Black Opal
JF-Expert Member
- Jan 22, 2023
- 233
- 298
Habari Wakuu,
Leo asubuhi wakati naenda kwenye michakato yangu nimekutana na magari mawili njiani yakiwa na wanafunzi, kwakweli yanaogopesha na inatisha. Gari moja lilikuwa la wanafunzi na jingine la mtu binafsi lakini pia limebeba wanafunzi.
Gari lililobeba wanafunzi, gari la Shule ya St Mary's Schools T 748 DJV(W) (hii herufi ya mwisho haionekani vizuri) lilikuwa limeegemea upande wa kushoto yaani kama linataka kuanguka, tairi upande huo inakaribia kuguswa na body ya gari hata kwa mtu ambaye si mtaalamu wa magari ataona kabisa kuna shida. Ndani watoto wamebanana, wa kubebana wamebebana, wengine wamekaa chini na hapo mzazi/mlezi anatoa hela yake. Video hiyo hapo chini👇
Hii nyingine ni gari ya mtu binafsi, lakini kilichonishangaza ni jinsi walivyowabeba wanafunzi hao. Kwa haraka haraka nadhani watoto hawa walipewa lifti, sasa hata kama ni lift unawawekeje kwenye buti hivi kama mizigo? Si bora uwaache usiwape lifti kuliko kufanya hivi? Hii ni sehemu ya mizigo halafu unaweka watoto wa watu hivyo, hapo huwasaidii unawaweka kwenye hatari zaidi. Sidhani kama wangekuwa watoto wake angefanya hivi. Jionee mwenyewe hapo👇👇
Nadhani wakuu mtakuwa mmekutana na mambo kama haya barabarani huko, wazazi mnafatilia kujua mabasi ya shule yanayobeba watoto wenu yana hali gani na watoto wanakaaje ndani? Au mkishalipa pesa ya basi mmemaliza?