Watoto wa mjini vs wajanja wa mjini...!

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,640
729,672
Jeshi la Polisi Tanzania kwa siku hizi mbili wametumia si chini ya shillngi millioni 300 kwa kutengeneza hofu"fear of unknown" na kwenda kupambana na hofu waliyo jitengenezea wao wenyewe.

1.Hatua ya Kwanza walihakilisha wanamdanganya Mama wawa tu kuwa anaenda Kupinduliwa Mbeya na BAVICHA

2.Wakaokoteza hotuba za Twaha Mwaipaya (Mwenezi Bavicha) na Moza Ally (Makamu Mwenyekiti Bavicha) huko mitandaoni

3.Wakatengeneza taarifa feki ya Intelijensia uchwara na kuwapelekea wakubwa wao.

4.Wajanja wa TISS walijua ukweli kuwa hakuna mapinduzi yoyote yaliyopangwa kwa Jina la Gen Z

ila sababu ya tamaa ya "Madokezo Sabili" na wao wakaona pia kuna fursa ya Kulipana Posho za ufuatiliaji na udhibiti wakaliunga mkono Tango Pori (False information)

5.Mamlaka na Viongozi wa Serikali wakaingizwa mkenge na Watoto wa mjini,Wakapitisha Operesheni dhibiti BAVICHA

6.Serikali ya mkoa Mbeya ikapewa maagizo ya haraka,kuanza kukaa,Kupanga na Kudhibiti BAVICHA
Na wao wakasema "Allahamdulillah" hapa kuna Kulipana posho za bure.

7.Afande Awadhi akawasha chuma akiwa na dereva na Walinzi wake hadi Mbeya
alijua ukikaa Dodoma peke yake Dokezo linaweza Kukupita ujalamba Perdiem.

8.Afande Awadhi akaanza kufanya na majukumu ya Afande Misime ambaye alionekana kutojiongeza tangu mapema au sijui yupo bize na kesi ya Binti aliyebakwa na kulawitiwa..?

Basi Afande Awadhi kaanza kuwa Mkuu wa Operesheni kwa kutoa amri na vitisho,hapohapo akawa ndiyo Msemaji wa Jeshi la Polisi

Awadhi akawa kama Khalid Aucho pale Yanga ,yani anakupa alafu anaiomba tena.

Anatoa majukumu kwa Ma RPC alafu anasafiri kwenda Mbeya kufanya majukumu yale yale aliyotoa yeye akiwa Makao pale Dodoma...acha kabisaaaaa

Afande Misime sikazubaa bhanaa,shauri yake,kwenye Paylist ya Kusiaini Posho ataisikia tu redioni pale Makao.

9.Bavicha walivyo wahuni na wao,walipojua Maafande wana Mzigo wakajiongeza kimjini mjini.

Wakati wamepewa amri ya Kurudishwa makwao kwa magari ya Kukodi.

Wakawajibu mapolisi kuwa Kule Mbeya katibu Mkuu Mnyika ndiyo alikuwa anaenda Kulipa Pesa za Kukodi Magari na Kujaza mafuta ya Kurudia kumbe ela wanayo walichangishana laki laki.

Maafande wakaingia wazima wazima,Wakaanza Kulipa madereva na Kujaza mafuta njiani bureeee

Si ndiyo Madereva wakashtuana na wao,wakati wanawarudisha Bavicha makwao chini ya Ulinzi

"Oyaaa Maafande wana ela hawa"

Basi unaambiwa dereva anazimia gari katika gia ya "neutral" anaiweka pembeni.

Maafande wakija wanauliza mbona umesimama.? anaambiwa mafuta yameisha,Vijana wa Bavicha wanaulizwa nani ana ela ya Mafuta wanajibu Mnyikaaaaaaa

ndiyo alikuwa anaenda Kulipa magari.

Basi Maafande mtonyo si upo wa Kutosha,wanaagiza bodaboda dumu la mafuta,alafu wanamwambia Dereva ingia "sheli" weka full tank tuendelee na safari.

Watu weweeeee,Mjanja kakutana na Mjanja,Mpigaji kapigwa.

10.Ghafla viongozi wa CHADEMA, na BAVICHA wakiwa wameshikiliwa wanabembelezwa wapatiwe magari warudishwe makwao.

