Wazazi/Walezi andikeni WOSIA muwaache wategemezi wenu salama

Amicus Curiae

JF-Expert Member
Sep 12, 2012
5,351
7,633
Igweeeeee.....

Kuna hii kasumba huku mtaani kwamba kuandika WOSIA ni kujichulia. Hii siyo kweli hata kidogo. Sote tutakufa (death is certain). Ipo siku kila mmoja wetu ataiacha dunia hii. Swali ni je, utakapokufa, wategemezi wako utawaacha salama kiasi gani?

Kisheria tuna usemi mmoja kwamba ukifa bila kuandika/kuacha wosia unakuwa umekufa bila kuwajibika sawasawa hapa duniani.

Wosia ni tamko (la mdomo au la maandishi) linalobainisha ni kwa namna gani marehemu anataka mali zake zigawanywe atakapoiacha dunia hii.

Wazazi/walezi jiwekeeni utamaduni wa kuandika/kutamka WOSIA.

Aidha, WOSIA hauhusiani na mali tu, bali unaweza hata kuandika WOSIA ukibainisha ni nani unataka atoe uamuzi wa mwisho ikitokea umeumwa sana ukawa hujitambui, wosia wa namna hii unamteua mtu unayemuamini ambaye atafanya maamuzi hospitalini ukitakiwa ufanyiwe labda upasuaji n.k, huyu atafanya maamuzi kwa niaba yako.

Watu tunaodhani ni ndugu zetu wamegubikwa na tamaa mbaya sana siku hizi, ukiwa hai anaonekana mwema ila ukifariki anageuka mbogo!

Mwisho wa siku ukifa tu, wategemezi (watoto) na mke/mume wako wanaishia kuteseka tu.

Ukiandika wosia unamteua mtu mmoja ambaye atakagawa mali zako kwa wategemezi wako akisimamiwa na Mahakama hivyo mali zako zitakuwa salama.

Wosia unawezwa kuhifadhiwa Mahakamani, benki, RITA, kwenye ofisi ya Mwanasheria (Wakili) n.k.

Mwenye masikio na asikie.
 
Ungeongeza Kwa kusema Wazazi wenye Mali. Sasa Mimi godoro, sufuria mbili na bakuli naandika wosia kweli! Si kuchezea karatasi tu.
 
Ungeongeza Kwa kusema Wazazi wenye Mali. Sasa Mimi godoro, sufuria mbili na bakuli naandika wosia kweli! Si kuchezea karatasi tu.
Mkuu, usiseme hivyo. Usidharau hivyo vitu vidogovidogo vya ndani. Vinaweza pia kuwa msaada kwa kijana/vijana wako.
 
Hata wangeandika na wino wa damu....bado wachaga watang'ang'ania mirathi.
Kukishakuwepo na WOSIA hata akiwepo mchaga anayetokea kwenye ukoo wa kichifu ni lazima auheshimu wosia kwasababu mgawanyo wa mali unaratibiwa na Mahakama.

Isipokuwa kama wosia utakuwa wa magumashi. Na ni lazima ithibitike Mahakamani kwamba wosia huo si halali.
 
Mkuu, usiseme hivyo. Usidharau hivyo vitu vidogovidogo vya ndani. Vinaweza pia kuwa msaada kwa kijana/vijana wako.
Watagawana tu bila hata msimamizi wa mirathi. Hapo anakuja mwenyekiti wa mtaa anaongoza ugawanaji maisha Safi. Changamoto uwe na ng'ombe, Mali za kudumu, ardhi, viwanda,magari. Unajua msiba wa masikini huisha baada ya tatu au arobaini? Lakini msiba wa tajiri hudumu hata miaka 10 kisa Mali. Hao ndo waandike wosia ambao wajanja wakiuotea haufanyiwi kazi.
 
Anyway, huu ni utashi wako, unatakiwa uheshimiwe. Ila amini kwamba inawezekana wakawepo ndugu ambao wanatolea macho hivyo vitu vidogovidogo vya ndani. Ukikata moto tu ndugu wanasalandia hivyo vitu.
 
Hata CV yako mwenye uwezo wa kuiandika vizur ni marehemu,inaelezwa tuandike CV kuhusu historia ya maisha yetu tangu kuzaliwa,shule,kazi ndoa nk hii inasaidia walio hai wasipate sana tabu ya kuandika historia yako ukifa
 
Anyway, huu ni utashi wako, unatakiwa uheshimiwe. Ila amini kwamba inawezekana wakawepo ndugu ambao wanatolea macho hivyo vitu vidogovidogo vya ndani. Ukikata moto tu ndugu wanasalandia hivyo vitu.
Unalolisema ni kweli lakini akuambia ndugu yangu wewe, hata Kama ukiandika wosia ndugu walafi wakiamua wosia haufiatwi na ukifuatwa watu watapigana vichomi mpaka Mali zitaenda Kwa walafi.

Kikubwa gawa ukiwa hai kwakumilikisha kabisaaaaaa, kama viwanja, nyumba, mashamba,magari n.k Ili ukifa tu Kila mtu anachukua chake.
 
Hata CV yako mwenye uwezo wa kuiandika vizur ni marehemu,inaelezwa tuandike CV kuhusu historia ya maisha yetu tangu kuzaliwa,shule,kazi ndoa nk hii inasaidia walio hai wasipate sana tabu ya kuandika historia yako ukifa
Uko sahihi kabisa mkuu.

Hayati Jaji Raymond Ruhumbika aliandika wasifu wake mwenyewe tangu kuzaliwa hadi ugonjwa. Familia/ndugu walimalizia kipengele cha matibabu hospitalini na kifo.

Kwakweli wasifu wake ulikuwa na mtiririko wa aina yake.
 
Unalolisema ni kweli lakini akuambia ndugu yangu wewe, hata Kama ukiandika wosia ndugu walafi wakiamua wosia haufiatwi na ukifuatwa watu watapigana vichomi mpaka Mali zitaenda Kwa walafi. Kikubwa gawa ukiwa hai kwakumilikisha kabisaaaaaa, kama viwanja, nyumba, mashamba,magari n.k Ili ukifa tu Kila mtu anachukua chake.
Mkuu, ukishaandika wosia hakuna wa kuingilia matakwa (wishes) zako. Labda uzungumzie kulogana.

Kumikilikisha mali zako ukiwa hai ndiyo hatari zaidi. Kuna watoto vichaa, wakijua umeshawagawia wanaweza ku-demand mali zao na hutakuwa na cha kufanya kwasababu tayari kutakuwa na transfer of ownership.
 
Tena wakiona unazingua wanakuua kabisa wagawane mapema.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom