Wazanzibari msikubali kufanya kosa kama alilofanya Uingereza la kujitoa EU, mkitoka kurudi ni ngumu na ni gharama sana

Lu-ma-ga

JF-Expert Member
Sep 21, 2010
4,780
3,227
Itakuwa kosa kubwa sana kwa Wazanzibari kukubaliana na sera ya serikali tatu inayopigiwa chapua na ACT chini ya jemedali Maalim Seif.

Siku zote formula ya 1+1 = 3 ina manufaa makubwa na hasa kwa muungano wetu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania japo una changamoto zake, lakini changamoto siku zote zimekuwa zikipungua na ipo siku zote zitaendelea kupatiwa majibu.

Historia ni Mwalimu
Historia ya hivi karibuni imetufundisha juu ya madhara ya kujitoa kweny umoja wa nchi shirika. Miaka ya hivi karibuni Uigengereza tumeishuhudia ikishadadia kujitoa EU na baada ya debe kulia sana EU iliiruhusu uingereza kufuata taratibu za kujitoa na hatimaye wengi wakapiga kura ya kujitoa. Baada ya siku kadhaa upweke kwa Uingereza ulianza kuwaingia kwa kasi ya ajabu.

Uingereza waliamini kuwa wataweza kuwa peke yao kwa kuwa wanauchumi imara, upweke uliendelea kuwakumba na kabla ya kufika mbali Corona ikawakumba wakaanza kupambana nayo kama Uingereza, kwa upande mwingine EU imeendelea kukabiliana na madhara ya CORONA kwa ushika wa nchi zote ndani ya EU kwa kuhakikisha watafuta majibu kama jamii moja lakini bila ushiriki wa Uingereza.

Sawa Uingereza ina hali ngumu maana inakwenda kwenye Taasisi za kibenk kama nchi, wakati EU wanatembelea nguvu ya 1+1 =3
Waingereza walikosea mahesabu wakadhani wataweza wakiwa peke yao kama UK, kumbe ulikuwa uamuzi usio na majibu, leo hii wanaenda mbali zaidi kama UK, baadhi ya nchi ndani ya UK zinataka KUTENGANA na UK na kurudi EU,lakini is already too late.
Ubaguzi ukianza huwa unatabia ya kupinga kambi kwenye jamii ile hadi kufikia ubaguzi wa kiukoo na kifamilia.

Mwisho
Ninaamini Wazanzibari hawatakubali kuingizwa mkenge na wachache ambao lengo lao ni kukamata dola bila kujali ni mbinu gani imewafikisha na hata kama matokeo yake ni mabaya kwao siyo hoja.
 
Brexit na muungano/mkorogano wa Tanganyika na Zanzibar, ni sawa na kulinganisha machungwa na embe vile ;)
Labda nikupe kidokezo tuu, kilichopo sasa hakina maslahi ya mzanzibari. Hakuna atakae jutia kupata mamlaka yake na kuacha kuomba omba ruhusa uko Dodoma.
 
Brexit na muungano/mkorogano wa Tanganyika na Zanzibar, ni sawa na kulinganisha machungwa na embe vile ;)
Labda nikupe kidokezo tuu, kilichopo sasa hakina maslahi ya mzanzibari. Hakuna atakae jutia kupata mamlaka yake na kuacha kuomba omba ruhusa uko Dodoma.
Zanzibar itabakia kua koroni la Tanganyika milele, maana gharama za kuvunja muungano ni ngumu kwa Zanzibar kuzimudu. Zanzibar imeitumia sana Tanganyika kujikuza kiuchumi, tulizeni bori tu.
 
Zanzibar itabakia kua koroni la Tanganyika milele, maana gharama za kuvunja muungano ni ngumu kwa Zanzibar kuzimudu. Zanzibar imeitumia sana Tanganyika kujikuza kiuchumi, tulizeni bori tu.
Kajifunze kiswahili kwanza, koroni ni matusi hayo kwa kiswahili cha huku visiwani. Inabidi utake watu radhi kwanza.
Bori pia ni matusi, hata tukulituliza inabidi mtulipe fedha zetu tunazowadai. Halafu utajua kama nani kamtumia mwenzake.
 
Back
Top Bottom