Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa,akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya msiba wa mama wa Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, alipofika kutoa pole kwa wafiwa.Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini,Dk. Medard Kalemani na anayefuatia ni Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni ,ambao waliongozana na Waziri Mkuu kwenda kutoa pole kwa wafiwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka,ambaye amefiwa na mama yake.Waziri Mkuu yuko mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi.
Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni(kulia),akimpa pole Mbunge wa Muleba Kusini,Profesa Anna Tibaijuka, aliyefiwa na mama yake,marehemu Aurelia Kajumulo.