Sugu anawaambia kwangu mimi ni Mbeya,wakamwambia Sugu ni uongo huo,Usijifanye mjanja kwako wewe ni Dar unakofanyanga Bongo flavor honors

Sugu akabaki mdomo wazi..!

Masihala masihala Sugu akapewa Landcruiser mpyaaaa,maafande kama 7 hivi,full tank na posho wanampeleka nyumbani kwake Dar kutokea Mbeya.

Chezea mtonyo wewe.? hizi bahati hazijagi mara mbili mbili Bob.

11.Lissu wakaanza kumepeleka nyumbani kwake Songwe kutokea Mbeya.

Kufika maeneo ya Vwawa wanauliza bodaboda,nyumbani kwa Tundu Lissu ni wapi.?

Bodaboda wakawajibu Lissu kwake si Dar es saalam..? Maafande wakawakaaaa,wakawaambia mnatudanganya na mnajua kulifanganya jeshi la Polisi ni Kosa la Jinai..?

Wakawa wanataka kumpeleka Lissu nyumbani kwake Sumbawanga

kama siyo Tundu Lissu kudai dawa zake alizoziacha Dar,Tegeta ilikuwa waende naye Namanyere kule Rukwa.

Wakamuuliza Lissu,dawa zipo wapi.? Tundu akawajibu Tegeta,Dar es saalam,Wakamwambia tunakupeleka ufuate Dawa zako, alafu tunakurudisha nyumbani kwako Sumbawanga,usitufanye wajinga.

Kama siyo Lissu kufika Tegeta na Kugoma kutoka tena nje ya geti tena,muda huu huenda wangekuwa Mikumi wanampeleka nyumbani kwake Sumbawanga.

11.Mbowe ndiyo funga kazi,Kila akisema Kwangu ni Dar es saalam, Wanambishia wanamwambia kwako wewe ni Machame Mwenyekiti.

Mwenyekiti usitufanye wajinga,tunajua ulikuwa Mbunge wa Hai na tuliona nyumba yako mitandaoni ipo Machame

Mbowe akawaambia nimekuja na ndege mmenikamata Airport ya Songwe ,Ticket yangu ni "go and return" nimeshailipia nisipopanda ndege inakuwa imepotea bure.

nipelekeni airport tafadhali ndege ikija mnipandishe nirudi Dar es saalam.

Maafande Wakamwambia "Mwenyekiti acha Ubinafsi" ulipanda ndege utahujumu uchumi na mapato ya nchi na hilo ni kosa jipya kwa mujibu wa sheria.

Vituo vya mafuta havito uza mafuta,familia zetu zitakosa chakula,Mama lishe njiani hawatouza chakula,Matairi ya gari hayatoisha,vipuri vya gari havitoisha,Usijitizame wewe Mbowe tafadhali tazama na wenzio pia.

Mbowe akakubali kwake ni Machame akapewa Landcruiser hadi Dar es saalam alipoacha nguo zake ili aende kuzibeba kisha aende nao Machame,kama si Mbiwe kugoma kutoka ndani alikoingia kuchukua nguo muda huu angekuwa njiani Segera anarudishwa Machame.

Hatimaye Wahaini wakaachiwa wote bila masharti na bila kuwekewa dhamana na mtu yeyote kisha Wahaini wakapewa na Bonus ya usafiri wa kurudishwa makwao kama motisha kutoka Jeshi letu bora na tukufu la Polisi Tanzania.

ili siku nyingine wasiache kupanga tena mapinduzi dhidi ya serikali ya Samia.

Basi ndiyo hivyo ndugu wananchi,hivi ndiyo siku mbili hizi kodi zenu zilivyo tafunwa kirahisi kabisa na Wajanja.

Kama wewe ni fundi ujenzi au ni Mkuu wa shule na unamdai Afande Awadhi leo ndiyo siku ya Kumshtua japo kwa sms tu.

"Afande Awadhi habari za leo.? Pole na kazi.."

Ukipata chochote usiache kunikumbuka na mimi niliyekutonya ,nakuwekea na mawasiliano yangu usipate tabu kutuma muhamala .😂😂🤣
20240813_125236.jpg


Boniface Jacob
Ex-Mayor
0712 239 595
 
Back
Top Bottom