Waziri MAHIGA kuzungumza na Rais wa MALAWI kuhusu watanzania 8 wanaoshikiliwa huko

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,485
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr AGOUSTINE MAHIGA ameingilia kati sakata la Watanzania wanane waliowekwa kizuizini Nchini MALAWI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dr AGOUSTINE MAHIGA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr AGOUSTINE MAHIGA ameingilia kati sakata la Watanzania Wanane waliowekwa kizuizini Nchini MALAWI, kwamba anakusudia kuonana na Rais wa Serikali ya Malawi Profesa PETER MUTHARIKA.

Dr MAHIGA ametoa kauli hiyo Mjini Lilongwe baada ya kuhitimisha Mkutano wa siku Nne wa Ushirikiano baina ya MALAWI na TANZANIA na kuthibitisha kuwa Raia hao Wanane wenyeji wa wilaya ya Songea Mkoani Ruvuma wako salama, jitihada za kuwatoa zinaendelea.

Aidha waziri Mahiga anasema Idadi kubwa ya watanzania wako vizuizini katika nchi mbalimbali duniani, sababu kubwa ni kukutwa na biashara za dawa za kulevya.

Watanzania hao wanashikiliwa Nchini Malawi wakiwa katika Gereza la Mzuzu, ujumbe wa Tanzania uliohudhuria Mkutano wa Ushirikiano wa Tanzania na Malawi, umewatembelea watanzania hao.

Naibu Katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi RAMADHANI MWINYI, amesema watanzania wako salama wakiwa gerezani Mzuzu.
 
Hivi na sisi tukianza haya wanayoyafanya hawa majirani zetu kweli watapona????Au Malawi wanahitaji political sympathy????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…