Waziri wa Afya: Wafamasia Msiwauzie wananchi Dawa bila Cheti cha Daktari

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,330
4,692
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa Wafamasia wanaotoa dawa kwa Wagonjwa wasiokuwa na vyeti vyenye maelekezo ya Madaktari ambao walipaswa kuwa na vyeti hivyo, kuacha kufanya hivyo ili kuepusha kutengeneza usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Waziri Ummy ametoa maekezo hayo Dodoma leo kwenye Kongamano la 14 la Chama cha Wanafunzi Wafamasia (TAPSA) na kilele cha Wiki ya Famasia Kitaifa.

Ummy amesema kuna wakati waliwahi kuweka mtego na wakabaini uwepo wa Wafamasia wanaouza dawa bila utaratibu “Tunatengeneza jambo ambalo mnalijua la usugu wa dawa kile kipindi cha mlipuko Watu walikula sana AZUMA Mtu anapewa bila maelekezo, nitoe onyo kwa Wafamasia kutowauzia Wananchi dawa ambayo haina cheti cha Daktari.”

Katika hatua nyingine Ummy amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Tsh. Bilioni 184 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya dawa.

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ametoa onyo kwa Wafamasia wanaotoa dawa kwa Wagonjwa wasiokuwa na vyeti vyenye maelekezo ya Madaktari ambao walipaswa kuwa na vyeti hivyo, kuacha kufanya hivyo ili kuepusha kutengeneza usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa.

Waziri Ummy ametoa maekezo hayo Dodoma leo kwenye Kongamano la 14 la Chama cha Wanafunzi Wafamasia (TAPSA) na kilele cha Wiki ya Famasia Kitaifa.

Ummy amesema kuna wakati waliwahi kuweka mtego na wakabaini uwepo wa Wafamasia wanaouza dawa bila utaratibu “Tunatengeneza jambo ambalo mnalijua la usugu wa dawa kile kipindi cha mlipuko Watu walikula sana AZUMA Mtu anapewa bila maelekezo, nitoe onyo kwa Wafamasia kutowauzia Wananchi dawa ambayo haina cheti cha Daktari”

Katika hatua nyingine Ummy amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 Tsh. Bilioni 184 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya dawa.

Tobaa
 
Back
Top Bottom