Waziri Dkt. Ndumbaro: Uwanja wa CCM Majimaji Kufanyiwa Ukarabati

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,588
1,190

WAZIRI DKT. NDUMBARO: UWANJA WA CCM MAJIMAJI KUFANYIWA UKARABATI

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine mbili za kukatia nyasi katika uwanja wa mpira wa miguu wa CCM Majimaji kwa uongozi wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine hizo Desemba 21, 2023 mjini Songea ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali kufanya maboresho katika viwanja mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kukarabatiwa kwa uwanja huo kutawezesha vilabu mbalimbali nchini kuutumia uwanja huo kwa mechi za ligi kuu jambo ambalo litaongeza hamasa ya soka mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuboresha sekta ya michezo nchini hususani mkoa wa Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.

Makabidhiano ya mashine hizo zenye thamani ya Shilingi Milioni saba yameshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Bw. William Kapenjama na viongozi wengine wa chama na serikali ambapo pia Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemleta mtaalam atakayetoa mafunzo kwa wasimamizi wa uwanja kuhusu matumizi ya mashine hizo uwanjani hapo.
 
Attachments

  • GB7lvyxXQAAZ5f8.jpg
    GB7lvyxXQAAZ5f8.jpg
    254.7 KB · Views: 4
  • GB7lwnlWAAAYEg7.jpg
    GB7lwnlWAAAYEg7.jpg
    245.7 KB · Views: 3
  • GB7lxbyW0AA8iZ_.jpg
    GB7lxbyW0AA8iZ_.jpg
    241.1 KB · Views: 3
  • GB7lzEVXgAAgTdu.jpg
    GB7lzEVXgAAgTdu.jpg
    229.6 KB · Views: 4

WAZIRI DKT. NDUMBARO: UWANJA WA CCM MAJIMAJI KUFANYIWA UKARABATI

Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine mbili za kukatia nyasi katika uwanja wa mpira wa miguu wa CCM Majimaji kwa uongozi wa chama hicho Mkoa wa Ruvuma.

Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekabidhi mashine hizo Desemba 21, 2023 mjini Songea ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali kufanya maboresho katika viwanja mbalimbali nchini.

Amesema kuwa kukarabatiwa kwa uwanja huo kutawezesha vilabu mbalimbali nchini kuutumia uwanja huo kwa mechi za ligi kuu jambo ambalo litaongeza hamasa ya soka mkoani humo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndg. Odo Mwisho ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa jitihada mbalimbali inazofanya kuboresha sekta ya michezo nchini hususani mkoa wa Ruvuma ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025.

Makabidhiano ya mashine hizo zenye thamani ya Shilingi Milioni saba yameshuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini Bw. William Kapenjama na viongozi wengine wa chama na serikali ambapo pia Mbunge wa Jimbo hilo na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amemleta mtaalam atakayetoa mafunzo kwa wasimamizi wa uwanja kuhusu matumizi ya mashine hizo uwanjani hapo.
Hii haikubaliki, hivi sasa imekuwa kawaida kuchota pesa ya serikali kwa ajili ya kukarabati viwanja vya CCM.
 
Back
Top Bottom