Wazo la Biashara Bongo Movie

Salahan

JF-Expert Member
Sep 10, 2014
2,963
3,675
ZINGATIA:Haya ni mawazo yangu binafsi hivyo yaweza kupuuzwa au kutiliwa maanani bila shuruti yoyote.

Kwanza ningependa kuwapongeza kwa kuipigania kazi ya sanaa hususani sanaa ya maigizo.Ninyi na wadau wengine mmekuwa chachu ya mabadiliko ya taswira ya Bongomovie kimaendeleo nikimaanisha ilipo sasa niwazi inasonga na kurudisha heshima yake.Mimi kama Mtanzania na mdau wa Bongomovie nafarijika na kuona mapambano yanaendelea kuinua sanaa hii.

MIMI HASA NI NANI
Mpaka nafikia kuwasiliana nawe/nanyi kwa hakika ningependa neno langu lienee kwa wahusika wote wa sanaa hii Tanzania hasa waigizaji na waandaji.Mimi nje ya kuwa shabaki wa sanaa ya maigizo za nje na zandani mimi pia ni msambazaji mdogo wa sanaa hizi ambae sio rasmi na hasa nahusika na izo ya nje sio za ndani nikiri pia kwamba sina kibali.Lengo sio kujikamatisha wala kujitutumua bali nikutaka kufahamiana.Singatia kwamba sina na sijawahi kuuza izo bongomovie sababu yakule kufatiliwa na cosota ama wasanii wenyewe.Zingatia kwamba siuzi hardcopy (cd) bali softcopy kwa njia ya flash drive.

NATAKA NINI HASA
Kwa kuzingatia maelezo hapo juu niwazi nina jambo kuu na muhimu kwa tasnia ya filamu Tanzania. Kama nilivyoeleza hapo awali kwamba sina filamu za kibongo mpya wala za zamani sababu ni kule kukamatwa na kulipishwa mara 50000-100000 japo hii tulikuwa tunapewa kama onyo kabla ya kupelekwa mahakamani ambako ndio zile gharama za fine au jela au vyote kwa pamoja kama anavyoelezeaga yule mtumishi wa Cosota.

Sasa hizi purukushani za kuchukua Vifaa vyangu Computer ambazo ndio muda huo vinatambulika kama MTAMBO WA KURUDUFU kazi za wasanii hupelekea upotevu wa vifaa au kuharibika au vyotee kwa pamoja na kujikuta twapata hasara isiyozidi hasara mnayopata ninyi wamiliki.Suala hilo la ukamataji ndilo lililonifanya niachane filamu za kibongo na kusambaza izo nje zilizotiwa maneno ya kiswahili na madj mbalimbali Tanzania. Kwa hakika hivi sasa wingi wa uhitaji wa filamu za kibongo umeongezeka na unaoangezeka kila siku.Ninachokitaka hasa ni KUTUSAJILI NA KUTUPA KIBALI ILI KUTUTAMBUA KAMA WASAMBAZAJI WA SOFTCOPY.

KWANINI NI MUHIMU KUTUSAJILI
1.Mfumo wa CD unakwenda kuchukuliwa na Flash Drive hivyo uhitaji wa softcopy unaongezeka kila siku.Watu wanatumia flat screen zinahitaji flash kuangalia HD movie Ukiwa na flat tv huitaji deki tena.

2.Wamiliki wa libral wapo kila mtaa wenye computer watakaotumika kusambaza kazi izo softcopy hata sasa wanasambaza kimagendo.

3.Softcopy ni rahisi kusambaza na kuwafikia wengi ukilinganisha na hardcopy bila kupoteza ubora wa kazi iyo mtejaa ataangalia HD daima na itaishi muda mrefu katika uhalisia wake.

4.Softcopy yaweza pia kusambazwa kwa njia ya internet na kumfikia mteja/msambazaji kona zote Tanzania hata awe mipakani vijijini atahitajika awe na internet tu hudumaa itamfikia.

5.Gharama za production na usambazaji wa CD zipo juu ukilinganisha na Softcopy ambayo itahitajika Mb kusambaza kwa njia ya Internet kumfikia Msambazaji wa libraries.

6.Twende na technolojia movie za watu wanatizama hadi kwenye simu smartphone siongelei streaming huko hakuna kheri kwa uchumi wa wabongo wengi hatuwezi.Yan mtu alipie subscription kisha alipie mb za streaming movie nzima hadi iishe kwa bando zetu kwakweli huko mtafeli na hamtafikia lengo.Hapa namaanisha nje ya mteja kuwekewa kwenye flash drive wengine huja na smartphone kuwekea humo movie.

HILI LINAWEZEKANAJE
Nimejaribu kuulizia library zinazopatikana izo bongo movie ki ukweli wanauza ila hawako huru na wapo tayari kuununua uhuru.Ukweli ulio mbaya ni kwamba tunakamatwa kwa kusambaza kazi kimagendo nasi tunalalamika kutokupewa vibali vya uwakala wa kusambaza izo softcopy.

