Waziri Mkuu Majaliwa: Viroba marufuku kuzalishwa wala kutumiwa kuanzia Machi 01, 2017

Sometimes common sense is not common, hii ni kwa faida ya vijana wetu, yaani utakuta vijana wamekaa tu kwenye viduka wananyonya viroba, nchii hii inaenda wapi jamani nguvu kazi ya taifa inapotea,kwanza pombe inawekwa kwa namna ambayo inaondoa hadhi ya pombe yenyewe na mmwaji wake, nakupongeza sana waziri mkuu kwa hilo, ila inabidi iwekwe rasmi kabisa, kiutaratibu yaani kisheria.
Subiri wahamie kwenye gongo kama zamani ndio utajua hadhi ya pombe za kwenye chupa...
 
Sometimes common sense is not common, hii ni kwa faida ya vijana wetu, yaani utakuta vijana wamekaa tu kwenye viduka wananyonya viroba, nchii hii inaenda wapi jamani nguvu kazi ya taifa inapotea,kwanza pombe inawekwa kwa namna ambayo inaondoa hadhi ya pombe yenyewe na mmwaji wake, nakupongeza sana waziri mkuu kwa hilo, ila inabidi iwekwe rasmi kabisa, kiutaratibu yaani kisheria.
Ya Leo Gusa unaswe
 
Kwa nchi inatogemea kuendeshwa kwa kutegeme 20% ya budget kutoka kwenye viwanda na makampuni ya vileo.....ndo yale yale ya kuisoma namba....sisiem ni ilele....
 
Amesema wameshakaa na wenye viwanda vya kutengeneza pombe hizo na kuwaambia viroba kuwa kuanzia tarehe 1/3/2017 ni marafuku kutengeneza viroba.

Amewataka watengeneze pombe zenye ukubwa unaokubalika kwani viroba vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi.

Amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la kupiga vita dawa za kulevya

Itasaidia sana kuokoa nguvu Kazi. Uamuzi mzuri nauunga mkono....
 
Utafiti wangu bubu unaonesha bei ya kiroba na gongo vinawiana, na sioni kinywaji kingine cha kuziba pengo la kiroba zaidi ya gongo... Hakuna na hakutakuwepo.

Tujiandae na biashara haramu ya viroba kutoka nje ya nchi (Zambia, Malawi nk) na gongo kurudi katika utukufu wake wa miaka iliyopita.

[HASHTAG]#YaLeoKali[/HASHTAG]
Mkuu uko sahihi Zambia na Malawi zinapombe nyingi sana za karatasi tena kali kuliko hata kiroba.....Naona ni muda muafaka wafanyabiasha wa magendo mipakani kutajirika.
 
Amesema wameshakaa na wenye viwanda vya kutengeneza pombe hizo na kuwaambia viroba kuwa kuanzia tarehe 1/3/2017 ni marafuku kutengeneza viroba.

Amewataka watengeneze pombe zenye ukubwa unaokubalika kwani viroba vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi.

Amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la kupiga vita dawa za kulevya

Serikali iliruhusu hii kitu kwa utaratibu uliokubalika na mamlaka ya mapato imekuwa ikikusanya kodi kupitia hivyo viroba na vina trade mark...kwahiyo suala la kuvizuia si la maagizo ya majukwaani...Pm apunguze kukurupuka
 
Kwa hili la leo naomba nimuunge mkono waziri mkuu, nadhani hajapiga marufuku pombe yenyewe ya viroba ila tu ifungashwe katika vifungashio vinavyo kubalika na katika ujazo ambao ni reasonable utakaofanya viwe na bei ya juu kidogo. Hii itasaidia watu wengi ikiwemo wanafunzi kutomudu bei kirahisi na hivyo kuchangia kuokoa nguvu kazi ya taifa. Viroba ni portable sana, ni rahisi mtoto wa shule au mtu yeyote kununua na kuficha mfukoni kwa matumizi yake muda wowote tofauti ikiwa pombe hiyo itafungashwa kwenye chupa.
 
Amesema wameshakaa na wenye viwanda vya kutengeneza pombe hizo na kuwaambia viroba kuwa kuanzia tarehe 1/3/2017 ni marafuku kutengeneza viroba.

Amewataka watengeneze pombe zenye ukubwa unaokubalika kwani viroba vimekuwa vikitumiwa na wanafunzi.

Amesema zoezi hilo litaenda sambamba na zoezi la kupiga vita dawa za kulevya

Waelimishe watumiaji sio kudhibiti wazalishaji kuna ajira nyingi zitapotea. Siasa zisiingilie uchumi
 
Back
Top Bottom