Anachofanya yaani uwazi katika mapato na matumizi ndio muhimili wa "good governance". Suala hili lingetekelezwa katika ngazi zote uongozi wa taasisi zetu.Ni kweli hata mie namkubali sana hapo kwenye ukusanyaji wa kodi na kuwa muwazi katika matumizi.
Kipande tu cha ushauri ninachoweza kumpa ni kuwa abuni namna nyingine sasa ya kuongeza pato la taifa, isiwe kwenye makusanyo tu ya kodi, viwepo vyanzo vya mapato vingine kama utalii, viwanda na mabomba ya mafuta nk.
Lakini pia aangalie uwezekano wa kuisimamia benki kuu iingize noti mpya hasa za 500 kwenye mzunguko na kuziondoa hizi zilizopo, zimechakaa sana na zinaleta usumbufu sana kwenye manunuzi kwa wananchi wengi.
Jingine inaonekana more than 40% ya mapato yake yanatumika kwenye kulipa mishahara, inatakiwa ahakikishe pesa nyingi inaelekezwa katika kuzalisha na sio kulipa mishahara, hatuwezi kuwa taifa la kuspend tu bila kuzalisha
Wewe unawashwa na Lowassa,unajuaje halipi kodi stahiki?
Weka data ya kodi anayolipa unayoijua wewe,tujue haubweki upuuzi mtupu
Umeandika Uzi wako vizuri ila ukaupaka matope kwa kumtaja lowassa
Good analysis, ila ulipomtaja Lowasa rais wa rohoni...lazima wafuasi wakupinge tuuuu
umeanza vizuri ila aipendezi kumtaja lowassa hapa au ungeweka ushahidi wa yeye kutolipa kodi
mpaka umtaje lowasa
Pia kuna Nyumba za kulala wengine, ni muda muafaka sasa mtu ukilipia chumba upewe risiti ya EFD, sio kama sasa hivi ni uhuni mtupu unaofanyika.
Nchi kuna vyanzo vingi tu vya mapato lakini viongozi wetu hawafuatilii.
Barbarosa,
..unamaanisha nyumba alizoiba magufuli na wenzake hazitozwi kodi ya pango?
..sasa hebu fikiria nyumba hizo zingebaki mikononi mwa serikali tungekuwa tunaingiza kiasi gani.
..kwa kweli wizi wa nyumba za serikali uliousimamiwa kwa umahiri mkubwa na Pombe Magufuli ni jipu kubwa na tunapaswa kumsaidia Raisi ajitumbue.
cc Quarterpin
Ninamshangaa sana JPM anapotokwa na povu eti 'anatumbua majipu' wakati na yeye ni jipu kongwe. Na wakati huo huo haishi kujiapiza eti 'msema kweli ni mpenzi wa Mungu' - mbona yeye hasemi ukweli kuhusu huo wizi wa nyumba za umma!! Kama kweli kuna jahanamu huko kwa Muumba, ninafikiri wanasiasa wote wataelekezwa mtaa wa jahanamu!Kweli hebu Magufuli arudishe zile nyumba zote alizouza, tunajua alifanya kwa influence ya wakubwa, hebu saiv kwa yy ndo mkuu, arudishe. Tunajua wakati akiwa waziri alitetea sana, lakin utetez mwing uliegemea kwenye uchkavu wa nyumba bila kuangali prime areas ambako nyumba zipo.