Waziri Lukuvi, Waziri Makamba na wengineo hawatabaki; watakwenda na maji

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Ima kwa kuondolewa na Rais,maamuzi yao au hata Bunge. Hawatabaki. Ni siku itakapotamkwa Mahakamani,Mahakama Kuu ya Tanzania Kitengo cha Ardhi,kuwa bomoabomoa haikuwa halali. Zuio la leo ni mwanzo tu.

Zuio la leo haliiachi salama Serikali ya Rais Magufuli. Mchoro wa ubabe na kukurupuka kwa wahusika umeanza kuchorwa. Kesi ya msingi ya Mbunge Mtulia wa Kinondoni itaunguruma. Itatolewa uamuzi. Ili Mawaziri na wahusika wengine wabaki salama,Mahakama ibariki bomoabomoa na kuitupilia mbali kesi ya Mtulia.

Zuio la leo si la kubeza. Ni mwanzo wa mweleka wa kueleweka kwa Serikali ya Rais Magufuli inayoratibu bomoabomoa. Mchezo umeanza!

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
Kwanza hebu Twambie zuio hili lina wahusu wakina nani? na ni wa wapi? Mahakama imesitisha ubomoaji kwa wakazi wa bonde la mto msimbazi ambao ni wakazi 650 na ni wale walio jiandikisha kuwa wamefungua case dhidi ya serikali!

Kama umesikia hukumu ya leo judge amesema kuwa zoezi hili lina maana na ni muhimu kwa serikali na amesitisha zoezi kwa wakazi wa bonde la mtu msimbazi(walio fungua case) na kwa wengine litaendelea kama kawaida.


Kwa taarifa tuu ni kwamba kamwe hakuna waziri atakayefukuzwa kwa kutekeleza zoezi ambalo wameagizwa na serikali na kamwe kwenye case hii wananchi hawatoshinda!
 
Last edited:

..watakwenda na maji kivipi?

..kwani huko mahakamani hakuna MAJAJI WAKEREKETWA WA CCM?

..CCM ndiyo wameshinda uchaguzi, hivyo SERIKALI, BUNGE, MAHAKAMA, JESHI, vyote ni vya CCM.
 
Sheria ni lazima ifuate mkondo wake!!
#SHERIA TUNAZO TABU IPO WAPI?
SHERIA HIZI TULIJITUNGIA WENYEYE ILI KULINDA MAZINGIRA YETU.
SEREKALI ITABAKI KUSIMAMIA SHERIA ZILIZOPO NA HAITAOGOPA VITISHO!
TAFADHALI MAHAKAMA ZETU ZIZINGATIE SHERIA ZILIZOPO!
RAIS AU WAZIRI SI MTUNZI WA SHERIA ZILIZOPO #BALI NI WATENDAJI NA WATEKELEZAJI TU.
---->>IKUMBUKWE HII SIO SEREKALI DHAIFU, NI SEREKALI INAYOFUATA SHERIA ZILIZOPO!!!.
**TUSIPOYAREKEBISHA SASA NI NANI ATAKUJA LAUMIWA?**
**WAZOMBWAPO NA MAJI PIA HUANZA KULIA LIA HOVYO NA KUOMBA MISAADA!
ii
 
Last edited:
Baadaye watu watasema wanaobomoa nyumba za wananchi wanachochea chuki baina ya serikali na. Wananchi!
 
Daaa kwa namna hii kweli taifa linahitaji ELIMU
Eti mahakama imetoa haki kwa RAIA halafu nyumbu mmoja Wa kijani anasikitika! Subiri yampate yeye ndio atajua maana ya utawala wa sheria.
 
Maamuzi ya mahakama hayawezi kwenda kinyume na agizo la serikali waliokwenda mahakamani kupinga zoezi la ubomoaji wa hizo nyumba wajiandae kisakolojia kwa maamuzi yatayotolewa na mahakama.@Pasco kila kinachofanyika kwenye serikali ya JPM kimejaa usanii
 
Ni bora ninyamaze ili nisiitwe mchochezi ila hii nchi ilipofikia ilikuwa ni lazima ubabe utumike ili watu wakae kwenye mstari
ubabe wa kubomoa makazi ya watu? hujawahi kujenga kenge wewe. linene kakichwa kadogo.
 
ningekuwa ndo mkazi wa maeneo hayo ningetumia muda huu kutafuta namna nyingine huku nikiibomoa nyumba yangu taratibu kuliko kutegemea wanasiasa uchwara
 
Mi nimeshangaa kuona wakazi wa mabondeni wanashangilia kwa usitishwaji wa zoezi. Nikafikiri baada ya kujipanga kuondoka wao wanaona kama wameshinda kesi tayari. Subiri hukumi itoke watajuta kwanini hawakuhama mapema..sasa hivi.wanapata temporary relief tu.
 
Taifa linawatu wajinga sana kwahiyo unataka kutuambia wale watu waliojenga mabondeni na maeneo ya wazi wapo kihalali?
 
Kuna watu wanatoa maoni mbuzi humu hadi kero. . Hiyo nafasi ni bonge la tusi lipo hapo. CCM wana laana.
 
ubabe wa kubomoa makazi ya watu? hujawahi kujenga kenge wewe. linene kakichwa kadogo.


NapigaNgumi Mwenye kakichwa kadogo hapa ni nani mie au wewe uliyejenga eneo ambalo si stahili kujenga?

Mwenye kakichwa kadogo hapa ni nani mie au wewe ambaye hujui kuwa kuna maeneo ambayo hayastahili kujenga na kujenga ni makosa

Naweza kuwa Kenge lakini mie ni Kenge mjanja ambaye najua kuna residential area, industrial area, open space etc ..

wewe ambaye hujui hiyo nakuita KENGE MJINGA na kama unajua ila unafanya makusudi basi wewe ni KENGE MPUMBAVU
 
Last edited:
CCM wamelaaniwa..

Wananchi wamegeuzwa wanyama..Wanakua wakimbizi ndani ya Taifa lao, kibaya zaidi ni wakimbizii wasio na hifadhii
 
Kuna njomba moja humu inamalizia kwa kusema wana nchi watashindwa kwani kwani serekali ni nani au ni ya nani? Mimi nasema watashindwa sio kwa sababu hawana hoja ,ila kwa sababu mbunge aliefungua mashtaka anatoka cuf .hili ndio tatizo fitna ipo hapo tu
 
ambalo wameagizwa na seriksli?kwa hiyo wao sio serikali!!!
 
UKAWA hemu tuambieni, hili zoezi lifanyike vipi ili muone lipo kihalali?

Naona mnatetea wavunja sheria tu hapa...tunaomba mtoe mbadala...Je serikali iache raia waendelee kuishi mabondeni, kwenye maeneo ya wazi, maeneo ya mikoko (ufukweni) na wengine kwenye viwanja vya wat? Au nini kifanyike?
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…