Safi sana Mkuu wa mkoa. Lakini nashauri tusiishie hapo. Kuna watu wako nyuma ya uozo huu. Nikuibie tu siri: Kuna maafisa utumishi/tawala ambao wanakagua payroll na kuidhinisha kila mwezi kabla ya mishahara kulipwa. Hawa wanapaswa kufukuzwa kazi. Huwezi kuendelea kuidhinisha mhahara wa mtumishi ambaye hayupo kazini na kuruhusu mshahara wake kuendelea kulipwa kwa zaidi ya mwaka! Hii haiwezi kuwa bahati mbaya. Pili, fedha hizo zilikuwa zinalipwa kwenye akaunti za watu (kwa mfumo wa ulipaji serikalini kwa sasa), je ni nani hao? Watafutwe na kushitakiwa mahakamani. Tatu, wafuatilie pia wakuu wa Idara zinazohusika. Kwa nini waliruhusu hali hii kuwepo? kazi yao ni nini? Ninavyofahamu, katika sehemu yoyote ya kazi, 50% au zaidi ya budget huwa ni kwa ajili ya personnel. Inashangaza kwamba unakuwa na mtu anaitwa DAP au RAS au DAS lakini hajui na hawezi kuthibiti 50% ya bajeti katika idara yake. Kwangu, mtu wa namna hii hapaswi hata kuwa na cheo hicho in the first place.