The Palm Beach
JF-Expert Member
- Dec 30, 2015
- 1,547
- 3,184
Hakuna ubishi kuwa, mambo katika nchi yetu hayako shwari. Uamusho na ukombozi huwa hauji katikati ya furaha ya kula na kunywa.
Mambo yalifikia ukomo wa uharibifu mwaka 2015 mara baada ya John P. Magufuli kutawazwa kuwa Rais wa 5 wa Tanzania.
Huyu alianza kwa kuharibu mfumo wa kisiasa na ustaarabu wa Watanzania. Akabomoa ustaarabu wa kupingana kwa hoja ktk majukwaa ya kisiasa bila kupigana ama kuuana.
Hayati John P. Magufuli akaja na utamaduni mpya usio na hofu ya Mungu. Utamaduni wa kuteka, kutesa na kuua wapinzani wake kisiasa waziwazi na mchana kweupe bila woga.
Baadhi walikubaliana na aina ya utawala na uongozi wake uliokuwa na kila elements za kishetani.
Akaharibu na kujiua mwenyewe kwa kupora mchana kweupe pasipo hofu haki za raia wote wa nchi hii kupitia chaguzi za mwaka 2019 na 2020.
Aaah, hii ilikuwa mbaya sana
Hat Mungu hakuweza kulivumilia hilo. Ilibidi aruhusu kifo kimwondoe mtu huyu ili kuikoa nchi yetu.
Hivi ndivyo ambavyo Mungu hufanya kwa wanaotawala watu kwa niaba yake wanapotaka kujiinua juu ya mamlaka yake.
Hebu kila mmoja ajiulize na kujibu swali hili
Kwamba, kwa aina ya uongozi wake John P. Magufuli uliojaa u - mimi na ukatili, kama angeruhusiwa kuwepo ktk nchi hii mpaka leo tunadhani angeshatengeneza himaya (empire) mbaya na ya hatari kiasi gani kwa raia akiwatumia watu hatari kwa sampuli ya Ole Lengai Sabaya, Bashite au Makonda, Jerry Muro, Ally Hapi, Job Ndugai na wengine?
Sikilizeni ndugu zangu wananchi wa Tanzania.
Tanzania inatoka mikononi mwa CCM taratibu na hatua kwa hatua
Nalisema hili kwa mamlaka toka ktk engo nyingine kabisa ambayo wengi hamtanielewa.
Mikakati kwa msaada wa Mungu mwenyewe ipo na inafanyika taratibu maana vita yetu sisi wengine tunaipigania ktk masafa mengine.
Nawaomba wote tuendelee kuchukua hatua. Tekelezeni wajibu wenu kwa hekima na busara. Tusinyamaze kimya.
Pale ambapo ni lazima kusema, kila mtu aseme.
Na pale ambapo ni lazima kutenda, kila mmoja na atende kwa busara akijua kuwa shetani mwizi na muuaji bado yupo ndani yao. Ukienda vibaya, watakuua tu...!!
Kifo rahisi kabisa cha Rais wa nchi aliye madarakani mwaka 2021 ni ishara njema sana kwa wanaotaka na kulilia ukombozi wa mara ya pili wa nchi hii toka kwa wakoloni weusi wenzetu waitwao CCM.
Magufuli na mambo yake akaishia hapo.
====================
March, 2021 kwa binde na msuguano mkali ndani ya CCM na serikali, mwanamama Mzanzibari Samia Suluhu Hassan akatawazwa Rais wa 6 wa Tanzania kuchukua mahali pa hayati John P. Magufuli.
Hili la mtu toka nchi nyingine iitwayo "Zanzibar" tena mwanamke kutawala nchi nyingine likawa kosa kubwa lingine kufanywa na CCM.
Wanaofikiri pafupi, wakadhani Tanzania imekombolewa ghafla. Hapana, mambo hayaendi hivyo...!.
Ukombozi unaenda hatua kwa hatua. Huyu mama amekuja kuusogeza ukombozi hatua inayofuata... Amekuja kuachilia maumivu mengine na kupitia kwake, Tanzania inakombolewa na Tanzania inakwenda ktk majira na msimu mwingine mpya wa kiutawala na kisiasa CCM ikiwa imeshazikwa.
Haya matatizo muyaonayo sasa ya viongozi kuiba mali na fedhs za umma na kufanya ufisadi uliokithiri, ukame, nchi kukosa umeme, ukosefu wa madawa na vifaa tiba kwenye hospitali zetu, maji, mikopo ya elimu ya juu na huduma zingine za kijamii yanayofungamanishwa na tatizo la nchi kukosa uongozi bora ni njia tu ya kuwaharibu watawala hawa japo ni kwa maumivu makali ya sisi wananchi.
Tuvumilieni jabo ni kwa kitambo kidogo tu. Nchi nyingine mpya ya Tanzania itazaliwa si kitambo kirefu. Niaminini mimi.
Wanaosema kuwa wananchi wa nchi hii ndiyo wajinga na mbumbumbu na wapole sana kwa kuwa tumeruhusu hali hii, hawajui wasemalo...!
Haya yameruhusiwa na Mungu mwenyewe. Mungu ameruhusu tuwe hivi. Mungu mwenyewe anadhibiti haya...
Nawakikishia jambo moja kuwa, kwa wakati mwafaka, Mungu ataachilia mwamko na ujasiri wa hatari kwa watu wake mpaka watawala watakuja kushangaa na watakimbia wasione hata pa kujificha nyuso zao....
Laiti CCM na serikali wanayoingoza wangekuwa na akili na maarifa, basi wangetengeneza mambo yao haraka, Mungu angeweza kuwasamehe na kuwarehemu...
Lakini kwa kuwa akili na ufahamu wao umefungwa ktk ubinafsi na ulafi, basi kama ni kufa, hakika na wafe tu maana hiyo ndiyo haki astahiliyo mjinga...
MUNGU HAWAHI NA WALA HUWA HACHELEWI
Nimemaliza. Usiku mwema kwa kila mtu.