Escrowseal1
JF-Expert Member
- Dec 17, 2014
- 4,537
- 4,499
Wakati wa kipndi cha Rais Magufuli na mheshimiwa Lukuvi walijitokeza madalali wa kampuni ya PMM wakaanza uthamini wa nyumba za watu zaidi ya 4000 na wakazi 70,000 katika eneo la Vingunguti. Kwa kuwa uthamini huo ulikuwa wa kitapeli usiokuwa na manufaa kwa umma Serikali ya awamu ya tano iliingilia kati na kusitisha madalali hao na zoezi liliishia hapo mwaka 2017.
Hivi karibuni zoezi hilo liliianza upya kwa madai kuwa kuna mwekezaji analitaka eneo hilo na zoezi la kuwathamini wakazi likafanyika kwa madai ya kuwaondoa wakazi hao. Hatuna uhakika ni kwa manufaa ya nani na kama uthamini unayo manufaa ya umma ama ni mwendelezo wa yale ya PMM.
Vingunguti ni eneo ambalo Serikali ilishatoa leseni za makazi halali kwa wakazi wake. Familia zimekaa miongo kadhaa, wananchi wanaokaa eneo hili proud yao ni sawa sawa na yeyote mwenye mansion yake Masaki au Mbezi beach. Kwanini hawa wawekezaji wasiwanunue walioko Masaki ama Mbezi beach sawa sawa na hawa wanyonge wa Vingunguti. Hii serikali ni muhimu kusimama na jamii ya watu wake.
Kumuondoa mzee kwa vi milioni kadhaa kwamba aanze upya kutafuta eneo la kusettle ni ukatili usio na kifani. Maeneo haya ni very prime na yako kati kati ya jiji sina uhakika u prime wake unazingatiwa katika uthaminishaji ama la baada ya miaka kadhaa wananchi hawa wataendelea kutopea kwenye umasikini huku hawana share kwa mabilionea watakaojibanza kwenye hizi prime areas za masikini.
Naomba mhakikishe dukuduku hii inamfikia mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam maana ofisi yake inahusika pamoja na waziri wa ardhi mh Slaa watoke wazi kama alivyotoka Lukuvi watoe msimamo wa haya yanayofanywa ni kwa manufaa ya nani.
Ni kwa nini Serikali ya awamu ya tano ilisitisha zoezi hili na wananchi wakamshangilia na sasa uthamini unafanywa kimya kimya bila kuwahusisha wakazi wake.
View: https://youtu.be/f2_59KIcUog?si=cGvzDUOoxEiT5N5c