Watanzania tunalishwa sana uchafu na sumu kwa kujua na kuto kujua

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
4,124
10,923
Ukiangalia Sakata la Mbwa kule Hedaru utagundua kwamba haya matukio yanajirudia rudia sana mitaani na hii inasababishwa na uuzaji holela sana wa vyakula bila kufuatiliwa.

Ukiachana na Mbwa, pia kulishana Vibudu hii ndo zaidi, Wanyama hasa Ng'ombe wanao jifia huwa hawatupwi bali huchunwa na kuiingizwa Butchan, hata kuku, na hii inaenda hadi kwenye mayai pia full of antbiotic.

Nani anatupa mayai yake kisa kawaoa kuku antibiotic? Mtu atupe trei zake 20 kwa siku kisa kawapa kuku dawa? Hapana mayai yale yanaingizwa sokoni na watu wanayapiga kwenye chips na kadhalika.

Kuku wanaweza kuwa ni hawajafa ila unakuta kuku wamepigwa antbitic nyingi sana, kuku hawa waki sasa wanapewa mno antbiotic ambazo ni mbaya mno kwa mwili wa binadamu.

Njoo kwenye matunda sasa na Mboga za majani, hapa ndo kuna sumu za kutisha, mboga zile zinapigwa mno mbadawa na watu wanaweza piga dawa leo na kesho wakachuma kupeleka sokoni kuuza.

Tunalishwa sana Sumu kwa kiwanho ambacho sisi hatukijui, na Serikali imelala inaonea watu huruma eti Wapiga kura, Bila kuweka mifumo ya kukagua vyakula vyote kabla haviaingia sokoni tutapata shida sana.

Mbaya sana hadi watoto wadogo tunawalisha sumu ingawa ni kwa kuto kujua, Una mnunulia mtoto wako Tango au tikitik maji, unamtengenezea juice kumbe ni sumu tupu una mnywesha.

Katika vitu ambayo Serikali inapaswa kuwa wakar kupita maelezo ni Swala la Usalama wa vyakula wanavyo lishwa watu,
 
tule nn sasa ambacho ni cha asili
 
Kitu salama nenda kaishi shamba lima vyakula vyako usitie madawa, mchezo unaungua na kuisha.

Hata huko shamba kwenyewe vitu vyote ni GMO, kwahiyo hakuna pa kutokea.
 
Hivi hata kama ni wewe mkuu, ng'ombe wako amekufa, umemuhudumia kwa miaka nenda rudi, utakubali kumtupa?

Kuku umewapa antibiotic, eti ukae siku mbili au tatu bila kuokota mayai?
Wewe kuweza mkuu?
Maana hiyo ndiyo faida yenyewe.
Au ng'ombe umemchoma dawa eti maziwa usikamue hayafai kwa matumizi ya binadamu, wewe unaweza mkuu wakati ndiyo faida yenyewe?
 
Kwenye usalama wa chakula watanzania na serikali haija weka maanani Sana ila kuna hatari kubwa Sana uko ndio maana Dada zetu siku hizi wanatoka vitambi Kama viwavijeshi.
 
Mfumo ndio umetupelekea hapa
Tunaishi hivi

Unaamka Asubhi unaenda Kazini Unarudi Jioni

Muda wa kupata Kufuga Kuku huna
Muda wa Kulima Bustani Huna
Muda wa kufuga Ng'ombe huna Tena Umepanga
Watoto wenyewe wa Kuwapa Majukumu hayo huna

Sasa Hivi watu wanalima Kilimo biashara Na Kinapigiwa Kelele sana Kuliko kuangalia Wanalimaje Hao Wakulima
 
Hapo kwenye mbogamboga, usipime. Huko dodoma.maeneo ya swaswa mbogamboga zinalimwa eneo ambapo majitaka hua yanaenda kumwagwa na haya magari. Hayo ndo ya kumwagilizia mboga.
 
Unachoongea ni sawa lakini pia ni uzembe wetu binafsi. Kwa maana kitu kama vegetables, unaeza kupanda hapo hapo kwako kwenye mifuko ya nylon na zikakua vizuri tu. Ukitaka nyama nenda machinjioni, tafuta connection ya ustaadh mmoja alieshika dini, uwe unaenda siku moja kwa wiki unachukua mzigo mkubwa unaeka kwenye fridge. Kwenye mayai tafuta ya kienyeji au fuga kuku wako freee range hapo nyumbani. Acha kula broiler, fuga wa kwako wa kienyeji utakaowapa mwarobaini instead of antibiotic. Kwenye matunda, jua matunda yanayopigwa dawa sana kama matikiti, achana nayo. Jitahudi kula matunda yasiyopigwa dawa kwa wingi kama ndizi. Mwisho, acha kutumia nyanya kwenye mapishi, tumia karoti in the place ya nyanya.
Angalizo: mimi mwenyewe sifanyi hayo yote ni baadhi tu, 🤣🤣🤣🤣 maana jf kila mtu tajiri
 
Siku hizi nyanya zikichumwa zinapigwa dawa kuzuia kuoza mapema then zinapelekwa gengeni. Ngoja carcinoma itunyooshe vizuri
 
Unachoongea ni sawa lakini pia ni uzembe wetu binafsi. Kwa maana kitu kama vegetables, unaeza kupanda hapo hapo kwako kwenye mifuko ya nylon na zikakua vizuri tu. Ukitaka nyama nenda machinjioni, tafuta connection ya ustaadh mmoja alieshika dini, uwe unaenda siku moja kwa wiki unachukua mzigo mkubwa unaeka kwenye fridge. Kwenye mayai tafuta ya kienyeji au fuga kuku wako freee range hapo nyumbani. Acha kula broiler, fuga wa kwako wa kienyeji utakaowapa mwarobaini instead of antibiotic. Kwenye matunda, jua matunda yanayopigwa dawa sana kama matikiti, achana nayo. Jitahudi kula matunda yasiyopigwa dawa kwa wingi kama ndizi. Mwisho, acha kutumia nyanya kwenye mapishi, tumia karoti in the place ya nyanya.
Angalizo: mimi mwenyewe sifanyi hayo yote ni baadhi tu, 🤣🤣🤣🤣 maana jf kila mtu tajiri
Huwezi ukajitegemea Kwa kila kitu. Uzuri mwenyewe pia umekiri Hilo. Hata ulime mbogamboga zako, ujifugie kuku wako, ulime matunda yako nk bado hutajitosheleza. Utasafiri au utakula vyakula mahali pengine nk. Kimsingi serikali ianze kutupia jicho usalama wa vyakula
 
Ni uzembe uliokithiri. Vitu vidogo vidogo hivyo, malizana navyo hapo hapo nyumbani kwako.
Lima mbogamboga hata kwenye makopo.
Weka Banda lako la kuku angalau watano ili upate mayai kila siku na nyama inapobidi.
IMG_2022-04-15-11-51-35-891.jpg
 
Back
Top Bottom