Yapo yakuzingatia ili maneno yangu yalete ukombozi......
i)Lazima kila mmiliki wa library atakayekubali kusambaza kazi zenu bongomovie awe na kibali cha uwakala atakacholipia hima kwa mwezi mmoja au miwili au mitatuu na risiti ya movie husika anayouza.

ii)Lazima kila mmiliki wa library asiyekubali kulipia basi ahakikishe hasambazi softcopy yoyote na huyu hasa ndio wakubanwa.
iii)Kutokana na wingi wetu libraries na umuhimu wetu huku mtaani izo gharama za subscription za uwakala ziwe rafiki naamini Tanzania nzima tunazidi 5000 (Tanzania inajumla ya mitaa 4263 kwa mujibu wa tamisemi)prove me wrong na naamini kila mtaa uko na library 1 au zaidi.

iv)Kuna uwezekano wa kuendelea na uuzaji wa hardcopy kama kawaida mana sio wote wenye flash na smartphone sisi wasambazaji wa softcopy tukawepo kama tageti kuu.

V)Kuwepo na wasimamizi wa mawakala wa softcopy kwa ngazi za milaya na kata ili uwajibishwaji na usimamizi uwe wa kueleweka.Ufuatiliaji ndio kila kitu bila ufuatiliaji hakika nayasikitia mawazo yangu na yule atakayeyafanyia kazi.

Vi)Kuwepo na kibali hususani cheti na kibandiko cha WAKALA ALIYETHIBITISHWA.
Vii)Makusanyo yatakayopatikana basi yaboreshe tasnia hii mwisho wa siku mapata ambayo naamini ni zaidi ya mil 100 kwa hesabu ya mkitoza 20000 kila mwezi kila mmili wa library hivyo kila mwezi mtakusanya 20000Tshx5000=100,000,000/=Tsh Kama makadirio ya juu kwa makadirio ya kati 20000Tshx2500=50,000,000/=Tsh.Makadirio ya chini kabisa ni 20000x1250=25,000,000/=.

Kwa hesabu hiyo hasa ya juu na yakati ikitumika kuwekeza kwenye uzalishaji basi naamini zitatoka filamu bora nikiamini bajeti ndio huamua ubora wa filamu.

Viii)Serikali na mamlaka zake husika,kampuni za uzalishaji filamu,usambazaji,wasanii,mawakala na wadau wengine wa bongomovie wote tunahusika katika kulinda na kusimamia zoezi hili ili Bongo movie ifike kimataifa.

ZINGATIO
Inapendeza wamiliki wa filamu izo muwe na umoja utakaosimamia usambazaji ili isiwe sio tunapokea toka kwa kila msanii au mzalishaji bali mzifikishe kwa msambazaji mkuu atakayetusambazia mawakala wake mtaani hata kwa njia internet itatufikia tu.

Hatuwezi kununua kwa kila msanii bali kwa msambazaji fulani.Huenda mnalipwa pesa kidogo na wasambazaji wa sasa pengine sababu ya unyonyaji au usambazaji wake mbovu au hajawahi kuwaza fursa hii adhimu basi limfikie hili neno au yeyote anaweza kuwekeza kwenye hili wazo ninalolitoa bure sababu tu sina mtaji wakuwekeza kulifanikisha hili.

Msambazaji utakayekuwa tayari kututambua sisi kama mawakala wa softcopy basi atuhakikishie kutupatia kila toleo jipya la Movie litokapo punde tu baada ya kuingia sokoni.

MOVIE HUTOFAUTIANA UBORA,MVUTO NA UHITAJI WAKE MTAANI HAPA ITAKUWAJE.
Hii ndio sehemu ngumu ili mtu apate anachostahiki.Kuna movie zinatumia gharama kubwa katika uandaaji naa zingine gharama ndogo nasi twazitaka zote sasa itakuwaje kwenye usawa na haki kulingana mauzo.Nimewaza hiviiiii.

Msambazaji aandae platform ya mtandaoni hasa App ambayo wasambazaji watanunu filamu na kuruhusiwa kudownload softcopy ya movie aitakayo.Hapa nashauri gharama za uwakala ziwe chini walau iyo 20000 kwa mwezi au ili pia aweze kununua mtandaoni.Hii platform watanunua humo mawakala na watu binafsi hivyo mtaweza kujua movie gani imeuza zaidi kwa kuwa na download nyingi zaidi.

Kila wakala lazima awe na movie aliyonunua (bei iwe rafiki walau 1000 part 1&2 sawa na bei ya jumla).Kila mtu anaponunua basi kuwe na code inayotumika kama risiti ya copy husika.

Mkaguzi/msimamizi lazima amkague wakala uanachama wake wa muda husika na risiti ya movie husika (sio lazima awe nayo risiti bali anaweza kuonyesha kumbukumbu za manunuzi kwenye profile yake kwenye platform ya manunuzi.

