Watu 9 waliohusika kutungua chopa na kumuua rubani wakamatwa

Eti polisi wamekamata majangili Simiyu baada ya kuwakamata mmoja akasema yeye alihusika kuitungua helkopita ya doria. Jamani hivi mtu mwenye uwezo wa kutungua helkopita kweli anaweza kukubali kosa kirahi hivyo? Tena bila hata kufikishwa mahamani?

Mambo ya jeshi waachie wenyewe.

Kuna teknolija kibao za kuhoji mtu nyingine unampiga mtu nusu kaputi,au unamdunga sindano,au kumnywesha uji hata wa mtori lakini ulioungwa kitu nk anaropoka kila kitu akiwa kapoteza fahamu za kawaida.Kama walikuwa majambazi mia yaliyoshiriki anakutajia majina yao yote mahali walipo wanapoweka silaha na kuongea kila kitu.Akizinduka akirudi akili timamu hajui kilichotokea lakini kamwaga kila kitu.

Wewe si unajua njia za zamani ilikuwa jambazi lingine hata ulikate na shoka korodani halisemi wala kutoa siri zao.Sasa hivi shughuli rahisi wewe shiriki uhalifu au ugaidi halafu wakudake .Mtandao mzima Polisi wataudaka kupitia wewe mwenyewe
 
Majangili wengi ni MAJUNYA huwezi amini.
Mtu ukisikia ameitwa Jangili usije ukadhani kwamba huyo mtu labda anambinu zote za kijeshi au za kiintelijensia.
Hao watu ni MAJUNYA kishenzi.hata mazingira na maisha yao ni yakishamba elimu duni lakini uwezo wao kwenye shabaha ni noma.
 
Sio rahisI kiivyo ingekuwa wanashikwa kirahisi hvy ujangili ungeisha tanzania
Usibishe Kumbuka Upelelezi ni FANI watu wanakalia DAWATI na wanaGraduet....na kwa nchi hii ukikuta tukio linapotezewa na jamaa wa Usalama basi ujue waliopewa hilo jukumu wana maslahi nalo Vinginevyo hata ufanyeje utadakwa tu.....Tambua hili tukio linahusisha KIFO cha MGENI lazima serikali itataka kujiosha mbele ya Macho ya Kimataifa kwamba wanamaanisha kupambana na Majangili
 
Hawa wakibanwa sawasawa wanaweza kuwataja watu wanaowàuzia hizo pembe na meno ya tembo, wasiishie ktk tukio la kuua tu wabanwe ili vigogo wanaonunua nao wakamatwe waunganishwe kwenye kesi ya mauaji hayo
 
Mambo ya jeshi waachie wenyewe.

Kuna teknolija kibao za kuhoji mtu nyingine unampiga mtu nusu kaputi,au unamdunga sindano,au kumnywesha uji hata wa mtori lakini ulioungwa kitu nk anaropoka kila kitu akiwa kapoteza fahamu za kawaida.Kama walikuwa majambazi mia yaliyoshiriki anakutajia majina yao yote mahali walipo wanapoweka silaha na kuongea kila kitu.Akizinduka akirudi akili timamu hajui kilichotokea lakini kamwaga kila kitu.

Wewe si unajua njia za zamani ilikuwa jambazi lingine hata ulikate na shoka korodani halisemi wala kutoa siri zao.Sasa hivi shughuli rahisi wewe shiriki uhalifu au ugaidi halafu wakudake .Mtandao mzima Polisi wataudaka kupitia wewe mwenyewe
Kwa Mara ya kwanza naona umeandika kwa kutumia Akili yako Safi sana.....huo ndio ukweli zamani majambazi yalikuwa tayari kufa lkn hayakukubali kufunguka ila sasa mambo yamebadilika sana
 
Ni shida sana humu jamvini mtu kusema pumba tupu za kukandia kuonyesha kwamba serikalini hakuna wajuzi wa mambo ya Upelelezi waliobobea,so mtu anaharisha upuuzi kuonyesha hamna kazi inayofanyika,nchi zilizoendelea wanajua kwamba Tanzania kuna watu wenye uwezo mkubwa kuliko walivyodhani wao,mfano ni mlipuko wa mabomu ktk ofisi za USA kwa Tanzania na Kenya,ukifanya jambo ukadhani utaishia mtaani kimya jua watu wanapotezea,ila wakiamua kula sahani moja na wewe huchomoki.
 
