Habari wana jamvi,
Kila aliyepo DSM naamini anajua kinachoendelea kwa sasa,habari ya mjini ni hii bomoa bomoa ya nyumba za mabondeni.Kwa kweli inaumiza sana,ukipita pale Mkwajuni kwenye kibonde karibia nyumba zote zimesafishwa kabisa.Kinachouzunisha mimi ni kwamba hata nyumba za kwenye kilima zinabomolewa.
Rais wetu Magufuli kumbuka ulisema wewe una huruma na watanzania,fikiria wale binadamu wataishije kwa kipindi hiki,fikiria pia kwamba mtu kaishi DSM pengine zaidi ya miaka 20 ndio akajenga kijumba chake,halafu ninyi mnabomoa kwa siku moja, kweli ni haki hiyo?
Fikiri mtu ambaye hana kazi ya kumpa kipato cha kutosha leo hii anabomolewa kijumba chake,anayepika chapati na kushona viatu leo ataishije?
Mbaya zaidi hili zoezi limekuja mwisho wa mwaka,kipindi cha wapangaji kulipa kodi,xmass watoto wanahitaji kuvaa,ada za shule watoto kulipiwa na kijumba kinabomolewa. Je, hayo ni maisha?
Mbona lile ghorofa pacha za pale mtaa wa Indra Gandhi Posta linalohitajika kubomolewa baada ya pacha lake kuanguka hadi leo halijabomolewa, kama sio uonevu ni nini?
Inauma sana