HITIMISHO
Hakuna mtu anapenda kula kupitia mgongo/jasho la mwingine,hakuna mtu anataka kuhukumiwa kwa kosa la wizi.Ni aibu na sio busara kumnyonya binadam mwenzio.Ni muhimu kuthamini kipaji cha mtu na kazi ya mtu ili mwisho wa siku kila mtu ainuke kiuchumi kila mtu anufaike na fursa hii ya ajira iliyo ndani ya sanaa ya maigizo.Ifike mahali bongomovie ifike tuzo za Oscar.

Nimalizie kusema kwamba ruhusuni soko la softcopy liwe soko chaguo la kwanza hivyo hata usimamizi wake na uwekezaji utakuwa wa juu pia.

MWISHO
By Salim Mhina
0713055107
Morogoro Town

Screenshot_20201108-112548.png
 
Umeandika upuuzi mtupu na ndo maana hata ulio watumia hyo Email hawakukujibu mpaka muda.
Eti ada 20000 ya uwakala kisa Bongo Movie tu?
Ha ha haaaaaaaa
 
Nafikiri una mawazo mazuri, hata mimi nishawahi kuwaza kitu kama hichi muda mrefu sana, kama wadau watakusikia na kukaa chini kuboresha na kuunda kitu kizuri zaidi naamini hili litawezekana penye wengi hapaharibiki neno!.
 
Umeandika upuuzi mtupu na ndo maana hata ulio watumia hyo Email hawakukujibu mpaka muda.
Eti ada 20000 ya uwakala kisa Bongo Movie tu?
Ha ha haaaaaaaa
Acha matusi toa hoja Yaani umeona hicho tu kwenye maelezo yote aliyo andika.

Pili, hayo ni mawazo yake Toa yako yenye tija.
 
Ni mawazo na mchango mzuri sana.

Upembananua vizuri.

Nashauri nenda kwa wenyeviti wa wasanii hawa wa maigizo useme wazo lako, kuna watu watalichambua na kuliandikia mswada vizur zaid na kulipigania liwe halali.

Serikali inatafuta njia ya kuingiza mapato, na pia wasanii watanufaika, wauzaji kama ww watanufaika. Na wapenz wa Bongo Movie watafurahia.

Naomba kusema , Wakati huu ni wa technologia, na jinsi inavyokuwa na Watu tukashindwa kwenda nayo basi hatutafanikiwa.

Nina iman kuna wakina Kanumba wengi hatuwajui kwasababu kazi hazifiki kwa watazamaji.

Ni wazo zuri sana . Big up.
Tunaweza kuliandikia Business proposal kabisa na likafanyiwa kazi
 
Umeandika upuuzi mtupu na ndo maana hata ulio watumia hyo Email hawakukujibu mpaka muda.
Eti ada 20000 ya uwakala kisa Bongo Movie tu?
Ha ha haaaaaaaa
Naam... Tafadhali tusaidie mawazo yako yenye tija...Huenda umeona tatizo ni bei tajwa basi Pendekeza bei unayoona itakuwa rafiki kwa wadau wote wa tasnia hii (msanii,msambazaji,mtazamaji na serikali kiujumla).Tafadhali kosoa huku ukitoa wazo sahihi.
 
Mimi nitakuwa competitor wako nitatengeneza mfumo wa ku stream Bongo movies kupitia simu janja na SmartTV
 
Samahani sijasoma issue yote kwahio huenda nikawa nje ya mada..., ila kabla ya kuwaza biashara / usambazaji / kuingiza pesa / na kupata faida ni vema kuzingatia soko / uhitaji na hilo litaendana tu iwapo kazi zitakuwa nzuri na watu kuzihitaji kuzipenda na kuzitafuta unless otherwise unaweza ukataka kuuzia watu kitu ambacho hata bure hawakitaki....,
 
Samahani sijasoma issue yote kwahio huenda nikawa nje ya mada..., ila kabla ya kuwaza biashara / usambazaji / kuingiza pesa / na kupata faida ni vema kuzingatia soko / uhitaji na hilo litaendana tu iwapo kazi zitakuwa nzuri na watu kuzihitaji kuzipenda na kuzitafuta unless otherwise unaweza ukataka kuuzia watu kitu ambacho hata bure hawakitaki....,
Point
 
Samahani sijasoma issue yote kwahio huenda nikawa nje ya mada..., ila kabla ya kuwaza biashara / usambazaji / kuingiza pesa / na kupata faida ni vema kuzingatia soko / uhitaji na hilo litaendana tu iwapo kazi zitakuwa nzuri na watu kuzihitaji kuzipenda na kuzitafuta unless otherwise unaweza ukataka kuuzia watu kitu ambacho hata bure hawakitaki....,
Movie zinauza mtaani watu kibao wanaulizia
 
Mimi nitakuwa competitor wako nitatengeneza mfumo wa ku stream Bongo movies kupitia simu janja na SmartTV
yap ni moja ya maboresho na sasa tayari zipo app playstore zinaruhusu streaming na kusave offline.But wadau wa flash wapo pia kibao
 
Back
Top Bottom