matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,634
- 18,552
Kwa utafiti wangu usio rasmi hiki ndicho nimegundua.
Yule jamaa aliyekuwa anafanya kazi za kulipwa 3000 kwa siku, tena akitegea anakatwa. Kazi ngumu kiwanda cha samaki. Alipoanza kufundisha tution akajenga nyuma, alipopata fursa ya kusoma zaidi leo ni muathiri mkubwa chuo flani nchini.
Yule jamaa Graduate aliyekuwa anazunguka kama chizi na kikapu cha urembo vijijini, akizunguka minadani mchafumfachu, alipopata kazi ya kawaida tu NGO alijenga nyumba tatu wakati bosi hana hata kiwanja.
Yule graduate aliyekuwa mlinzi kwenye ile kampuni, alipopata kazi yenye mshahara 1M, aligeuka mfanyabiashara mkubwa wa kusafirisha ng'ombe na kunenepesha.
Yule graduate aliyekuwa anauza nyanya na viungo kwa baiskeli kuanzia gongo la mboto hadi Tabata, alipopata kazi ya 500K jijini, alinunua kiwanja na kujengq nyumba wakati na kuoa na sasa anawatoto watatu. Anaishi kifahari utadhani anapokea 5M.
Yule waziri mkuu mstaafu wa china, alipotimuliwa akafulia akawa anafanya kazi za aibu ili yeye na mkewe wasife njaa. Deng Xioping alipomkumbuka na kumpa ugavana. Alifanya Economic Miracle jimbo lile na ikabidi apewe uwaziri mkuu ili alichokifanya hapo afanye china nzima.
Mambo ya maisha.
Biblia inasema " katika kila kazi mna faida" Mithali 14:23. Faida sio pesa tu hata kujengewa uwezo utakaokusaidia siku ukihamishwa daraja la kipato.
Usikae nyumbani kisa umesoma na unasubiri kazi za au mitaji. Ingia mtaani hivyohivyo kuna faida. Kapike deiwaka kwa mama ntilie.
Sukuma mkokoteni/guta/torori
Kuwa winga
Jaribu udalali
Kuwa houseboy/Girl
Fanya vibarua mashambani na kwenye nyumba za watu.
Kuwa kondakta au dereva au mpiga debe.
Kila kazi ina faida.
Ni hayo tu
Mtumishi Matunduizi.