technically
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 12,480
- 50,874
Mkuu umenikumbusha wanajeshi wa Kenya KDF walienda Somalia kupigana na all shabab........Ukitaka kujua pesa ni shetani wapewe hilo zoezi jeshi, hutakaa uamini jinsi jeshi litakavyonuka rushwa. Wangalau kwenye nchi hii taasisi iliyobaki na maadili ya kazi ni jeshi. Kuhusu unga naona hujui unazungumzia nini, wafanyabiashara hii wana hela ya kufa mtu. Na wanachofanya kila penye uzia wanapenyeza rupia, na asikudanganye mtu wanajeshi nao ni watu maskini tu wao na familia zao, kitendo cha kuona dola za kimarekani itakuwa ni sawa na siagi juu ya kikaango kwenye moto. Hao wanajeshi wabaki huko makambini wasubiri vita ama wapewe maeneo makubwa ya kilimo wazalishe kwa wingi kuepusha njaa nchini.
Jamaa Sasa hivi sio vita tena wanachoma mkaa uko na kuwauzia wasomali ndio biashara iliyoko Sasa.......
Lakini Sasa hivi wanaingiliwa na maadui mpaka kwenye kambi wanaua wanajeshi..........
Wanajeshi wakishaanza kuonja pesa za biashara au pesa haramu ni hatari sana......
Mpaka Uhuru anaogopa Sasa kuwarudisha nyumbani maana akishindwa kuwalipa kama walivyokuwa wakilipwa na un pamoja na biashara ya mkaa ni hatari hata kwa usalama wa Kenya ........
Nimependa hoja yako hawa jamaa wakishaingia huko ni hatari kwa usalama wa taifa kabisa bora tubakini na police ambao ni rahisi kuwathibiti............