na serikali iliahidi kulioa baada ya mfuko wa PPF kuipeleka ATCL mahakamani na kushinda kesi na kupewa amri ya kukamata mali za ATCL na kuzinadi ili kuwalipa wastaafu hao. Serikali watakuja na gea ya wenye vyeti feki hewa hivyo kutolipa.
 

Huruma tunayoitaka ni kurudishwa kazini mh raisi tusamehe ni kweli tumekukosea tunapmba msamaha kwa hili
 
Huruma iliyobora ni kuwapa chance warudi darasani QT watafute vyeti halali, halafu baada ya hapo qualifications zao nyingine zitambulike kuwa ni halali!. otherwise hawa wameshakuwa condemned to a very tough psychological torture!

Kipindi cha Mkapa wale walimu wazee wa UPE walipigwa presha warudi shule kama wanataka kuendelea na ualimu au Wapigwe chini, basi wale wazee walikomaa na shule na kuna waliofanikiwa kupata qualifications, kwa hiyo na hawa wenye vyeti feki wakipewa choice ya kurudi shule au kutumbuliwa naamini watarudi shule na watapata credits tu.
 
Wakirudishwa lakini hawa nitachukia Kweli Kweli. Pia wakilipwa Mafao hawa moyo wangu utahudhunika Kweli Kweli. Pesa na mafao yao yabaki huku huku serikalini. Wameshakula haki yao. Salio litumike kuajiri watu wengine.
 
Nadhani hii ni njia nzuri sana ya ku-handle jambo hili. Kuna mtu namfahamu alikuwa miongoni mwa top brain wakati akichukua Masters yake, na isitoshe Serikali imempeleka nje mara kadhaa na hata sasa hivi yuko nje ya nchi na huko alipo ni lulu, kwa ifupi yuko serious na anaijua kazi. Unfortunately, jina lake nimeliona miongoni mwa waliogushi cheti cha form four. Definitely plan ya namna hii inaweza kuliokoa taifa kupoteza brain za namna hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…