Watumiaji wa king'amuzi cha Azam ushauri wako Muhimu!!

Liparamba

JF-Expert Member
Jun 12, 2016
690
592
Nimekuwa nikitumia king'amuzi cha Azam toka Mwaka Jana tatizo lililopo huwa kila nikilipia kupitia M Pesa naambiwa "transaction Canceled", kwahiyo nikimpigia aliyeniuzia(mweye duka).
Huwa ananiambia tuma Kwangu nikununulie nimekuwa nikifanya hivyo na kuchukulia kawaida .

Juzi ilibini nilipie huwa na Lipa kifurushi cha 15000Tsh. Nikajaribu tena kupitia kwa M-PESA yangu jibu ni lilelile nikapotezea nikapiga simu Makao Makuu Dar(Customer care) nikaeleza nikataja namba za kwenye kadi, jibu nililopewa kwamba huwa siwezi kulipia kwa M-PESA au Huduma yoyote ya kifedha sababu hicho king'amuzi changu ni kwa matumizi ya Malawi au Uganda viliingia nchini kwa Makosa ndiyo mana hata Azam HD,TV one sizipati.

Nikauliza nafanyeje ili niwe nalipia mwenywe? Nikajibiwa nitafute kingine au niendelee na mfumo huohuo wa kutuma Pesa kwa mwenye duka nililo nunua yeye ataendelea kunilipia.

Nikauliza kwani yeye analipia wapi? Na kwanini sistahili kulipa mwenyewe kupitia M-PESA yangu? Badala ya kujibiw nikaulizwa kuna tatizo lingine mbali na hilo? Nikaishiwa pozi.

Napata maswali mengi yasiyo na majibu au niliingizwa chaka na muuzaji au mwenyewe Azam?

Samahani kama sitoeleweka!!
 
Mbona umeelezwa vizuri tu.Azam wana provide service nchi nyingi huenda ikawa decoder uliyonunua ni ya nchi nyingine.
Kuhusu suala la kulipa kwa aliyekuuzia haliwahusu kama ukilipia na unaona channels endelea kulipia
 
Jikaze Ndugu, kama upo mpaka kiuze kwa nchi tajwa ili ununue cha tz
 
Mshitaki aliyekuuzia
 
Ushauri ukienda nunua kisimbuz cha azam uliza kwanza hiki ni kwa matumizi ya hapa nchini au nchi jirani? Usije ukawa mtumwa wa kutuma pesa kwa wakala akununulie, hiv na yy huyo wakala ananunua wap isije ikawa ni dili kiwango anacholipa ni kidogo kuna pesa inabaki...
 
 
Pole sana kama unalipa 15000/ na Azama HD hupati unaibiwa ndugu yangu.

Sioni kosa la watu Azam, na huna haja ya kuwalaumu, hapo dawa ni kunyooka na muuzaji wako iweje akuuzie halafu asikupe maelezo ya kina kuhusu hicho king'amuzi.

Huo ndio ujanja wa wafanyabishara wetu, kupenda faida kubwa bila kujali mlaji
 
Usisumbue kichwa kaka kuna watu wanaweza kuzungumza kwa niaba yako, na wakanyoka vizuri. Tanzania tunaenda kijamaa sana ndo shida tuliyonayo.
 
Rudisha kwa aliyekuuzia, umejibiwa vizuri tu, pengine huyo aliekuuzia aliviiba kutoka huko Malawi
 
Wauzaji ni wahuni deal nao severely, mm walishawahi kuniuzia king'amuzi cha mtu mwingine ambacho kilishasajiliwa, walinipa king'amuzi kingine kipyaa na hela juu ya usumbufu, vinginevyo wangenyea debe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…