Akili za aina hii ni kielelezo cha watu ambao hawawezi kuja kuendelea, kila siku unahisi unadanganywa, unahisi unadhulumiwa, kila kukicha unahisi unatapeliwa. Matokeo yake huwezi kuwa na constructive mindset. Unaishia kuwa mdogo katika ujengaji wa hoja, unaishia kuwa mlalamikaji aliyejaa mifano mingi ya siku zilizopita ambayo unaitumia katika kujenga hoja dhaifu. January Makamba aliwauliza wapinzani "what would you have done differently?".
Hawajielewi tu
 
Hawa wakibanwa sawasawa wanaweza kuwataja watu wanaowàuzia hizo pembe na meno ya tembo, wasiishie ktk tukio la kuua tu wabanwe ili vigogo wanaonunua nao wakamatwe waunganishwe kwenye kesi ya mauaji hayo
Soko kuu lipo China...rejea ile report ya Al Jazeera..ndani ya ule report wadau walimwaga kila kitu bila kujijua..
 
Harakisheni hukumu za haya majitu.....sipati picha ishu kama hii ya kutungua ndege na kumuua rubani ikawa na hukumu ya kunyongwa mtu halafu magu akapelekewa asaini adhabu hiyo..
 
Tunao wapa zamana ndio hao wausika wakuu.iv inawezekana vp mimi raia wa kawaida nifahamu kuwa police fulani ni mwizi mkubwa ila wenyewe wasijue? Kama wako makini na jazi zao waende morogoro kuna mapolisi ambao ni wezi kabisa wasisubili adi wakutwe kwenyematukio.majina ni mjalubi, pambano, matiku na wengine wengi tu wakionesha hali ya kuwashugulikia nasi raia tutaonyesha ushilikiano zaid...
 
Sarakasi hizi wala hazieleweki.
Hizo meno sijui huwa zinapotelea wapi baada yakufika Polisi.
Huwa hukumu yao pia ni ya siri maana hatujawahi ona wapi wamefungwa
 
Lazima ifikie mahali ambapo kama kuna jambo jema linafanyika kwa manufaa ya nchi wote kwa umoja wetu tuliiunge mkono.
Haina maana serikali inapojaribu kutatua tatizo fulani watu wengine waanze kubeza. Jamani serikali ni sisi wenyewe. Viongozi ni stewards tu. Wanachokifanya ni kutekeleza Yale ambayo ni matakwa yetu. Hivyo kama majangili yamekamatwa tena kwa haraka basi yahukumiwe kwa uharaka pia. Na kesi zingine nazo zihukumiwe kwa uharaka ili hali itendeke. Nafikiri adhabu Kali itolewe iwe ni fundisho kwa wengine.
 
Eti polisi wamekamata majangili Simiyu baada ya kuwakamata mmoja akasema yeye alihusika kuitungua helkopita ya doria. Jamani hivi mtu mwenye uwezo wa kutungua helkopita kweli anaweza kukubali kosa kirahi hivyo? Tena bila hata kufikishwa mahamani?

Haina tofauti na ile ishu ya Kova kuhusu aliyemteka Dr Ulimboka, Kova alituambia eti wamemkamata muhusika baada ya yeye kwenda kuungama kanisani, watu tulijiuliza hivi kweli jeshi letu linasubiria wahalifu waungame kanisani ndiyo liwakamate? Baadae ikasemekana jamaa alikuwa chizi hivyo akaachiwa huru.

Haya maigizo hayalisaidii taifa nadhani mnawapa kichwa wahusika wa haya matukio maana wanajua wakiyafanya watakamatwa watu wengine.

#ngumu_kumeza
Movie ndio kwanza linaanza hapo kama kawa
 
Jeshi la Polisi Simiyu limewakamata watu 9 waliohusika kutungua helkopta ya kampuni ya Mwiba na kumuua rubani wa helkopta hiyo Rogers Gower.

Baada ya kuuawa kwa rubani Rogers Gower, familia yake imechangisha fedha ili kuendelea kupambana na ujangili nchini kuenzi kifo chake.
View attachment 321824
rubani Rogers Gower wakati wa uhai wake

===================
Je hii kesi iliishia wapi?
 
Back
Top Bottom